Mawifi jamani, hivi wana nini?

Pretty

JF-Expert Member
Mar 19, 2009
2,575
552
Habari zenu wanaJF,
Hivi mawifi wana nini lakini? Natarajia kujitosa kwenye ndoa, lakini wifi ananiletea vituko mapema kabla ya kufika huko. Mama mkwe wangu ananipenda lakini wifi yangu maneno maneno.

Ana kazi na familia yake lakini bado tuu ananisema, eti anataka nimpigie magoti ninapomsalimia, anawaambia watu kaka yake anaoa binti wa mjini hawana heshima.
Hivi unapomsalimia mtu ukimpigia goti ndio heshima?

Wadada mliolewa hebu nipeni mbinu za kumdhibiti huyu wifi.
 
wifi yako ni dada ni mchaga wa rombo,kwa hiyo kwangu shaka ondoa!hutapiga magoti
 
heheheheh!i can see shemeji ON HIS WAY TO HEAVEN!
tumsifu yesu klistu shemeji...........
 
Hiyo ndio raha ya wachaga, hawamind mambo ya magoti. Huku ninakoenda magoti hao wanaona kama ndio heshima kwa msichana.
 
Milele Amina Shemeji. Naona mtoto Pretty anaogopa kupiga kagoto kumsalimia wifi. Watoto wa mjini bana! Nasubiri kipyenga kipulizwe nihitimishe safari ya kuingia Heaven. Mpwa naona bado kuamka.
 
Badilisha mawazo njoo kwetu. Hakuna makuu, Muulize shemeji yangu.
 
dah!
dada lake mimi kanda ya ziwa naona kushoto sana.watakuwa wanakuslap kila siku.kwanin usimalizane na chrispin?mim nimechukua changu mapema nyumbani kwao.na wewe nenda huko huko
 
Milele Amina Shemeji. Naona mtoto Pretty anaogopa kupiga kagoto kumsalimia wifi. Watoto wa mjini bana! Nasubiri kipyenga kipulizwe nihitimishe safari ya kuingia Heaven. Mpwa naona bado kuamka.

mpwa jana alikuwa chawote-bar.mimi nilipitiliza home,si unajua nilikwambia nina kazi fulani?
 
dah!
dada lake mimi kanda ya ziwa naona kushoto sana.watakuwa wanakuslap kila siku.kwanin usimalizane na chrispin?mim nimechukua changu mapema nyumbani kwao.na wewe nenda huko huko

Tatizo huyu mtoto mbishi. Huo ushauri nimempa mapeeema lakini kabisha. Inaelekea huyo msukuma habari yake si mchezo. Hahaha!
 
mpwa jana alikuwa chawote-bar.mimi nilipitiliza home,si unajua nilikwambia nina kazi fulani?

Nakumbuka shemeji. Na kale katripu kameota mbawa? Hiyo Cha wote lazima nitie timu siku moja. Inaelekea ina wahudumiaji viwango. Mpwa kapang'ang'ania sana hapo. Lazima kuna siri ya urembo pale.
 
Tatizo huyu mtoto mbishi. Huo ushauri nimempa mapeeema lakini kabisha. Inaelekea huyo msukuma habari yake si mchezo. Hahaha!
hehehe!wasukuma wana kitu kimoja kizuri sana na spesho wanawake wanakifurahia.WASUKUMA WANAJUA KUPENDA,WANAJUA KUKEA!na hamna mwanaume anakufa vibaya kwa mwanamke kama msukuma
 
Ulijuaje!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom