Mawazo yangu kuhusu ufisadi na suluhu yake

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Swali la kujiuliza tunawatayarishaje watu wetu kuingia kwenye ofisi za umma na katika utumishi wa umma? Tume wa train vipi watu wetu katika nidhamu zao na maadili. Binadamu hakui kama uyoga ni zao la makuzi na malezi katika familia yake, jamii yake na Taifa. Ni zao la elimu anayopewa shuleni na katika jamii inayomzunguka. Tunajifunza kwa kuona na kwa kusikia.

Tutarudishaje maadili katika ofisi za umma kama hatutazingatia malezi na makuzi ya watoto wetu? Tunachoangalia hapa ni kujenga tabia ambazo zitakuwa zenye manufaa kwa taifa letu. Na tabia za binadamu zilizobora huanza kujengwa mtoto akiwa mdogo.

Sheria ina nafasi yake lakini sheria hufanya kazi vyema kwa jamii inayojitambua na yenye maadili. Jamii ambayo haijitambui inahitaji elimu zaidi. Kwahiyo tunahitajika kufanya juhudi kutoa elimu zaidi kwa watu wetu juu ya utaifa. Ili hata kama tunaadhibu tunaadhibu watu wanaojitambua.

Kwahiyo kama tumekosea, tumekosea katika sehemu hizi. Na kama tunataka kurekebisha mambo ni muhimu kuangalia sehemu hizo pia.

Tukae tongee matatizo ambayo yanatukabili kama taifa yahusuyo maadili ya nchi yetu katika utumishi wa umma kisha tufikie muafaka kwa pamoja. Kwasababu tusipofikia muafaka kwa pamoja kuhusu kilichobora kwa taifa letu, hatutafika kama taifa. Mabadiliko ya kitabia yanahitajika kwetu sote. Na hakika hatutapata dira kama hatutakubali kubadilika wote na kufuata kilichobora kwetu.

Kwahiyo ni muhimu tukajua hili. Na tukawa tayari kurudisha uzalendo katika nchi yetu, ambao tayari umeanza kutoweka. Haya mambo yote yanahitaji kufikiri zaidi na busara ili kuyatatua na ili kujenga jamii zilizobora zenye umoja na zinazojitambua.

Na ili kujenga jamii ambayo kila mmoja ana timiza wajibu wake katika kujenga taifa imara na bora. Kuna msemo ambao ulikuwepo CHEO NI DHAMANA ni muhimu sana kujenga watu wetu katika fikra hizo. Unapopewa ofisi ya umma ujue umepewa jukumu la kufanya kazi kwaajili ya wengine na sio kwaajili yako binafsi. Na kutumia ofisi za umma kwa manufaa binafsi iwe dhambi kubwa ambayo mtu ataionea haya mbele ya macho ya jamii.

Kama tunataka kubadili taifa hili ni muhimu familia zetu na jamii kukubali kuwa tayari kubadilika na kulea watoto wetu vyema. Kwa wazazi kutimiza wajibu wao katika malezi. Ni lazima tuimarishe elimu yetu kuwa bora na yenye misingi bora ya kinidhamu na maadili . Taasisi za dini kutimiza wajibu wao kwa kuhubiri watu kuacha uovu na kumrudia Mungu na serikali kutimiza wajibu wake kwa kusimamia sheria na haki. Kama kote huko pameharibika hakuna jamii itakayojengeka ikawa bora kama juhudi hazitofanyika kuparudisha katika uhai wake. Ili kujenga jamii bora ambayo inachukia ufisadi ni muhimu kuzingatia mambo haya.

Kama mtoto wako anakuwa na utajiri usioeleweka na wewe mzazi unakaa kimya unawajibika na hali ya ufisadi uliotamalaki katika nchi yetu. Unajua fika kipato cha mtoto wako lakini unakaa kimya na kufurahia mapato haramu ambayo mtoto wako ameyapata kwa kuiibia jamii. Vile vile katika kanisa iweje hauulizi mtu anachangia kanisa na misikiti mamilioni ya fedha na ni mtumishi wa umma bila kuuliza kazitoa wapi? Kuna mambo ambayo tunapaswa kuyabadilisha kama jamii na ni zaidi ya kutumia nguvu. Mambo haya hayawezi kurekebishika kama hatutajua chanzo cha tatizo. Tunaweza tukafungua mahakama ya mafisadi na kufunga watu wengi lakini mambo yasikae sawa.

Ili kuondoa ufisadi katika nchi yetu tunahitajika kufanya kazi kwa pamoja. Tunahitajika kujua tunataka kwenda wapi kama nchi. Na kuwa tayari kujitolea kutumikia taifa letu kwa kila mtu kuwajibika ipasavyo katika eneo alilopo kwa uadilifu na kwa watumishi wa umma kujua cheo ni dhamana. Na kujua kwamba utajiri wa haraka haraka si salama kwao na kwa maendeleo ya taifa. Tunaweza kukusanya mapato mengi sana kama kila mtu akitimiza wajibu wake pasipo kusukumwa na kama mapato hayo yatatumiwa vizuri nchi yetu itafika mbali.

Lakini tabia nyingine zimetengenezwa na wanasiasa na watawala. Wanapotoa hongo kwa wananchi ili waingie madarakani kwa kupigiwa kura wanategemea kujenga wananchi wa namna gani? Unaingia kwa kutoa rushwa madarakani utawezaje kupambana na wala rushwa au kujenga jamii ambayo inayochukia rushwa wakati unaamini rushwa ndio njia pekee inayorahisisha mambo?

Hivyo hivyo kwa uongo na ulaghai. Viongozi wanapokuwa waongo na walaghai wananchi na watumishi wanafuata mkondo. Ni dhahiri tunahitaji mabadiliko katika taifa letu. Mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hasa ya kijamii na kisiasa , ya kiuchumi yatafuata yenyewe. Uchumi wa nchi yeyote ni zao la kazi na ili tuweze kuendelea ni lazima watu wetu wawe tayari kufanya kazi kwa uadilifu na kwa nidhamu.

Aristostle aliwahi kusema; Watu wote waliotafakari kuhusu utawala wa binadamu walikuja kufikia muafaka ya kwamba baadae ya taifa lolote inategemea sana jinsi gani jamii inalea, kukuza na kuelimisha vijana wake.''

Ni wazi kwamba tukiwaachia taifa hili vijana ambao hawakutiishwa katika nidhamu wakiwa watoto na wakati wakiwa vijana wakikua, watarivuruga. Kuendelea kwa taifa lolote kunahitaji nidhamu na utii wa sheria. Na vijana hawatotii sheria kama hakutakuwa na malezi bora pamoja na elimu.

Watakapopata nafasi katika utumishi wa umma hawatokuwa na nidhamu wala maadili. Na wakiwa wazee hawatokuwa na cha kuwafundisha vijana na watoto kuhusu nidhamu na maadili na matokeo yake kwa vizazi kadhaa tutakuwa na watu wasiokuwa na maadili na nidhamu. Ofisi za umma zitakuwa sehemu ya ufisadi na zisisokuwa na thamani machoni pa raia. Na uzalendo utatoweka kwasababu kila mtu atajifikiria mwenyewe badala ya jamii kwa ujumla wake. Hii yote inahitaji elimu kwa watu wetu kujua umuhimu wa taifa lao kwa maendeleo yetu wote ya leo na ya vizazi vijavyo.

Tusitibu ugonjwa tudhibiti ugonjwa usitokee kwa malezi bora yenye nidhamu na maadili , pamoja na elimu iliyoimara na bora, badala ya kusubiri ugonjwa utokee kisha mahakama na selo zetu zijae watu wahalifu na mafisadi. Na wahalifu na mafisadi wakizidi wataingia kwenye mifumo ya serikali yetu na vyama vyetu vya siasa na mwishoni watakuwa viongozi wetu. Uhalifu ukizidi hakuna sheria itakayofaa kuwafunga kamba watu kutenda katika usahihi. Kwasababu watakuwa wameingia kwenye mifumo ya serikali na ya maamuzi.

Vijana wetu watafungwa kamba dhidi ya tabia haribifu kwa malezi na elimu bora na kwa jamii kuwajibika kwa pamoja. Sheria zetu zitakuwa na maana kwa watu wenye maadili wanaoogopa kuzivunja na sio wahalifu ambao wamekomaa na wasiojali sheria. Ambao kutokana na malezi mabovu wamechipua na kukua na sasa wanazaa matunda. Tabia bora za binadamu hujengwa wakati mtoto akiwa mdogo tukishindwa huko tusitegemea matunda bora kutoka kwa vijana wetu.

Kwahiyo udhibiti unafaa katika familia zetu na katika jamii zinazotuzunguka kama tunataka kupambana na uhalifu kwakuwa wahalifu ni dada zetu na kaka zetu, majirani zetu na marafiki zetu.

Ni muhimu kujiuliza haya mambo yameanzaje? je Kuna wakati taifa letu lilikuwa na good order na sasa linavurugwa na wizi pamoja na ufisadi? Kuna wakati mambo yalikuwa yanaenda sawa katika ofisi zetu za umma na sasa yanaenda mrama? Tunahitaji kutafakari yote haya kama wasomi na kama tunataka kujenga jamii iliyobora. Kwasababu ukiwa msomi hutakiwi kujifikiria mwenyewe. Kuna wakati itabidi ufikirie majaliwa ya taifa lako, jamii yako lakini pia majaliwa yako mwenyewe. Tunaishi kipindi kifupi sana hapa duniani , lakini tunatumaini kama wasomi, tutakapokufa tuiache jamii yetu ikiwa bora kwaajili ya umoja na maendeleo ya watoto wetu.

Ni mawazo yetu ambayo hujenga taifa letu. Sasa inategemea sana kama mawazo yetu ni bora na chanya au mawazo yetu ni ya hovyo. Ni wapi tunapoelekeza mawazo yetu? Majaliwa yetu kama taifa yanategemea mawazo yetu na matendo yetu tunaelekeza wapi. Je ni katika kujenga familia zetu, jamii zetu na taifa letu ? Au ni katika masuala ya kipumbavu na kijinga? Tujichambue kama taifa kisha tutafute njia ya kufanya mapito yetu kwa pamoja kama taifa. Ili tuendelee kama taifa kuna baadhi ya tabia lazima tuziache ambazo hazina manufaa kwetu. Tujenge jamii inayopenda kufanya kazi na kujifunza kila wakati. Ni katika kupata maarifa ndipo tutakapoendelea hakuna kuendelea pasipo maarifa. Ni muhimu kwetu sisi kutafuta uelewa na kukuza uelewa wetu. Kinachotofautisha jamii iliyoendelea na isiyoendelea ni maarifa waliyonayo.

Naomba niongeze maneno mengine kutoka kwa Edmund Burke ; Mwanafalsafa na statesman wa uingereza kuhusu jamii za binadamu, civilization na nidhamu. Ameongelea mambo ya muhimu sana katika kujenga jamii bora.

'' Uhuru ni nini bila ya maadili? Ni miongoni mwa uovu mkubwa. Uendewazimu usio na mipaka. Binadamu wanastahili uhuru katika jamii ikiwa tu wakiwa na nidhamu. Ikiwa tu wakiwa na uwezo wa kuwa na nidhamu ya kudhibiti matamanio yao. Bila ya hivyo jamii haiwezi kuwepo. Hadi kuwepo na nguvu inayodhibiti matamanio yao kutoka ndani yao na kutoka nje.''

Haya ni maneno ya rais wa pili wa marekani akiongelea kuhusu katiba na maadili ya taifa;


"We have no government armed with power capable of contending with human passions unbridled by morality and religion. Avarice, ambition, revenge, or gallantry, would break the strongest cords of our Constitution as a whale goes through a net... Our Constitution was made only for a moral and religious people. It is wholly inadequate to the government of any other."

John Adams.
 
Back
Top Bottom