Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,653
Leo ningependa kuendelea kujadili jambo ambalo nimekuwa nikijadili kwa muda mrefu sana kuhusu maadili na nidhamu. Lakini leo nitajikita katika dhana yenyewe ya maadili na nidhamu na nitaongelea kidogo na mahusiano yake na kuendelea au kutokuendelea kwa taifa lolote.
Maadili ni kitu gani na nidhamu ni kitu gani na ni kwanini ni mambo muhimu sana ili taifa letu au taifa jingine lolote lile liendelee?
Neno maadili linatokana na neno '' Adili ''. Linahusiana sana na mwenendo wa binadamu. Adili maana yake kuenenda katika usahihi. Nidhamu na maadili vina mahusiano ya karibu sana. Huwezi kuwa muadilifu bila kuwa na nidhamu. Je nidhamu ni kitu gani?
Nidhamu ni uwezo wa akili kuongoza mawazo na matendo yake katika mkondo unaofaa ambao utakuwa na faida kwake na kwa jamii yake.
Kwa kawaida binadamu anawaza mamia ya mawazo kwa siku. Baadhi ya mawazo ni yenye faida na mazuri na baadhi ya mawazo ni mabaya. Kwa hakika ni mawazo yasiyofaa. Mawazo mabaya huzaa watu waovu na mawazo mema huzaa watu wema. Kwahiyo uwezo wa kujizuia na kuongoza mawazo yetu ndio kitu kinachoitwa nidhamu. Mtu asiyekuwa na uwezo huo ni mtu asiyekuwa na nidhamu.
Kwa mfano mwizi hawezi hatuwezi kumuita ni mtu mwenye nidhamu. Mtu anayetukana hatuwezi kumuita mtu mwenye nidhamu kwakuwa ameshindwa kuongoza mawazo yake katika mkondo unaofaa. Kwahiyo nidhamu ndiyo inayorekebisha tabia zetu. Nidhamu ni jeuri ya kushinda vishawishi na tamaa. Nidhamu hii humuongoza binadamu kuwa mtu mwema na mwenye faida kwa jamii na taifa.
Mahusiano yetu kama watu wa taifa hili yatajengwa kama tu tutakuwa na nidhamu na kudhibiti tabia zetu na mawazo yetu. Na kuelekeza tabia zetu na mawazo yetu katika mkondo unaofaa. Ili taifa hili liendelee nidhamu ni jambo la msingi sana. Hatuwezi kujenga taifa hili bila nidhamu na kiongozi yeyote asiyeongelea hili anawaongopea nchi hii haiwezi kutoka kwenye umaskini kama watu wake hawana nidhamu na maadili. Ni lazima tuangalie kwa ukaribu tabia za watu wetu.
Huo ni msingi wa kwanza wa taifa lolote lile imara na lenye akili. Hatutaweza kujenga familia imara au taifa imara pasipo nidhamu. Na mahusiano yetu kama watu wa taifa hili yatategemea sana nidhamu zetu. Hatutaweza kuheshimiana kama hatuna nidhamu. Hili jambo tunapaswa kulijenga kama taifa. Hatutaweza kufikia malengo yetu pasipo hili jambo kuzingatiwa.
Malengo yetu yeyote yale yawe ya muda mfupi au mrefu hatuta yafikia kama hatutajenga nidhamu, na elimu tunayotoa haitokuwa na faida kwa taifa hili. Kwahiyo ni lazima tujitolee kujenga taifa hili na tuwe na nidhamu. Nidhamu huleta dira. Naongea hili tena na tena sababu ni jambo muhimu. Ili watu wetu wawe na faida kwa taifa lao.
Kwahiyo tunatakiwa tubadili jinsi tunavyofikiri na tuongoze mawazo yetu katika mkondo unaofaa. Mawazo yeliyotawanyika hayawezi kuwa na faida. Kwahiyo ni lazima tuongoze mawazo yetu kwenye utaifa. Tukitambua kuwa tuna taifa ambalo kila mmoja wetu anapaswa kulijenga na kulipenda hatuna taifa jingine zaidi ya hili.
Tukiwa na nidhamu tutaweza kujenga mahusiano mazuri kati ya mtu na familia yake, mtu na majirani zake na mtaa wake na wilaya yake na taifa lake pia, Tujitoe ubinafsi tuuvae utaifa na tulpende taifa letu hiyo itakuwa hatua moja kubwa sana kwetu kuendelea.
Vyuo vyetu lazima vizalishe watu wenye nidhamu ya juu ambao wtakuwa chachu ya maendeleo yetu. Elimu yetu lazima iundwe ili kuwezesha taifa hili kusonga mbele. Kila mtu lazima atambue kuweka utaifa mbele ni heshima. Na umoja ni bora zaidi ya utengano na ubinafsi. Tunauwezo wa kujenga taifa zuri na kubwa. Tubadilishe tabia zetu sisi sote. Tubadilike na tutafute njia mpya ya kupita.
Lakini tuna bunge ambalo kazi yake ni kutunga sheria. Sheria hizi kazi yake ni ku shape behaviour za raia katika mkondo ambao tunadhani utakuwa na faida kwa taifa. Sheria hizi husaidia kujenga nidhamu za raia. Kama shule haikufanya kazi sawa sawa, kila sehemu ina kazi yake.
Bunge linapotunga sheria serikali inatakiwa ifanye enforcement. Kitu kimoja ambacho kinatufanya tushindwe kujenga raia wa namna hiyo ni kutokana na watu tunaowachagua kwenda bungeni na tunaowapa uongozi kuunda serikali. Haiwezekani serikali isiyokuwa na nidhamu ikajenga nidhamu kwa raia na utii wa sheria. Raia huvunja sheria wanapoona viongozi wakivunja sheria. Hapo ndipo tulipokwama. Sheria kama sheria ni nzuri kwa mustakabali wa taifa lolote lile kama ni zenye misingi ya haki.
Kwahiyo kushindwa kwa serikali kuondoa ufisadi ni matokeo ya kukosa nidhamu na uwajibikaji jambo hili madhara yake ni makubwa sana.
Jamii huparaganyisha na taifa kwa ujumla, na kufanya nchi kuwa ya makundi na magenge. Na ni chanzo cha kushindwa kwa utawala na utii wa sheria.
Raia wanapaswa kutii serikali yao lakini serikali inaposhindwa kusimamia sheria, raia wanakuwa sio watiifu kwa serikali yao. Na nchi inapokuwa na serikali isiyokuwa na nidhamu katika uendeshaji wake, inapokuwa na serikali ambayo haizuii rushwa na ufisadi sababu ya kutokuwa na nidhamu kwao hupelekea nchi kwenda shimoni.
kunapokosekana kushindwa kujizuia katika nchi na nidhamu, taifa haliwezi kuepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe. Nidhamu ni kujizuia. Kwahiyo tunaposhindwa kutumia akili na kufuata matamanio yetu ya mali na kufanya mali ni kitu cha kwanza kuliko utu wetu na utaifa wetu, hatuta epuka na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Sasa tunaona viongozi wengi wanaenda kwenye siasa kwaajili ya manufaa binafsi. Kuna tokea misuguano mingi. Ukiangalia kwa ukaribu hayo yote ni kwasababu ya tamaa ya wengi miongoni mwao. Wamelirarua na kuligawa taifa.
Tunapochagua kiongozi wa namna yeyote yule kuingia madarakana raia watafanana na serikali ya namna hiyo. Serikali ikikosa nidhamu nchi inakosa nidhamu. Ikiwa serikali ya uongo uongo na ulaghai na raia watafuata mkondo. Kuharibika na kuoza kwa taifa lolote kunatoka na aina ya viongozi wanaoingia madarakani. Ni wao wanaotunga sheria na sera na kuzisimamia. Kiongozi mwenye nidhamu na adili atafanya taifa kuwa na nidhamu na adili. Kama mimi ni kiongozi mwenye hekima nitataka raia wangu wote wawe na hekima sitacheka na ujinga.
Ni ukweli tunauhitaji wa kubadilisha serikali na hivyo kubadilisha mwelekeo wa taifa letu. Hili jambo ni la msingi sana. Lakini ni lazima tutafute watu bora miongoni mwetu ili kufanya hayo mabadiliko. Ukweli ni kwamba tunauwezo wa kufanya taifa hili kuwa kubwa. Nguvu hiyo iko mikononi mwetu. Lakini kama tu tutabadili mwelekeo wa mawazo yetu na tabia zetu. Kama tutaheshimu taifa hili na kulipenda na kuwa tayari kulitumikia.
LET US HONOR THIS COUNTRY ABOVE ALL OTHER NATION. WE GOT VALUE.
WHAT I DESIRE IS THE CHANGE NOT OF THE GOVERNMENT BUT CHANGE OF THE HEARTS TO THOSE PEOPLE WHO ARE IN GOVERNMENT AND TO ALL CITIZENS OF THIS COUNTRY. LAZIMA TUJE PAMOJA TUUNDE TAIFA MOJA. NA MUNGU ATAKUWA UPANDE WETU. MUNGU HAPENDI MGAWANYIKO. TAIFA MOJA CHINI YA MUNGU MMOJA.
Kama nembo yetu ya taifa inavyoonyesha mwanamke na mwanaume wakifanya kazi pamoja kujenga taifa hili. We must work together. ili taifa hili lisonge mbele bila ubinafsi najua tunaweza kama tukiamua. Hii nguvu iko ndani yetu kama tutajitoa kwa nguvu zetu zote na akili zetu zote. Najua una uwezo wa kulinyanyua taifa hili.
'' Taifa halijengwi kwa kuwa na maghorofa mengi au magari mengi. Taifa hujengwa katika mioyo na akili za watu na hubomolewa katika akili na mioyo ya watu. Hili pia ni sawa katika familia kuna familia zina mali lakini ndani hapakaliki. Ni wakati sasa wa kujenga taifa letu. Tutakapoanza kujenga taifa hili kwenye mioyo na akili za watu hakuna kurudi nyuma. Na uhakika tutashinda. Familia zitakuja pamoja na taifa litakuja pamoja. Hatutakuwa na furaha ya mtu mmoja au familia moja bali ya taifa zima. Tutapunguza kutokuwepo usawa katika nchi hii na maskini watafurahia. Siku ya ukombozi wa taifa hili itakuja haiko mbali. Ni katika ukweli na haki.''