Mawaziri wanaongoza kwa wizi serikalini - Deo Filikunjombe

KELVIN GASPER

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,066
454
Mbunge huyo ametakiwa athibitishe kauli yake na naibu spika.

Lukuvi amemtaka Mh Filikunjombe athibitishe kauli yake kuwa mawaziri Wengi ndio wanaoongoza kwa kuitafuna nchi hii.

Filikunjombe kasema yupo tayari kufanya hivyo, je tutegemee nini toka kwa serikali yetu inayovuliwa nguo hata na wabunge Wa CCM?
 
Natamani niyajue yaliyoko moyoni mwa wabunge wa CCM kuhusu mustakabali wao na chama chao 2015
 
Watu wamechoka sasa hadi wabunge wenyewe wa ccm wanaona kila siku ujinga unafanyika na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.
 
Filikunjombe kausema ukweli ambao wote hapo mjengoni wanaujua...Mashujaa kama Deo wamechoshwa na serikali yao isiyo na haya kwa walipa kodi wake
 
Hivi kasema atawasilisha au kasema anayo na wakitaka anaweza kuwapa...

Nadhani from experience hawatataka kwahio hatawapa..., hii kitu itasahaulika kama mengine mengi yanavyosahaulika
 
Nimeona mjadala wa jana na hv ndivyo bunge linatakiwa mawazir wote walikuwa kimyaa kama wafiwa kwenye vitu vyao.big up sana kwa wabunge wote haswa vijana wa vyama vyote kwa mwendo huu inawekana
 
Vita ya panzi hiyo..ngoja tusubiri jioni.
Lisu kaua balaa, situation ni mbaya sana kwa serikali ya baba mwanaasha.
 
Dah! Hicho kichwa cha habari! kitauza magazeti ya udaku

Muhimu ni kama anayo hiyo orodha na akaiwasilisha panapohusika litakuwa jambo la kheri hata kama magazeti yatauza.

Mimi ningetegemea awataje moja kwa moja ili kuepuka kuchakachua taarifa yake, ofisi ya spika haiaminiki sana kwa masuala serious and sensitive.
 
Lema aliambiwa apeleke ushahidi wa waziri mkuu kulidanganya bunge. Na aliiwasilisha, je iliishia wapi? CCM wajinga hadi wakubali hiyo orodha ianikwe. Filikunjombe angeonekana mzalendo wa kweli kama angeanza moja kwa moja kutaja majina pamoja na mali walizoiba wakati akichangia hoja, na si kusubiri akaiandae halafu ailete.
 
nani aliyempa mkulo ruhusa ya kuuza viwanja mali ya umma?si wizi huo?
Ni kweli mkuu.

Mambo yote tata yanayohusisha rushwa kubwa kubwa yamekuuwa endorsed na mawaziri. Chukua mfano wa Richmond, TICTS, issue ya Waziri Nundu juu ya bandari, ATCL, TRC. Hizo are just a drop in a ocean ya mifano iliyo wazi na mnaweza kuongezea mnavyojua pia.

Kwa maana hiyo haiwezi kumpa shida sana Mh. Deo Fikulinjomba kulitolea ushahidi. lakini wangelikuwa serious katika ushahidi basi wangelikuwa wameshathibitisha endapo Mh. Lema Godbless ushahidi wake aliouwakilisha ulikuwa sahihi au la

 
Lukuvi alitaka kuchafua hali ya hewa alimnukuu vibaya filikunjombe na Fnjombe akamuumbua kwamba sijasema mawaziri wote bali mawaziri wengi ni wezi na ushaidi ninao
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom