Mawaziri wanaongoza kwa wizi serikalini - Deo Filikunjombe

Hao akina Lukuvi inaelekea ndiyo wale design za yes Sir. No wonder wanasurvive kila awamu!!
 
Nilishamwona muda mrefu huyu Kijana Filikunjombe uwezo wake, uchungu kwa wapiga kura wake na kwa taifa. Hapa JF mmenishambulia kwa sana tu kuhusu mbunge huyu, na leo wenyewe mnaona alivyo mtetezi mkubwa ndani ya bunge bila kujali itikadi za kichama.

Juzi tu nilifanya utalii Mkoa mpya wa Njombe, tofauti ya majimbo ya uchaguzi yanayoongozwa na wabunge wa CCM Njombe Kusini la Spika Anna makinda na la Ludewa la Filikunjombe utaona tofauti kubwa. Kijana kaanza juzi tu barabara zinaakisi kushughulikiwa tofauti na kwa Makinda. Stand ya mabasi Njombe ikinyesha mvua ni matope na kukiwa Jua ni jangwa la vumbi unatakiwa vaa kitambaa na maski vinginevyo mafua yatakuanzia hapo hapo uwanjani.

Tuachane na ushabiki, Kijana Filikunjombe yuko Mtanzania halisi asiye mbinafsi na mwoga na anayejali utaifa na ni mzalendo wa kweli. Hawa ndio tunaowataka na kesho wakiamua kujing'oa CCM na kujiunga na kambi ya akina Tundu Lisu, ndo kasi ya maendeleo ya nchi yetu itakavyopiku mataifa yote ya afrika mashariki.



kuna mahali nimeona post yako kuwa uko USA kwa obama na kuwa ndege iliingia mushikeli...vipi mkuu usharudi
 
jamani hata Mungu alivyotaka kuwakomboa waisraeli kule Misri aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu kwanza ili aweze kuziona nguvu za Mungu. Bila shaka na kwa ccm pia kinachofanyika hapa ni kuwa na moyo mgumu ili waione nguvu ya umma. ili ukubali ukatae ukombozi wa watz u karibu. wabunge wakikosea hii timing ya ss basi tena.
 
Lukuvi ememtaka Mh Filikunjombe athibitishe kauli yake kuwa mawaziri Wengi ndio wanaoongoza kwa kuitafuna nchi hii. Filikunjombe kasema yupo tayari kufanya hivyo, je tutegemee nini toka kwa serikali yetu inayovuliwa nguo hata na wabunge Wa CCM?
Kwa kuwa speaker ubongo ni matape ataharishe Bunge kama kawaida yake, she can't deal with isssues
 
kuna mahali nimeona post yako kuwa uko USA kwa obama na kuwa ndege iliingia mushikeli...vipi mkuu usharudi

Dunia inazidi kuwa ndogo sana, kwani kama jana ulikula dinner Moscow, usishangae kesha unakula breakfast pale Mikocheni Shoppers center. Ukifanya tathmini ya kutosha unaweza kugundua lini mwandishi alitembelea huko kwa akina Makinda na Filikunjombe kabla au baada ya kupata msukosuko wa ndege kusitisha kuruka kwa masaa kadhaa pale Zurich Internationa Ariport kwa ndege ya US Airways.
 
Vijana wamechoka kuburuzwa na wazee kwa manufaa yao, mizee inachota halafu inataka vijana waufyate. BIG UP Filikunzombe!!!!
CCM imeoza, inakuwa kama ni chama cha watu fulani wenye nguvu na sio kwa wanyonge walio wengi. Tunahitaji kufanya mabadiliko hata ya kuingia msituni.
 
Kwani usibitisho wa Lema walisha usoma....kama bado wausome kwanza wa Lema ndiyo waombe mwingine

Kimsingi kwa kukaa kimya wenye akili walijua kuwa waziri mkuu alidanganya bunge. Kwa hiyo PM wetu ni MUONGO. Lakini inaonekana serekali iliingilia kati kumlina PM na ndio maana wakafanya njama ya kumuondoa Lema Bungeni.
 
Huyu Mhe, Filikunjombe alikuwa Polisi kwaiyo anaposema anaoushahidi atakuwa amejipanga lakinio pia jamani wenye ushahidi wakumsaidia kuongeza nguvu Mhe, Filikunjombe wampe ili watanzania wajue Serikali ilivyo na uozo.
 
Jana Deo Filikunjombe na Zitto Kabwe walinong'onezana waombe muongozo wa spika wakawa wanaambiana nianze mm au wewe na kweli wote walisimama kumzungumzia mkulo so Deo sio mjinga aseme mneno mazito yasiyo na ushahidi,pili ikumbukwe Deo ni makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya mashirika ya Umma na anafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na zitto so kwa nafasi hiyo anayo nafasi ya kujua mengi sana juu ya wizi na wezi wenyewe.
 
Imefika hatua sasa mwana kumkana mzazi wake kama hali ndo hii tutegemee makubwa zaidi juu ya kuanikana kwa chama kilicho madarakani maana mawaziri wako bize ni jinsi gani watafaidi keki ya taifa lakini si kufaidisha wananchi " DHULUMA SIKU ZOTE HAIDUMU NA KILA ADHULUMUYE HUADHIBIWA KWA KUDHALILISHWA NA MUNGU ILI KUWAPA FUNDISHO WENGINE"Tutegemee mengi zaidi kutokana na laana ya walioapa mara moja bungeni/mara mbili mbungeni na kisha Ikulu na kisha kuomba Mungu/Allah awasaidie kulinda mali na rasilimali za nchi hii hali nyoyoni hawako hivyo; sasa yaliyoko nyoyoni sasa ndo yanatoka nje na anayetetea hata mwizi siku naye akianikwa atasema ni wabaya wake wa kisiasa?
Je yeye anayewatetea hakuwahi kuingizwa mkenge hata siku moja na makampuni ya utafiti wa madini maana yamezagaa kila sehemu kama naye ni mbuge kama walivyowengine atakuwa amewahi hata kuingizwa mkenge kuwa washirikiane na mwekezaji ili wapate faida ya rasilimali za nchi hii ili awe tajiri au wa ahadi/kutoa huduma kwa wapiga kura wake na sasa ajue siri zinatolewa na makarani/ watu wanaowaamini ndo maana wakihitaji vielelezo unakuta anayezungumza anavyo na mimi naona bora "WALETE SHERIA YA KUBANA UHURU WA HABARI BILA HIVYO WATAJUTA KUINGIA KATIKA UTANDAWAZI"
 
Lukuvi ememtaka Mh Filikunjombe athibitishe kauli yake kuwa mawaziri Wengi ndio wanaoongoza kwa kuitafuna nchi hii. Filikunjombe kasema yupo tayari kufanya hivyo, je tutegemee nini toka kwa serikali yetu inayovuliwa nguo hata na wabunge Wa CCM?



NDUGU WANA JF HAKUNA MTU ANAYEWEZA KUTUWEKEA VIDEO YA MICHANGO YA HAO WABUNGE JANA?>????? WAKATI WA UKOMBOZI NDIO HUU, WEKENI HIYO KITU HATA WABISHI kama........... WAKOMAGE. JUA WENGINE HATUKUIONA MICHANGO MINGINE YA KINA TUNDU LISU. Tafadhali tafadhali KAMA YA KICHAA WA "chukua chako mapema " KULE ARUMERU ILIWEKWA KWA NINI HII CHACHU YA MAPINDUZI IKOSEKANE?????????????????????
 
Back
Top Bottom