Mawaziri Wakuu wote bomu, isipokuwa Kawawa na Sokoine!!

Ok, I am speechless
Waberoya,
Si hilo tu. Mwaka 1973 Kawawa alimfukuza marehemu David Martin wakati huo alikuwa mwandishi habari wa The Guardian la London. Wakati huo Mwalimu alikuwa ziara ya kikazi Czechoslovakia. Sikumbuki makala aliyoandika David Martin. Mwalimu alipata hizo habari kupitia BBC na nasikia ali' hit the roof' kwa hasira kwa sababu David Martin alikuwa rafiki yake. Alipewa 24 hrs kuondoka nchini so by the time Mwalimu anarudi Martin alishaenda zake Uingereza. Mwalimu alijaribu kumshawishi arudi Tanzania lakini baada ya uhuru wa Zimbabwe alihamia huko ambako alifia.
 
“Kiongozi yeyote anayefunga maduka ya watu binafsi kwa nguvu na kusababisha usumbufu kwa watu wasipate mahitaji; ni adui wa Ujamaa. Maduka binafsi yatakufa kifo cha kawadia vitakapotokea vyama vya ushirika makini na vyenye nguvu, vitakavyosimamiwa vizuri”.

Jasusi,Waberoya,..

..sasa kama msimamo wa Mwalimu ulikuwa kwamba maduka binafsi yawe replaced na maduka ya vyama vya ushirika kitu gani kilimsukuma kuvivunja vyama vya ushirika?

..mimi naona Mzee Rashidi Kawawa alifunga maduka ya watu binafsi kwa kufuata utaratibu uleule uliotumika kutaifisha majumba, mabenki,viwanda,na mashamba makubwa.
 
Mbarikiwa,

..kwa mtizamo wangu kauli ya CD Msuya ama haikueleweka au ilikuwa blown out of context.

..kauli hiyo iliitoa bungeni baada ya kutokea mjadala mkali kuhusu wananchi kuchangia huduma mbalimbali za jamii kutokana na serikali kuwa ktk hali mbaya ya kifedha.

..nakumbuka wabunge walikuwa wanapinga ada ya shule za sekondari. argument ya CD Msuya ilikuwa ni kwamba wananchi wangeweza kuchangia kiwango hicho kidogo, ambacho wakati huo Msuya alidai ni sawasawa bei ya mkungu mmoja wa ndizi.

..sasa badala ya kuupa umuhimu mjadala unaohusu kuchangia huduma za kijamii kwa fedha toka mfukoni vs kutokuchangia, magazeti yakaikuza na kujielekeza ktk kauli moja tu "kila mtu abebe mzigo wake."

..CD Msuya aliwahi kuhojiwa kuhusu kauli hiyo aliyoitoa ktk kikao cha bunge. katika kuelezea alichomaanisha, Mzee Msuya alitoa mfano wa role ya serikali na wananchi pale yanapotokea magonjwa ya milipuko. Msuya alifafanua kwamba wajibu wa serikali ni kuhakikisha kwamba madawa ya kutibu magonjwa yanapatikana, lakini wajibu kujikinga na maradhi ni wa kila mwananchi mmoja mmoja--"kila mtu akibeba msalaba wake."
 


Jasusi,Waberoya,..

..sasa kama msimamo wa Mwalimu ulikuwa kwamba maduka binafsi yawe replaced na maduka ya vyama vya ushirika kitu gani kilimsukuma kuvivunja vyama vya ushirika?

..mimi naona Mzee Rashidi Kawawa alifunga maduka ya watu binafsi kwa kufuata utaratibu uleule uliotumika kutaifisha majumba, mabenki,viwanda,na mashamba makubwa.
jokaKuu,
Hili la kuvunja vyama vya ushirika alikiri kwamba yalikuwa makosa.
 
Back
Top Bottom