Mawazo yetu yasiwe kwenywe siasa tu

Aug 10, 2011
81
9
ili inchi iwe na ustawi mzuri inahitaji siasa safi! Sawa lakini pamoja na hilo naona kama siasa inachukua ndio inachukua sehemu kubwa ya mawazo ya watu wengi mara uchaguzi ujao 2015, mara uchaguzi huu mara kiongozi huyu mambo ya kufanya yapo mengi nchi ili kujiletea maendeleo..my take!tunatakiwa kama jamii tujadiliane na kuibua mambo mengi zaidi ambayo yanaweza kusaidia jamii kuliko kila siku kuendekeza siasa..
 
huwezi kujadili suala lolote bila kuhusisha siasa kwa bahati mbaya sana nchi yetu wanasiasa ndio policy makers sio wataalam hivo siasa ndio zina shape hili taifa hivo huwezi kutenganisha siasa na uchumi au maendeleo
 
Kutokana na siasa mbaya za hapa TZ ndiyo maana watz wooooote wana maisha mabovu. Kama siasa ikitengemaa, Maisha nayo yatakuwa bomba ndipo tutapata fursa ya kuzungumzia vingine.

ONE THING AT A TIME.
 
ni ngumu kutengenesha siasa na maendeleo kama nchi kwakuwa politician ni policy maker hilo ni sawa..ndo maana nasema kuwa lazima tujadili vyote kwa pamoja siasa na mambo mengine kama tunawaachia wanasiasa wanatoa policy mbovu tunajadili miaka 5 halafu tunaendelea tena kuwaacha bila mkakati wowote ni kama hakuna tunachofanya!
 
Fikiria mtu hajihusishi kabisa na siasa, halafu Mabomu yametua na kutekeza biashara yake Gongo la mboto, na baadaye fidia analipwa elfu 70 kwa hasara ya milioni 5. Ataacha siasa ???.

Ipo mifano mingi inayowalazimu watu kuongelea siasa. Kifupi Uongozi mbovu unafanya watu muda wote wafikirie mbadala ! Uongozi ukiwa imara watu watazungumia maendeleo.
 
ili inchi iwe na ustawi mzuri inahitaji siasa safi! Sawa lakini pamoja na hilo naona kama siasa inachukua ndio inachukua sehemu kubwa ya mawazo ya watu wengi mara uchaguzi ujao 2015,mara uchaguzi huu,mara kiongozi huyu mambo ya kufanya yapo mengi nchi ili kujiletea maendeleo..my take!tunatakiwa kama jamii tujadiliane na kuibua mambo mengi zaidi ambayo yanaweza kusaidia jamii kuliko kila siku kuendekeza siasa..
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa hatuwezi kujenga nchi kwa kuwaachia wana siasa pekee ila ungetoa suggestion hata moja tufanyeje ingependeza zaidi.
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa hatuwezi kujenga nchi kwa kuwaachia wana siasa pekee ila ungetoa suggestion hata moja tufanyeje ingependeza zaidi.

Kalime kijijini kwenu na uwe mfano kwa wanakijiji, uwafundishe kuoga, kuvaa vizuri na kupika chakula kizuri/vizuri...

Maana nimetoka vijijini bara tatizo siyo pesa ila ni utamaduni wa kijima..ngombe 200 nyama mpaka ngombe afe aaagh!.
 
Back
Top Bottom