Mawaziri watendaji wapya kumjengea heshima kubwa Rais Kikwete

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,575
31,888
Wanabodi JF,
Baada ya Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utoh na zili za Kamati za Kudumu za Bunge kwa wizara zilizofanya ubadhirifu wa mali za umma, na kushinikizwa na wabunge kuachia ngazi.

Rais Kikwete karidhia kufanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri kulisuka upya, na kuwawajibisha watendaji wengine wakiwemo makatibu wakuu, wakurugenzi wa mashirika ya umma na wakuu wa idara mbali mbali za serikali waliotajwa katika ripoti ya(CAG ).

Hii ni heshima kwa serikali ya Kikwete kukubali kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na kujipanga kuchagua mawaziri watendaji ambao watamjengea heshima Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa habari zilizo rasmi wanaotakiwa kuachia nafasi zao ni George Mkuchika, Dr Haji Mponda, Ezekiel Maige, Prof Jumanne, Cyril Chami, Mustafa Mkullo, Wiliam Ngeleja, Omari Nundu, na Manaibu wao.
 
...what is this ?
Kumjengea heshima gani wakati yy ndo shina la matatizo ?

Matanuzi ya safari za nje za kujitangaza as if yy ni miss universe yanakula hela nyingi sana na hasa wapambe wasio na tija yoyote na maisha bora ya kila mtanganyika !

Soon again, huyoooo USA... kufuatilia kwa nn Ngasa hakununuliwa na Seatle Saunders !!!
 
Wanabodi JF,
Baada ya Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utoh na zili za Kamati za Kudumu za Bunge kwa wizara zilizofanya ubadhirifu wa mali za umma, na kushinikizwa na wabunge kuachia ngazi.

Rais Kikwete karidhia kufanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri kulisuka upya, na kuwawajibisha watendaji wengine wakiwemo makatibu wakuu, wakurugenzi wa mashirika ya umma na wakuu wa idara mbali mbali za serikali waliotajwa katika ripoti ya(CAG ).

Hii ni heshima kwa serikali ya Kikwete kukubali kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na kujipanga kuchagua mawaziri watendaji ambao watamjengea heshima Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa habari zilizo rasmi wanaotakiwa kuachia nafasi zao ni George Mkuchika, Dr Haji Mponda, Ezekiel Maige, Prof Jumanne, Cyril Chami, Mustafa Mkullo, Wiliam Ngeleja, Omari Nundu, na Manaibu wao.

May be I am missing something? What is the issue here? Kama umekosa cha kuandika kaa kimya na usome topic za wenzako kama mimi!!!!!

Tiba
 
this is not a thread .... dam low level think tank .... there is no any substantial theme on this thread

empty recycle bin
 
ritz sina nia ya kupingana na wewe ila naomba kuuliza; hiyo ripoti ya CAG iliyozua mambo bungeni Mh. Raisi hakukabidhiwa tokea April 2011? Toka akabidhiwe na mpaka mjadala kuja Bungeni siyo mwaka sasa na hao wabovu bado wapo madarakani? Mshaurini Mh Raisi awe na mshauri wa masuali ya taarifa za fedha na usimamizi wa fedha za umma kwani inawezekana alivyokabidhiwa ripotu hakujua ukubwa wa matatizo yaliyoelezwa kwenye taarifa lakini angechambuliwa na mshauri wake......
 
Last edited by a moderator:
Kama Kikwete yuko madarakani karibu miaka minane na hajajijengea heshima hii miaka miwili iliyobaki itasaidia kitu gani zaidi ya kupanic. Ni sawa na mtahiniwa anapoambiwa 15 minutes left, kama ni mwanafunzi mwelevu muda huo si wa kuanza swali jipya concentrate kwa yale uliyoanza.

Nikiangalia Kikwete hana chochote alichoanza cha kutuachia kama legacy yake zaidi ya Katiba mpya ambayo hata yenyewe kuna hatihati kama ataiweza. Uchumi umemshinda, maisha bora hayawezi tena kwa muda huu uliobaki.

Kama rais asipokuwa mwangalifu hili baraza la lala salama ndilo litakalompeleka kaburini kwa pressure, kwa vile mawaziri wanajua hawana muda wa kupoteza kujichukulia chao mapema na ikizingatiwa kuwa destiny ya CCM iko kwenye uncertainty situation.
 
Always postmotum. Mnaweza kuandamana kama mlivyo wendawazimu. ni wajibu wenu kudanganywa kama majuha. where was he to let all these fu****kin deseases. He is fig president ever.
 
Katika hotuba yake ya mei mosi leo JK badala ya kutueleza hatua alizochukua analialia ili tumuonee huruma kwa kuwa eti yeye ndiye aliyeagiza taarifa ya CAG iwekwe hadharani na kujadiliwa bungeni!
 
Nilipoteza na Imani na CCM zamani. JK kabadilisha mawaziri mara nyingi tu, sijaona lolote. Hakuna msafi pale. Mfumo ni ovyo. Mfumo wa NDIO MZEE na kuumbuana tu ndio umejaa
 
Wanabodi JF,
Baada ya Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utoh na zili za Kamati za Kudumu za Bunge kwa wizara zilizofanya ubadhirifu wa mali za umma, na kushinikizwa na wabunge kuachia ngazi.

Rais Kikwete karidhia kufanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri kulisuka upya, na kuwawajibisha watendaji wengine wakiwemo makatibu wakuu, wakurugenzi wa mashirika ya umma na wakuu wa idara mbali mbali za serikali waliotajwa katika ripoti ya(CAG ).

Hii ni heshima kwa serikali ya Kikwete kukubali kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na kujipanga kuchagua mawaziri watendaji ambao watamjengea heshima Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa habari zilizo rasmi wanaotakiwa kuachia nafasi zao ni George Mkuchika, Dr Haji Mponda, Ezekiel Maige, Prof Jumanne, Cyril Chami, Mustafa Mkullo, Wiliam Ngeleja, Omari Nundu, na Manaibu wao.

mkuu kumbe na wewe unaandikaga pumba?!
 
Ritz unaongea habari za kufikirika.

JK ni dhaifu na hana uwezo wa kuongoza. Mambo yatakuwa yaleyale kama hatajilazimisha kuwa mkali na mtu makini. Halafu tatizo lake mvivu wa kusoma hizo ripoti
 
Mkuu ritz,

Hata mimi naona hilo, ila kuna tatizo la udhaifu wa sheria! tukiweka watendaji wapya na kuboresha sheria zetu kila kitu

kitakuwa ndani ya mstari.
 
Wewe Ritz ni bingwa wa kuropoka mambo ya ovyo. Hivi unategemea tuchangie nini kwenye hoja hii..Sidhani nina muda wa kupoteza kujadili upuuzi kama huu. Eti nini????
 
Katika hotuba yake ya mei mosi leo JK badala ya kutueleza hatua alizochukua analialia ili tumuonee huruma kwa kuwa eti yeye ndiye aliyeagiza taarifa ya CAG iwekwe hadharani na kujadiliwa bungeni!
Ushabiki haujengi, in short kubalini kafanikisha ht mbumbumbu acyependa siasa anajua kilichotokea serikalini. Kabla ya hapo mbona mlikua hamhoji na possibly hamkujua nini kilikuwa kinaendelea.
Mpongezeni anapofaa kupongezwa na mkandieni anapofaa kukandiwa na si kila analosema ni baya, NO!
Binafsi nampongeza...
 
Kwa mfumo wa serikali ya Tanzania hata akodi Malaika toka kwa MUNGU wawe mawaziri wa nchi hii hawawezi kuleta 'IMPACT KIMAENDELEO' asikudanganye mtu sidhani kama Ubadhilifu uliotokea katika Halmashauri, Mashirika ya Umma na Mawizarani JK hana habari??? ana vyombo kibao vinamripotia nadhani TATIZO LA WIZI NA HUJUMA ZA TAIFA HILI NI MTANDAO NA UNA BARAKA ZA VIGOGO. Ndio maana hata mawaziri wana viburi. UKIINGIA KATIKA MFUMO WA UTENDAJI WA TAIFA LETU USIPOKUWA MWIZI UNAANGALIWA KWA JICHO NA KAULI YA 'HUYU SI MWENZETU NA SI MZALENDO' hata maisha yako yanakuwa masakani. Kwa hiyo sidhani kama wataleta Mabadiliko.
 
Mkuu
Baba yenu anasubiri kujengewa heshima na watu wengine wakati yeye mwenyewe ana doa ambalo ameosha hadi na mafuta ya break halitoki!!

Ajijengee kwanza heshima yeye mwenyewe ndio watu wengine wanaweza mjengea pia!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom