Mawaziri wanaongoza kwa wizi serikalini - Deo Filikunjombe

EWE Mungu kila lililo chini jua macho yako yanaona, endelea kuweka mambo hadharani ili kila aliyekuwa akifanya kwa siri yajulikane. ndio wewe usie sinzia wakati wa usiku. Endelea kuwapa ulinzi watu wako ili waseme kweli, kwa kuwa hiyo kweli itatuweka kuwa huru.
 
Lukuvi alitaka kuchafua hali ya hewa alimnukuu vibaya filikunjombe na Fnjombe akamuumbua kwamba sijasema mawaziri wote bali mawaziri wengi ni wezi na ushaidi ninao

Tatizo la Lukuvi ni kilaza na amepewa nafasi hii kwa upendeleo baada ya mke wake Gemina Lukuvi kumbembeleza sana JK amsaidie mume wake.
 
hao mawaziri wanalindana what does he need kuthibitisha ambacho CAG hajaonyesha in his report!!! Woooote waizi waizi tu!!!
 
dWAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, sasa
yuko katika hatari ya kuondolewa
madarakani kwa kupigiwa kura ya
kutokuwa na imani naye kufuatia
tuhuma nzito za ubadhirifu wa fedha za
umma unaodaiwa kuwahusisha
mawaziri watano wakiongozwa na
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo.
Akiwasilisha majumuisho ya Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Mashirika ya
Umma, mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto
Kabwe, aliliambia Bunge kuwa kuanzia
leo wataanza kukusanya saini za
wabunge wenye nia ya kupiga kura hiyo
na kwamba uamuzi wake utawasilishwa
bungeni Jumatatu wiki ijayo.
Mwenyekiti huyo alisema ikiwa mawaziri
hao ambao hata hivyo hakuwataja
majina mmoja baada ya mwingine
hawatakuwa wamejiuzulu wenyewe
hadi kufikia siku hiyo, basi wabunge
watamwondoa Pinda madarakani kwa
kumpigia kura ya kutokuwa na imani
naye.
Kwa hali hiyo, Zitto alisema kuwa
itakuwa ni jukumu la mawaziri hao
kabla ya Jumatatu wiki ijayo kuamua
wenyewe kujiuzulu au kumwacha waziri
mkuu atimuliwe.
Hatua hiyo ya Zitto ilitokana na hoja
iliyokuwa imetolewa mapema na
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu (CHADEMA), ambaye aliwataka
wenyeviti wa kamati za Bunge wakati
watakapokuwa wanajumuisha hoja zao
kupendekeza kupiga kura ya kutokuwa
na imani na waziri mkuu Pinda ikiwa
mawaziri wake hawatakuwa
wamejiuzulu wenyewe.
Lissu alisema wakati wa kupiga kelele
umekwisha, na sasa wanachotakiwa ni
kuchukua hatua, kwani mamlaka hiyo
wanayo kwa mujibu wa Katiba.
“Waziri Mkuu wajibika kwa madudu ya
serikali. Nitaomba wenyeviti wa kamati
hizi wanapomalizia mjadala huu
kupendekeza kura ya kutokuwa na
imani na waziri mkuu kwa kujenga
mfumo wa siasa wa udokozi. Tukifanya
hivyo wananchi watatuamini. Ninyi
chama tawala ndio mnaosababisha
haya kama mtatumia wingi wenu
sawasawa tutafanikiwa, sisi tupo
wachache.
“Badala ya kupiga makofi, chukua hatua
kwa uozo huu. Mkifanya hivyo
mtaheshimika na msipofanya hivyo
mtaingia kwenye vitabu vya historia,”
alisema.
Alisema masuala ya ufisadi yamekuwa
yakizungumzwa na zaidi ya miaka 10
sasa, lakini hawajawahi kuona serikali
ikichukua hatua.
“Wakati kila mwaka CAG anatuletea
taarifa za wizi, hatujawahi kuona serikali
ikichukua hatua dhidi ya wahusika.
Hatujawahi kuona mtendaji
amechukuliwa hatua wala waziri
kuwajibika katika hili. Watu wanapata
kupata nafasi za uwaziri ili kuhujumu
nchi,” alisema na kuongeza mfumo
uliopo ni wa kulinda wezi.
Tanzania sio ya CCM
Akichangia mjadala huo, asubuhi na pia
jioni, Mbunge wa Ludewa Deo
Filikunjombe (CCM) aliwafyatua
mawaziri kadhaa akisema kuwa
wanaongoza kwa kutafuna pesa za
Watanzania na kumtaja Waziri wa Fedha
Mustafa Mkullo kuwa kinara wa wizi
huo.
Mbunge huyo alisema baadhi ya
mawaziri wamegeuka kuwa mchwa
wanaotafuta fedha za Watanzania bila
woga na kuongeza kuwa sasa umefika
wakati kwa wabunge kuweka tofauti za
kisiasa pembeni na kuzungumza kwa
umoja masuala yanayoliangamiza taifa,
na katika hilo akadai kuwa hatakuwa
tayari kuwaachia mawaziri wachache
waangamize nchi.
“Mheshimiwa Naibu Spika, inashangaza
na kusikitisha kuwa nchi inatafunwa.
Wanaofanya haya ni mawaziri wetu.
Nchi inakufa na tuelewe kuwa Tanzania
sio mali ya CCM, ni ya Watanzania wote.
“Mawaziri wetu wamekuwa mchwa,
wanaangamiza nchi na leo nitamtaja
waziri anayeongoza kwa kutafuta fedha
za Watanzania. Ni Waziri wetu wa
Fedha, Mustafa Mkulo. Ameuza viwanja,
amelidanganya Bunge baada ya
kuivunja CHC,” alisema mbunge huyo.
Awali Filikunjombe alisema Waziri wa
Viwanda na Biashara, Cyril Chami,
alikuwa amelidanganya Bunge kwa
kudai amefuata maagizo yote ya Kamati
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Alisema kuwa ana ushahidi wa kutosha
jinsi mawaziri hao wanavyoitafuna nchi
na kuhoji Bunge linachukua hatua gani
inapobainika mawaziri wamelidanganya
Bunge.
“Waziri Chami amedai kuwa
ametekeleza agizo la kamati kuhusu
uchunguzi wa Shirika la Viwango
Tanzania (TBS). Uchunguzi ulifanywa
wakati mkurugenzi alikuwa akiendelea
na kazi, wakati kamati ilishauri wakati
wa uchunguzi mkurugenzi huyo awekwe
pembeni,” alisema.
Kutokana na kauli hiyo, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Bunge), William Lukuvi, ambaye pia ni
mnadhimu mkuu wa shughuli za serikali
bungeni, alimtaka kuthibitisha madai
kuwa mawaziri wote ni wezi kwa
kukabidhi ushahidi na kama hana
uhakika na anachozungumza afute kauli
hiyo. Hata hivyo, mbunge huyo
alisisitiza kuwa alichosema ni kwamba
mawaziri wengi ni wezi na si wote.
Mbunge wa Kasulu, Moses Machari,
alisema wabunge wanaotaka mawaziri
na wabadhirifu kunyongwa wanafanya
hivyo wakiwa na akili timamu kwa
sababu wamechoshwa na wizi wa
waziwazi unaofanywa na mawaziri na
baadhi ya viongozi wa serikali bila
kuchukuliwa hatua yoyote.
Kwa upande wake, Mbunge wa
Musoma Mjini, Vicent Nyerere
(CHADEMA), alitaja waziwazi majina ya
vigogo wanaomiliki kampuni za ukaguzi
wa magari ambazo zilitajwa bungeni
kama ni za nje, hali iliyolifanya Bunge
kuzizima kwa muda.
Nyerere alisema kuwa makampuni hayo
yalilipwa mamilioni ya dola za
Kimarekani kwa udanganyifu, na kibaya
zaidi waziri mhusika akalidanganya
Bunge akidai kuwa taarifa hizo zilikuwa
za uongo. Alionyesha kushangazwa
kwake na nguvu kubwa ya kumlinda
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango
Nchini (TBS) wakati ukweli wa mambo
uko wazi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril
Chami, alisema kuwa dhana iliyojengeka
kuwa wizara hiyo inaibena TBS na
mkurugenzi wake, haina ukweli, kwani
taarifa ya kamati ndogo ya uchunguzi
wa shirika hilo aliipata jana na
ameshaiagiza bodi ya shirika hilo
kuifanyia kazi.
Hata hivyo, alisema yuko tayari kuweka
rehani uwaziri wake iwapo mbunge
huyo atathibitisha kuwa kuna kampuni
hewa zinazokagua magari nje ya nchi na
iwapo kampuni hizo zina uswahiba
naye.
“Nimekosea wapi? Kila nilichoagizwa
nimetekeleza. Wizara halindi uozo.
Tukilazimishwa kufanya maamuzi bila
kufuata taratibu tutakuwa tunakiuka
sheria,” alisema.
Ujasiri huo hata hivyo, uliyeyuka kama
nta jioni, baada ya Nyerere kumuumbua
kwa kutaja majina ya wamiliki wa
kampuni hizo, hali iliyompa wakati
mgumu waziri huyo.
 
Tatizo la Lukuvi ni kilaza na amepewa nafasi hii kwa upendeleo baada ya mke wake Gemina Lukuvi kumbembeleza sana JK amsaidie mume wake.
hapa nafikia sehemu na kuamini kuwa hii nchi haitapiga hata hatua kama tutabakia kuendekeza huu ujinga.

Fikiria, rais anakaa na kufikiria ni jinsi gani apange baraza la mawaziri.

- Anaanza kwa ku-balance dini za watu ili wasije kumuona ni mdini
- Anaangalia makabila ili asionekane anaegemea makabila machache
- Anaangalia jinsia
- Anaangalia umri - wazee na vijana
- Anaangalia 'system' inasemaje
- Anakumbukia warithi - Akina Mwinyi, Malima, Kawambwa, Sioi, Makamba nk
- Anaangalia wanamtandao wanasemaje
- Anaangalia fadhila - fulani alimpaga lifi shangazi yangu kipindi kile anaenda ngomani
- .....
- ....
- Mwisho anaangali uwezo wa wateuliwa!

Sasa mfano mzuri ni kama sisi tuklioko huku mbali, hatuhitaji chochote katika uchaguzi kama huo bali tunahitaji huduma za jamii na maendeleo. Kwa hiyo hata kama nchi haina waziri kama yanakuja ni bora zaidi ya kuwa na mawaziri 60 ambao kazi yao kubwa ni kuangalia jinsi ya kuiba na kufilisi nchi ambacho ni kinyume cha viapo.

Sasa Mh. Filikunjombe unadhani ni kipofu na msaliti wa nafisi yake kwa kiasi gani mpaka asiyaone haya!??

Alafu mawaziri wanatamka waziwazi kuwa hawawezi kujiuzuru ...hii jeuri wanaipata wapi kama uteuzi wao hauku-base kwenye hivyo vigezo hapo juu isipokuwa cha mwisho!?

 
Back
Top Bottom