Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri Wapishana Kwa Waganga wa Kienyeji

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Ndallo, May 2, 2012.

  1. Ndallo

    Ndallo JF-Expert Member

    #1
    May 2, 2012
    Joined: Oct 1, 2010
    Messages: 6,725
    Likes Received: 430
    Trophy Points: 180
    Kuelekea kwenye kulisubiri baraza jipya la mawaziri hapa Tanzania ni kua sasa hivi ikiwa ni matumbo joto kwa mawaziri kutokujua hatima yao kama kuna watakao kuwepo au kutokuwepo kwenye baraza hili jipya, ni kua sasa hivi baadhi ya Mawaziri wameonekana kupishana kwa waganga wa kienyeji kutafuta tiba mbadala kuwanusuru na fagio hilo la chuma, hata mwenyekiti wa waganga wa kienyeji Tanzania alipoulizwa alikiri hilo na kudai kua wateja wao wakubwa ni mawaziri na mwenyekiti huyo amelalamika kua kuna baadhi ya mawaziri wamekua wanakwenda mikono nyuma kuomba tiba na wakishapatiwa tiba hizo mbadala na kufanikiwa huwa hawarudi kutoa fadhilia amelalamika mwenyekiti huyo wa waganga wa kienyeji Tanzania!

    Hii nimeamini sasa kua hata kule kwa waganga wanapopatiwa tiba hizo pia wanarusha je maendeleo kwa wananchi???

    Souce: Vyanzo vya habari magazetini leo.
     
  2. s

    sawabho JF-Expert Member

    #2
    May 2, 2012
    Joined: Feb 25, 2011
    Messages: 4,087
    Likes Received: 454
    Trophy Points: 180
    Picha wakiwa huko, tafadhali. Vinginevyo, mimi binafsi siamini hizi lugha za kutaka kuongeza mauzo ya magazeti.
     
  3. m

    mgeni wenu JF-Expert Member

    #3
    May 2, 2012
    Joined: Jan 2, 2012
    Messages: 3,670
    Likes Received: 613
    Trophy Points: 280
    Maji marefu aliwahikukiri hilo kuwa Wabunge wengi na mawaziri waliingia kwa juhudi zake
     
  4. DOUGLAS SALLU

    DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

    #4
    May 2, 2012
    Joined: Nov 13, 2009
    Messages: 6,757
    Likes Received: 875
    Trophy Points: 280
    Kwani siku hizi hawamuamini maji marefu tena?
     
  5. Ndahani

    Ndahani JF-Expert Member

    #5
    May 2, 2012
    Joined: Jun 3, 2008
    Messages: 11,455
    Likes Received: 106
    Trophy Points: 160
    Haya bwana...ndo utajiri wa waafrika huo. Hata economic consultancy tunapewa na "wataalamu".
     
  6. Ta Kamugisha

    Ta Kamugisha JF-Expert Member

    #6
    May 2, 2012
    Joined: May 17, 2011
    Messages: 2,436
    Likes Received: 361
    Trophy Points: 180
    Tupe majina au hacha majungu na umbea wa kike kike hapa
     
  7. Ndallo

    Ndallo JF-Expert Member

    #7
    May 2, 2012
    Joined: Oct 1, 2010
    Messages: 6,725
    Likes Received: 430
    Trophy Points: 180
    Maji Marefu uganga wake umeshaExpire!
     
  8. Gwalihenzi

    Gwalihenzi JF-Expert Member

    #8
    May 2, 2012
    Joined: Oct 21, 2011
    Messages: 5,066
    Likes Received: 9
    Trophy Points: 135
    ungekuwa umbea wa kiume ungeupokea?
     
  9. Kijana leo

    Kijana leo JF-Expert Member

    #9
    May 2, 2012
    Joined: Apr 6, 2012
    Messages: 2,851
    Likes Received: 12
    Trophy Points: 135
    Habari kama hizi uwe unaweka picha ili 2amini, coz ni ishu za imani, mbona wakiwa makanisani na msikitini wanaoneshwa? Icje kuwa porojo za magazeti kuuza.
     
  10. B

    Baba Collins JF-Expert Member

    #10
    May 2, 2012
    Joined: Sep 24, 2011
    Messages: 492
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 0
    Huwezi kuamini mkuu kwa kuwa wewe si mmoja wa wale wanaoutaka huo uwaziri!
     
  11. Mamndenyi

    Mamndenyi JF-Expert Member

    #11
    May 2, 2012
    Joined: Apr 11, 2011
    Messages: 27,026
    Likes Received: 1,602
    Trophy Points: 280
    Waje kwangu niwaombee ni bure hakuna garama na 100% ushindi.
     
  12. chitambikwa

    chitambikwa JF-Expert Member

    #12
    May 2, 2012
    Joined: Nov 8, 2010
    Messages: 3,932
    Likes Received: 3
    Trophy Points: 0
    huwezi kumtenganisha Mwafrika na imani za uchawi ,waisraeli tu wameweza
     
  13. b

    barakandesambur Member

    #13
    May 2, 2012
    Joined: Jan 17, 2011
    Messages: 20
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    khe makubwa kumbe uongozi mpaka kwa mganga
     
  14. S

    SokoroDar Member

    #14
    May 2, 2012
    Joined: Nov 16, 2011
    Messages: 39
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Hii habari ilipashwa kuchapishwa kwenye magazeti ya udaku sio hapa
     
  15. kongomboli

    kongomboli Senior Member

    #15
    May 2, 2012
    Joined: Apr 11, 2011
    Messages: 154
    Likes Received: 7
    Trophy Points: 35
    mi naona tayari dawa zao zishafanya kazi manake sisikii ata sioni dalili ya kusomwa kwa baraza la mawaziri
     
  16. Az 89

    Az 89 JF-Expert Member

    #16
    May 2, 2012
    Joined: Nov 20, 2011
    Messages: 1,549
    Likes Received: 31
    Trophy Points: 145
    Peleka facebook!
     
  17. Amoeba

    Amoeba JF-Expert Member

    #17
    May 2, 2012
    Joined: Aug 20, 2009
    Messages: 3,329
    Likes Received: 50
    Trophy Points: 0
    Huko ndiko alikoitoa, ameona aibu tu kusema chanzo kuwa ni gazeti la UWAZI!:bored:
     
  18. O

    Ogah JF-Expert Member

    #18
    May 2, 2012
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 6,188
    Likes Received: 12
    Trophy Points: 135
    Kwani "upepo" si ulishapita...........sasa hivi watu macho yako kwenye kesi za uchaguzi........Mawaziri wala msiwe na wasiwasi.........endeleeni kutafuna nchi..........
     
  19. Kiganyi

    Kiganyi JF-Expert Member

    #19
    May 2, 2012
    Joined: Apr 30, 2012
    Messages: 1,244
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 0
    Kweli mkuu cheki hii


    [​IMG]
    Chifu Kiongozi wa Kabila la Kisafwa Bwana Roketi Mwanshinga(Kulia) akiongoza jopo la Machifu kuweka tambiko la kukemea vitendo vinavyohusisha na Imani za kishirikiana katika Shule tatu za Msingi katika Kata ya Itenzi.

    [​IMG][​IMG]
    Chifu Kiongozi wa Kabila la Kisafwa Bwana Roketi Mwanshinga(pichani kushoto ) akiongoza jopo la Machifu kuweka tambiko la kukemea vitendo vinavyohusisha na Imani za kishirikiana katika Shule tatu za Msingi katika Kata ya Itenzi na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Tambukareli (pichani kulia) .
    [​IMG]
    Machifu wakiingia katika Ofisi ya Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi ya Tambukarelikufanya tambiko la kukemea vitendo viovu vinavohusishwa na Imani za kishirikina katika Shule tatu za Msingi, zilizopo Kata ya Itenzi.
    [​IMG]
    Machifu wakiingia katika madarasa na kufanya tambiko la kukemea vitendo viovu vinavohusishwa na Imani za kishirikina katika Shule tatu za Msingi, zilizopo Kata ya Itenzi.
    [​IMG]
    Wanafunzi wa Shule ya Msingi Igombe wakiwasikiliza Machifu licha ya mvua kubwa iliyokua ikiendelea kunyesha, katika zoezi la tambiko la kukemea vitendo viovu vinavyohusishwa na Imani za kishirikina.
    [​IMG]
    Wananchi waliojitokeza kutoka Kata ya Itenzi katika zoezi la Machifu waliofika katani hapo kutambika kwa lengo la kukemea vitendo viovu vinavyohusishwa na Imani za kishirikina.
    *****
    Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
    Machifu wa kabila la Kisafwa Mkoani Mbeya waliamuru kusitishwa kwa masomo kwa siku moja katika Kata ya Itenzi Jijini Mbeya, kutokana na wanafunzi wa jinsia ya kike kuanguka, kupoteza fahamu na kuwanyong'oshesha nguvu.    Tukio hilo limehusisha Shule za msingi za Gombe, Tambukareli na Mwasote, zoezi lililofanya na Chifu kiongozi wa kabila hilo Roketi Mwanshinga, akisaidiana na zaidi ya mchifu 30.    Pia zoezi hilo limehudhuriwa na Diwani wa Kata ya Itenzi Mheshimiwa Frank Mayemba na Askari wa Jeshi la Polisi na Ulinzi shirikishi L.M Kiyeyeu Aprili 2 mwaka huu.    Kabla ya kuanza kazi hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wananchi wanaozizunguka shule hizo, Chifu Mwanshinga alishusha lawama kwa Wachungaji wa madhehebu na makanisa mbalimbali Mkoani hapa, kutokana na kupokea waumini kwa kivuli cha kuokoka bila kuwauliza machifu.    Amesema kwani wao wanafahamu hawajaacha tabia zao za awali ndio maana vitendo hivi vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku huku makanisa hayo yakichipuka kama uyoga.    Chifu Mwanshinga ameenda mbali zaidi kwa kusema daima maisha yao ni duni, hivyo hufanya vitendo hivyo kwa nia ya kujipatia pesa wanajidanganya kwani pesa hupatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo.    Mkusanyiko huo umefanyika baada ya watoto wanaosoma katika shule hiyo hususani wasichana darasa la tano ndio wanaoathirika zaidi na ugonjwa wa kuanguka na kupoteza fahamu na kuwanyong'onyesha nguvu na hivyo kushindwa kuendelea na masomo na kuwapeleka nyumbani kwao.    Katika mkutanoi huo Machifu wameagiza yeyote anyejihusisha na masuala hayo aache mara moja na kutoa onyo yeyote atakayekaidi agizo hilo atatembea barabarani akiwa kichaa.    Aidha katika hali ya kusafisha mazingira hayo machifu wote walipita katika madarasa yote ya shule zote tatu na kwamba kuanzia sasa watapiga kambi kwa muda wa juma moja hatimaye kukomesha kabisa vitendo hivyo ambavyo huathiri huduma za maendeleo ya elimu na kiuchumi mkoani hapa.    Kutokana na kukerwa na suala hili machifu wameagiza wazazi wote wakeshe kwenye shule hizo ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.    Kwa upande wake pia Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Bwana Deusdedit Maseke amewashukuru wazazi kwa kuitikia wito wa kufika shuleni hapo na kuonesha jinsi walivyokerwa na jambo hilo.    Shule kadhaa mkoani Mbeya zimekubwa na janga la ushirikina na kupelekea kufungwa kutokana na vitendo vya kishirikina ikiwemo Shule ya Juhudi iliyopo kata ya Iganzo ambapo Ofisi ya Mwalimu Mkuu alisilibwa kinyesi pamoja na ofisi nyingine ya walimu mbali ya kusilibwa kinyesi vyombo vya chakula vilitapakaa kinyesi.

    [​IMG]


     
Loading...