Mawaziri wanaongoza kwa wizi serikalini - Deo Filikunjombe

filikunjombe njoo peoples power. Come come.
Huku ndio kunakufaa kusemea huo uozo wa Kletocracy government.
 
Sasa mambo yameiva!

Ni nani atakuwa Waziri Mkuu mpya wa JK?
 
Tatizo yuko na wachafu.... hili ni jembe iko siku litakuja home...
 
Wadau,nipo bungeni. Mbunge Filikunjombe amemwambia Naibu Spika kuwa anawasilisha orodha ya mawaziri wote wezi wa mali ya umma. Tunaisubiri orodha hiyo kuanzia jioni ya leo!! Haki ya Mungu ukombozi tayari!!!!
Ni yaleyaleeeee ya vasco dagama.
 
Hizi biti tumezizoea wasitufanye watoto,
tunataka kitu kinachobeba maji saiv....
Wapige kura ya kutokuwa na imani na serikali nje ya hapo ni porojo na kutuzingua tu.
 
Lukuvi ememtaka Mh Filikunjombe athibitishe kauli yake kuwa mawaziri Wengi ndio wanaoongoza kwa kuitafuna nchi hii. Filikunjombe kasema yupo tayari kufanya hivyo, je tutegemee nini toka kwa serikali yetu inayovuliwa nguo hata na wabunge Wa CCM?

Serikali sikivu ingeyafanyia kazi yaliyotamkwa na mbunge huyu (jembe ndani ya CCM0 anayesimamia ukweli. lakini nina wasiwasi kama serikali ya bwana Kikwete ni sikivu au ina masikio
 
Ni kweli Filipkunjombe asipochemka huko chini kunatisha, Mzee Nyimbo anazidi kubatiza watu kwa jina la CDM, hivyo akaze kamba umma huko kwake umeshaamka
 
Sio mawaziri, rais ndiye anayeongoza kwa kuibaka nchi na safari zake nyiiiingiiii zisizo na maana yoyote. Kaenda Brazil kumsalimia rais mstaafu Lula na kupewa jezi na Maximo, rais anachemka sijaona!

Hizi safari zina tija gani? Kwa nini serikali haitaki kutupa mchanganuo wa gharama zote za safari tangu Dec. 2005 alipoingia Magogoni mpaka sasa na tulichokipata kutokana na hizi safari ili tujue kama ni kweli anakwenda kutalii tu au la?!

Mbona naye hatembelewi kama anavyowatembelea? Sanasana amekuja Waziri Mkuu wa Somalia tena kwa masaa tu na kuondoka zake!
Kama baba anafuja unategemea watoto wafanye nini?
 
Kwa kuwaendekeza mawaziri kama Lukuvi ni janga kwa Taifa hili, anachojua ni kutetea vitu hata ambavyo havina msingi utadhani serikali imeundwa na malaika ambao hawakosea,hawali wala kutoa rushwa, wawajibikaji (Mwinyi,Mponda,Malima,Mkulo & co.????) na kufanya mambo mengine yasiyo na manufaa kwa taifa..

Nadhani anafanya hivi sijui ili kumfurahisha aliyemteua na kusahau hata huyo aliyemteua ana watu waliomchagua pale na kumbe wa muhimu ni wale waliomchagua bosi wake na si vinginevyo..!

Mh.Fili anafanya kazi ambayo tume ya maadili ya viongozi imewashindwa au kwa uoga au kwa kutokuwa na nguvu za kisheria kuwabana hao viongozi walafi na wafujaji wa mali za umma kwa bahati nzuri sheria ya kuunda hiyo tume imepitishwa na wabunge wengi wa CCM kwa kujua au kutokujua....

Kwa kuwa msamiati wa uwajibikaji kwao haupo kabisa..TAKUKURU nayo iko ICU-Kiutendaji inasubiri vijikesi vya laki moja watu wanafungia mpaka safari ..

kwa kifupi bila mfumo bora,imara na unaojitegemea kufanya kazi tutendelea kusikia hizi hadithi za ubadhirifu na hatua kali za kukomesha haya hazichukuliwi..!Nafasi nyingine adhimu watanzania tunapata kiujua kiundani serikali ambayo miaka 7 iliyopita walikuwa na wimbo mzuri wa 'Maisha bora kwa kila mtanzania..' ambao ukiwakumbusha leo ulipoishia waliotunga wanakutolea macho,dharau na kebehi..
 
Naona Godbless Lema reborn katika bunge, siku mahakama ikimrudisha watakuwa wameshaumana vya kutosha!!

Filikunjombe anafahamu kazi yake ni nini..
 
Back
Top Bottom