Peasant
JF-Expert Member
- Sep 27, 2007
- 3,949
- 687
Hivi huwa najiuliza kwa nini mawaziri wasukuma wanakuwa waadilifu kwenye kazi zao wakitumikia serikali ipasavyo na kusahau majimbo yao?
Kwa nini hawatumii nafasi yao kuleta maendeleo majimboni? Utaona kama waziri Ngeleja yupo nishati na madini lakini miaka mitano ishapita kule kwao sengerema hata kusogeza umeme kidogo vijijini ameshindwa? kuna miji inakuwa sana kule mfano kutoka sengerema kuna nyehunge, nzela .katwe , kahunda kwa nini mawaziri wameshindwa kupeleka umeme kule wakati miji imepanuka imekuwa mikubwa kuliko hata sengerema mjini yenyewe?
Nilienda kikazi huko nilishangaa kama mbunge wao ni waziri wa nishati na madini. na ni hivyohivyo kwa hata aliyepita. hawaoni wenzao wa kilimanjaro umeme mpaka vijijini?
kwa kweli wana JF naomba kuwakilisha mada
Kweli kabisa ila mbona mawaziri wa kilimanjaro na kwingineko wameweza kufanya maendeleo huku wakiendelea kumtumia mwajiri wao. mtu akitoka vijijini moshi akaja mjini hashangai umeme wala bomba la maji ngoja atokee huko mamwanza na masengerema
Rafiki mimi ni msukuma lakini naomba kutofautiana na wewe kidogo. Mawaziri wasukuma sio wote ambao ni waadilifu. Mfano Chenge huyu ni mwizi na mtovu wa nidhamu wa hali ya juu na wote tunajua hilo. Maghufuli japo si kwa 100 % ana nafuu na kazi zake zinaonekana na huko kwao kawapelekea barabara nzuri sijui mengine. Ngeleja sioni uadilifu wake hata kidogo zaidi ya kuwepo pale wizarani kuendesha miradi ya bosi wake Rostam Azizi aliyempa Ubunge na huo uwaziri. Maige sina data zake kamili.
halafu kama mnachunguza vizuri sio Ngeleja tu anaharibu hata wenzake waliotangulia! kama Chenge alishiriki kuwapora Wasukuma wenzake ardhi yenye rasilimali ya madini kuwapa wawekezaji kwa mikataba isiyo na manufaa akiwa kama Mwanasheria Mkuu! Pia akiwa kama Waziri wa Miundo Mbinu Chenge huyo huyo alishiriki pia kuiuza TRL kwa kampuni ya kilaghai ya Rites zaidi ya hapo akagonga Wasukuma wenzake na gari sasa hatujui kama alitumwa maana alilipa laki mbili kama faini akaachiliwa! cha ajabu zaidi akashinda Ubunge kwa kishindo! Mbali ya hayo ukiacha ndg zetu Wasukuma hata wenzetu Nshomile hawako nyuma kuna wakina Karamagi pia walileta TICTs na mikataba ya kifisadi ya kusaini hotelini ughaibuni! Ukiachilia mbali ukweli usiofichika kuwa wako kwenye sehemu nyeti sasa katika serikali hii ya Kikwete yaani Ukatibu Mkuu na Ukurugenzi, utendaji wao na elimu zao ni tofauti yaani elimu inawekwa pembeni inabaki kulamba makalio ya mafisadi na kushibisha matumbo!
Angalia type ya Silver Rweyemamu, na Mkandara hapo UD! Pia watu kama mama Mongela amekuwa Mbunge miaka nenda miaka rudi hamna cha maana alichofanya huko Ukerewe na mavyeo yoote aliyopata kuwa nayo! Mpaka najiuliza hawa watu na kuelimika kote, tatizo ni nini haswa? hawana uchungu na nchi hii? walio wasafi toka mitaa hiyo ni Dr Magufuli na Prof. Tibaijuka (ambaye yeye bado tunampima) tu! Jamani mnatuaibisha! wenzetu wa Kilimanjaro hawana shida kama sisi, isitoshe hata wakiiba huwakumbuka wapiga kura wao (mf. Mramba, pia kumbukeni Msuya, Mama Malecela, Dr Mathayo anasaidia sasa huko Upareni)! pia kumbukeni Mzee wa Kiraracha naskia alipelekaga barabara kwao alipokuwa waziri wa mambo ya ndani ukiachia mbali kuishikisha adabu polisi! Mbali na hayo hata watu wa Mbeya wanatuacha mbaali sana! angalia wakina Prof. Mwakyusa na wenzie walivyopigania mpaka uwanja wa Songwe unajengwa! hospitali ya Mbeya pia imeboreshwa na mambo chungu nzima ya maendeleo! Sie wa lake Victoria tumelogwa!
kwa kweli ni kurogwa na mganga kafariki. nimeshangaa sana, anashindwa nini kutumia madaraka aliyonayo kuweka umeme hasa kwenye miji inayokua kwa kasi vile?
Mbona nasikia huko usukumani kuna bonge la jiji linaitwa Gamboshi, limeendelea kama New York! Mbunge wa Gamboshi ni nani? Anastahili kuigwa, lol :clap2::clap2: