Mawaziri Wakuu wote bomu, isipokuwa Kawawa na Sokoine!!

Malecela peke yake ndie aliyekuwa makini

Yap Ive said it sasa wasiopenda kanyweni sumu

Huyo CHIGWIYEMISI aliyewaambia watu watunze pumba halafu zitawafaa wakati wa njaa ndo kabisaaa, ndo maana hata urais wenzio wameona hafai.
 
Huyu Pinda nadhani yeye anafuata upepo tu, kama BIG G anavutika pande zote. Anataka kumridhisha boss wake na WADANGANYIKA vile vile kwa wakati mmoja. Anaonekana ni muoga muoga, dhaifu flani hivi, ingawa EL ni fisadi wa kutupwa lkn jamaa lilikuwa sometimes linakemea kibabe, huyu Pinda dah ni propaganda kwa kwenda mbele. sijui kama tutafika kweli
 
Kawawa naye bomu tu..kawawa si ndo alifilisi mabenki kwa ajili ya miradi ya CCM
 
Huyu Pinda nadhani yeye anafuata upepo tu, kama BIG G anavutika pande zote. Anataka kumridhisha boss wake na WADANGANYIKA vile vile kwa wakati mmoja. Anaonekana ni muoga muoga, dhaifu flani hivi, ingawa EL ni fisadi wa kutupwa lkn jamaa lilikuwa sometimes linakemea kibabe, huyu Pinda dah ni propaganda kwa kwenda mbele. sijui kama tutafika kweli
Nakuunga mkono ni bora ya EL kuliko huyu wa sasa.
 
Hii thread haimek sense if u would ask me. Umahiri wa uwaziri mkuu unaezaje kupimwa objectively?? Je tuna eza u-quantify? System ya utawala inaendana na misifa tunayoimwaga??etc etc

Tuanzie hapo.
 
..makala ya Mihangwa wa raia mwema akiwachambua Mawaziri Wakuu wa Tanzania kuanzia wakati wa Uhuru.
Mkuu, umesikia wapi biography ya mtu aliye hai! Kawawa na Sokoine wanasemwa sasa kwa sababu wameshatangulia na hawaji tena saa hivi. Hata Mtikila akiondoka utaona sifa atakazomwagiwa, achilia mbali Mr zero.
 
C.D. Msuya was among the best PM!!! no longo longo... actions only...
Aa wapi actions zenyewe ni kuelekeza miradi ya maendeleo kwenye jimbo lake hata wakajenga barabara za lami hadi upareni milimani? He was so selfish , what he cared for was the development of his constituency
 
moringe alikuwa bonge la pm yaani alikuwa sirias sana alikuwa mzee wa kaz
sio pinda analialia tu. hiimhhmhi inauma sana hawa maalbino hiiiihmhhhm!
waziri mkuu unalia tena bungeni!
nakumbuka sokoine alianzisha sungu sungu, wachawi na wezi walikiona cha mtema kuni
 
moringe alikuwa bonge la pm yaani alikuwa sirias sana alikuwa mzee wa kaz
sio pinda analialia tu. hiimhhmhi inauma sana hawa maalbino hiiiihmhhhm!
waziri mkuu unalia tena bungeni!
nakumbuka sokoine alianzisha sungu sungu, wachawi na wezi walikiona cha mtema kuni

Mkuu, aliyeanzisha sungusungu national ni Augustine Lyatonga Mrema. Sokoine alianzisha Operation Linda Jiji iliyosimamiwa na JKT waakti huo OP Ulinzi. Nilikuwa mmoja wao siku hizo katika ulinzi. Makao makuu ya operation yalikuwa JKT Mgulani na sisi kambi yetu ilikuwa Kunduchi Mtongani pale wanapokaa mapolisi sasa hivi, tuliyabikiri sisi majengo yale. Weacha tu.
 
..hapa chini ni muendelezo wa makala ya Joseph Mihangwa.




KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya tuliona utendaji kazi wa mawaziri wakuu wa Tanganyika na baadaye Tanzania huru; kuanzia Mwalimu Julius K. Nyerere hadi Edward Lowassa; na jinsi Waziri Mkuu wa sasa, Mheshimiwa Mizengo Pinda anavyopiga jaramba kujaribu kuwapiku wote waliomtangulia.
Mawaziri wakuu wawili, Rashid Kawawa na Edward Sokoine ndiyo waliotia fora kwa utendaji; kiasi kwamba rekodi za utendaji wao hazijavunjwa na mwingine yeyote.
Nimeelezea pia ushupavu wa Kawawa enzi za uhuru, na jinsi alivyothubutu kutenda pale Nyerere aliposhindwa kutenda kwa hofu, na akafanikiwa. Ni yapi mengine yanayowafanya Kawawa na Sokoine (ambao sasa hawapo nasi), wang'are kuliko mawaziri wakuu wengine walioshika wadhifa huo mkubwa na nyeti?
Rashid Mfaume kawawa, ambaye kabla ya uhuru alikuwa kiongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TFL), alijenga uaminifu mkubwa kwa Nyerere, naye akajenga imani kubwa zaidi kwake kiasi cha kuendelea kumvisha nyadhifa na majukumu makubwa makubwa nchini.
Kawawa hakuwa kipenzi kikubwa cha watu ukimlinganisha na Waziri kama Oscar Kambona ambaye aliuvuta umma wa Kitanzania, hasa vijana na kina mama ambao waliiga kwa hamasa kubwa mtindo wake wa kuchana nywele, maarufu kama Kambona Style. Lakini pamoja na hayo, Nyerere hakuweza kumteua kuwa Waziri Mkuu, ila Rashid kawawa. Kwa nini?
Mwalimu analo jibu, anasema: "Oscar (Kambona) ni mtu mwenye haya. Pili, si mtu ambaye hoja zake zinashabihiana sana. Kwa hiyo, hata kama ukipata nafasi ya kuzungumza naye, hajui kujieleza vizuri sana; inawezekana hata katika vidokezo".
Akiwalinganisha Rashid kawawa na Oscar Kambona, Mwalimu anasema: "Oscar ni mtu wa watu. Na Rashid vile vile; lakini Rashid hashangazi mtu; Rashid hana upendeleo na mtu; si mtu anayeweza kugandana na mtu mwingine; Oscar ana uchungu mwingi sana. Na kama alivyo mtu yeyote mwenye uchungu, hujiundia vikundi anavyogandamana navyo mno".
Akaongeza kusema: "Rashid ni mtawala, mtekelezaji; hana uchungu mwingi; ukimpenda vema; na kama hutampenda, hilo halimzuii kufanya kazi yake. Na kwa vyovyote vile hatatokwa machozi hata kidogo" (soma: Mwalimu Julius Kambarage Nyerere" cha William Edgett Smith, uk. 211).
Kwa hiyo, alipomwachia Kawawa uongozi wa nchi kama tulivyoona, Nyerere alikuwa akifanya hivyo kwa mwanasiasa mshirika wake wa karibu kuliko mawaziri wengine. Na pale Nyerere aliporejea; safari hii kama Rais Mtendaji, wachunguzi wa mambo walianza kubashiri kwamba, Kawawa ndiye angekuwa mrithi mtarajiwa wa Nyerere wa kiti cha Rais.
Kawawa alikuwa bado Waziri Mkuu wakati Tanganyika na Zanzibar zikiungana mwaka 1964 kuunda Tanzania. Juu ya cheo hicho, alifanywa pia Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Muungano, na Mzee Abeid Amani Karume kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais.
Mwaka 1977 Kawawa aliondolewa uwaziri mkuu; tukio ambalo wengi waliliona kama matokeo ya ‘laana' kwake kutokana na jinsi alivyoendesha kwa matumizi ya nguvu, zoezi la kuhamisha watu kujiunga na Vijiji vya Ujamaa, na lile la "Operesheni Maduka", kwa kufunga maduka ya watu binafsi ili kutoa nafasi kwa maduka ya ushirika. Matukio hayo mawili yalimpunguzia kwa kiwango kikubwa sifa na umaarufu kwa wananchi wengi.
Kwa kushtushwa na kasi ya Kawawa ya "Operesheni Maduka", Nyerere alilaani akisema: "Kiongozi yeyote anayefunga maduka ya watu binafsi kwa nguvu na kusababisha usumbufu kwa watu wasipate mahitaji; ni adui wa Ujamaa. Maduka binafsi yatakufa kifo cha kawadia vitakapotokea vyama vya ushirika makini na vyenye nguvu, vitakavyosimamiwa vizuri".
Lakini ni Rashid Kawawa huyo huyo aliyesimamia mchakato wote wa kufutwa kwa vyama vya ushirika mwaka 1976, na nafasi yake kuchukuliwa na mamlaka za mazao hadi viliporejeshwa tena mwaka 1984.
Ni kutokana na matukio kama hayo na mengine wachunguzi wa mambo ya siasa nchini waliona kwamba kuanguka kwa Kawawa kulikuwa hakukwepeki.
Chaguo la Nyerere la mrithi wa Kawawa lilishutua wengi. Edward Moringe Sokoine, ambaye kabla ya kuteuliwa, alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, hakuwa mmoja wa wanafunzi au wafuasi wa Mwalimu; wala hakuwa na jina kwenye duru za siasa kabla ya uhuru. Uteuzi wa Sokoine kwa nafasi ya Waziri Mkuu nusura uvunje Muungano wa Tanzania. Kwa nini?
Rais Aboud Jumbe Mwinyi, Rais wa Awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais, aliyechukua wadhifa huo kufuatia kifo cha Mzee Abeid Amani Karume, mwaka 1972; tofauti na Karume, alipania kuimarisha kwa vitendo Muungano kwa kuwa karibu kiutendaji na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Nyerere.
Tena tofauti na Karume, Jumbe aliweza kumwakilisha Nyerere nje ya nchi mara nyingi; alitembea nchi nzima akitoa hotuba ndefu kutetea Muungano na hatimaye kuridhia kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU kuunda CCM, jambo ambalo lisingewezekana enzi za Karume.
Kwa sababu hii, Jumbe alianza kujihesabu kama mrithi halali wa Nyerere asiyeepukika kwa kiti cha Rais wa Tanzania. Jumbe akatumia muda mwingi kwa shughuli za Muungano na kumwakilisha Rais nje; akaitelekeza Zanzibar kwa matarajio ya kuukwaa urais wa Jamhuri ya Muungano.
Nao utendaji kazi wa Sokoine ulianza kujionyesha muda mfupi tu baada ya kuteuliwa. Alijipambanua kama mtekelezaji na mfuatiliaji mzuri wa maamuzi ya Serikali, mkweli na mwenye kujali watu; hasa Wanyonge. Hakupenda kuonea wala kuonewa.
Kwa sababu hii, alipendwa na wengi, hasa watu wa tabaka la chini; kiasi kwamba katika kipindi kifupi Taifa liliimba na kushangilia jina na sifa zake. Nyerere akafurahi na kumweka moyoni.
Habari zikavuja kwamba tayari Mwalimu Nyerere alikuwa amemweka Sokoine moyoni na katika kitabu chake kuwa mrithi wake mtarajiwa baada ya kung'atuka. Naye Jumbe akanusa upepo; uhasama ukaanza kati ya viongozi hao wawili.
Hatua ya kwanza ya Jumbe ilikuwa ni kuhoji mfumo wa uhalali wa Muungano na Sheria iliyouanzisha. Nayo Redio Zanzibar ikadaka haraka wimbo wa Jumbe, kwa kutangaza maneno ya kashfa dhidi ya Muungano kupitia kipindi kilichojulikana kama "Kiroboto Tapes", au Kanda za Kiroboto.
Na katika Sherehe za Mapinduzi mjini Unguja, Januari 12, 1984 ambazo Mwalimu alihudhuria, Jumbe aliendeleza uchokozi wake wa kuhoji Muungano na kuwataka Wazanzibari watulie wakati akishughulikia suala hilo. Akasema ikibidi angelifikisha kwenye Mahakama Maalum ya Kikatiba ili kupata ufumbuzi.
Hatua nyingine aliyochukua ni ya kumrejesha kwao Bara, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mheshimiwa Damian Lubuva; na badala yake akamteua Al-Haji Bashir Kwaw Swanzy, raia wa Ghana, na rafiki wa Jumbe tangu 1958.
Kisha Jumbe alimwagiza Swanzy kuandaa Hati kupeleka Mahakama ya Kikatiba kuhoji mfumo na uhalali wa Muungano.
Na baada ya hati hiyo kuwa tayari na kuwekwa mezani kwa Jumbe ili aitie sahihi, ilipotea katika mazingira ya kutatanisha, na kuibukia mikononi mwa Mwalimu Nyerere. Duru zinadai kuwa ni Seif Sharif Hamad aliyepora hati hiyo na kuipeleka kwa Mwalimu.
Mwalimu akachemka, akaitisha kikao cha dharura cha NEC mjini Dodoma ambako Jumbe aliitwa kujibu tuhuma za kutaka kuvunja Muungano. Na baada ya kukiri kuandaa hati hiyo, alivuliwa nyadhifa zote za Chama na Serikali na ikatangazwa "Hali ya kuchafuka kwa hali ya hewa ya Kisiasa Visiwani".
Sokoine hakurithi nafasi ya Makamu wa Rais kama alivyokuwa Rashid Kawawa, kwa sababu ilifutwa baada ya kuunganishwa kwa TANU na ASP, kuunda CCM, Februari 5, 1977.
Kule kuunganishwa tu kwa TANU na ASP kuwa Chama kimoja cha CCM, na Nyerere akiwa Mwenyekiti wake, kulimaanisha kuongezeka kwa majukumu ya Rais huyo. Kwa sababu hiyo, Sokoine alibebeshwa majukumu mengi na makubwa zaidi kuliko mawaziri wakuu waliomtangulia.
Kati ya yaliyohitaji ufuatiliaji wa haraka, ni pamoja na programu ya "Vijiji vya Ujamaa" iliyokuwa ikipita katika hatua ngumu ya utekelezaji. Kulikuwa pia na ufuatiliaji wa Mapendekezo ya Kamati ya Rais ya kudhibiti matumizi Serikalini (KRUM) yaliyokuwa yakisubiri utekelezaji.
Nchi ilikuwa ikipita pia katika hatua ngumu ya marekebisho ya kiuchumi na kijamii kufuatia kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na wakati huo ikilamba vidonda kwa kuhimili machungu ya kufutwa kwa vyama vya ushirika nchini kwa fagio la Rashid Kawawa.
Kana kwamba hayo hayakutosha, Sokoine alirithi mpango wa madaraka mikoani wenye kuyumba, huku tishio la kuzuka kwa vita kati ya Tanzania na dikteta Idi Amin wa Uganda likionekana dhahiri; wakati uchumi wa nchi haukuwa pia wa kutia matumaini. Sokoine hakuyaogopa hayo; alibeba furushi la matatizo yote na kulitia kichwani.
Sokoine alisafiri nchini nzima kusikiliza matatizo ya wananchi zaidi kuliko kutoa hotuba enzi hizo ambapo ufundi wa kuongea jukwaani ilikuwa kielelezo cha mwanasiasa bora na mahiri.
Mwaka 1980 Watanzania wakashtushwa na taarifa kwamba Sokoine alikuwa amejiuzulu kwa matatizo ya kiafya, na nafasi yake kuchukuliwa na Cleopa David Msuya.
Hata hivyo, Msuya, kama nilivyoeleza mwanzo, hakuweza kuvaa kiatu cha Sokoine kikamkaa; akaonekana kama ndege wa kupita tu.
Sokoine alirejea miaka mitatu baadaye kushika tena nafasi hiyo ambayo matuta yake tayari alikuwa ameyaelewa vizuri, lakini furushi la matatizo lilikuwa limeongezeka uzito na kimo kuliko wakati akiondoka mwaka 1980.
Moja ya matatizo aliyobaini ni ukosefu bandia wa bidhaa muhimu nchini uliosababishwa au kubuniwa na walanguzi wa bidhaa; hivyo akaamua kupambana nao ana kwa ana.
Na kadri mapambano dhidi ya walanguzi yalivyozidi kupamba moto, ndivyo mtego wa Sokoine ulivyoweza kunasa raia wema wasiokuwamo - wachuuzi wadogo wadogo, kama vile wauza viberiti na lita chache za petroli kando kando mwa barabara; huku walanguzi halisi wakikwepa mkono wa Serikali.
Hali hiyo inaweza kufananishwa na tatizo la rushwa na ufisadi nchini leo ambapo mkono wa Serikali (TAKUKURU) unakamata dagaa na kuwaacha nyangumi na mapapa yakiogelea salama katikati ya bahari yakibeba na kutafuna yanachopora.
Kwa sababu hii, Sokoine aliishia "kuwachokoza" wenye nguvu (mapapa) bila kuwasaidia walala hoi aliokusudia kuwakomboa, hadi mauti yalipomkuta kwa ajali ya gari, Aprili 12, 1984. Lakini pamoja na hayo alikufa kama "mtu wa watu" na mtetezi wa wanyonge.
Hawa wawili - Kawawa na Sokoine, kama nilivyosema mwanzo, hawajafikiwa kwa sifa na waziri mkuu mwingine yeyote tangu uhuru.
Hawa wawili hawakuwa mawaziri wakuu wenye haya ambayo ni ishara ya kukosa msimamo, maamuzi na kuacha mambo yaende shaghalabaghala, na Serikali kuyumba.
Kawawa na Sokoine walikuwa watendaji wenye hoja thabiti na msimamo usioyumba. Ndiyo maana waliweza kutoa maamuzi magumu katika masuala yaliyogusa watu na maslahi ya Taifa.
Hawa wawili, hawakuwa wenye uchungu mwingi kwa nafsi zao binafsi (over sentive to self personality), bali wenye uchungu kwa maslahi ya walio wengi. Hawakutamani kupendwa; bali kupendwa kwao kulikuja kwenyewe kutokana na kazi yao, na kwa wao kuwapenda watu.
Angalia mawaziri wakuu wa enzi zetu za sasa: wakiguswa tu kwa shutuma au kutakiwa kujirudi na pengine kubadilishwa kazi, wataruka juu kama wamemwagiwa upupu na kuunda vikundi na mtandao wa kuwasafisha; na pengine kuanzisha vita ya kubakia au kurejea madarakani kwa njia yoyote ile!
Lini tutapata viongozi wa aina ya Kawawa na Sokoine; wachapa kazi wasiotafuta sifa na utukufu ila kujinyenyekeza kwa wananchi kwa kutumikia badala ya kutumikiwa?
Wako wapi viongozi ambao, kama alivyosema Mwalimu, "ukiwapenda, vema; na kama hutawapenda, hilo haliwazuii kufanya kazi zao, na kwa vyovyote vile hawatatokwa machozi"? Hawapo, labda tunamwona kwa mbali Dakta John Pombe Magufuli akija, na pengine huyu Mizengo Kayanza Pinda, akipiga jaramba!



 
..kuna masuala ya kihistoria ktk hizi makala na wachangiaji naona kama mnashindwa ku-take note of them.

..kuna suala la Mwalimu Nyerere kujiuzulu uwaziri mkuu. wakati miaka yote tunaambiwa alifanya hivyo ili kwenda kuimarisha chama, mwandishi anadai Mwalimu alijiuzulu baada ya kushindwa mjadala mkali uliohusu sera ya Africanization.
 
Mi Sokoine peke yake ndio namfagilia.Pinda kidogo,Lowasa hata kidogo sipo kwenye boti yake kabisa,hao wengine siwafahamu vizuri.
 
Chimunguru said:
Ah wapi msuya alijenga kwao upareni akapeleka umeme, barabara mpaka milimani, mbona hakujenga barabara ya dodoma-tabora-singida-kigoma, ile ya tunduma-sumbawanga mbona hakujenga?

Chimunguru,

..kumbe Cleopa Msuya alishayatolea majibu haya madai yako kwamba alihujumu maendeleo ya maeneo mengine ya Tanzania na kupeleka jimboni kwake Mwanga.

..soma kipande cha mahojiano yake na Absalom Kibanda.


MWANANCHI JUMAPILI: Kumekuwa na madai kwamba ukiwa kiongozi, uliamua kutumia ramani ya Mpango wa Maendeleo wa Makao Makuu Dodoma (CDA) kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya ya Mwanga. Madai haya yana ukweli wowote?

MSUYA: Huo ni uongo kabisa kabisa, Huwezi kuchukua mpango wa Dodoma ambao maumbile yake ni tofauti nikaupeleka Mwanga ambako ni tofauti. Kuna watu walikuwa wanaeneza hayo mambo lakini ni uongo. Kitu ambacho nakiri kimefanyika ni kwamba, Wilaya ya Mwanga ilianzishwa na Serikali Julai 1979 kwa hiyo wizara ya Ardhi ya Mipango Miji iliombwa iende Mwanga kutengeza plan (mpango), wakaja wakatoa mapendekezo ya jinsi ya kuanza, mapendekezo yale yalikuwa mafinyu sana, tukashauri kwamba viongozi wa Wilaya ya Mwanga na viongozi wa Wizara ya Ardhi na Mipango Miji waende CDA kuona kwamba kweli itafaa na walipofika watalaam kule wakaona kuna marekebisho mengi ya kuyafanya na wakayafanya. Kwa hiyo kutumia utaalam na ushauri wao ndiyo, lakini, kusema tulichukua mipango miji ya Dodoma kupeleka Mwanga ni uongo.

MWANANCHI JUMAPILI: Kuna madai mengine kwamba ukiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais ulitumia muda wako mwingi kuangalia maendeleo ya jimbo lako la uchaguzi na wilaya yako ya Mwanga zaidi kuliko hata ilivyokuwa kwa maeneo mengine ya nchi, jambo ambalo baadhi ya watu wanaliona kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka

MSUYA: Hilo nalo pia napenda niseme ni uongo. Yamezushwa mambo mengi, unajua kwenye hizi nafasi za uongozi kila mtu anaona ni jalala lake la anatupa uchafu. Nakumbuka kuna watu walikwenda wakaeleza kwamba, huyu mzee pamoja na mambo yote, ametia barabara zote za lami katika Wilaya ya Mwanga sasa safari moja niko nyumbani kule kwenye hizi sherehe za mbio za Mwenge, hawa vijana wa Mwenge wakashangaa mabarabara yetu mabovu kule milimani, wakauliza yale mabarabara ambayo tunaambiwa Msuya kajenga yako wapi, wakaambiwa hayo ni maneno tu yanazongumzwa huko Dar es Salaam.

Kitu ambacho nakubali nimefanya, na si aibu nashauri hata wenzangu wabunge. Nilikuwa mbunge wa kuchaguliwa pale tangu mwaka 1980 mpaka 2000 nilipostaafu. Katika mwanzo wake, miaka ya 1980 kama mnavyofahamu hali ya uchumi ilikuwa mbaya sana, kwa hiyo kama mbunge kazi yangu ya kwanza ilikuwa ni kwenda kueleza wananchi kwamba wasije wakatazamia kwa sababu wamenichagua mimi kama mbunge wasifikiri kwamba watapata vinono kutoka serikalini, kwa sababu hamna lakini kama wakitaka maendeleo ni lazima tuungane nao watu wajikusanye nguvu, wachange, na wanaoweza kufanya kazi kwa mikono wafanye.

Kwa kweli nilifanya kazi ya ku-mobilise opinion na wananchi kujishughulisha na kazi ndogondogo za maendeleo za kujenga zahanati, shule maji, barabara na kitu kimoja ambacho nilijivunia na nikashawishi wakakubali si sehemu moja katika kila pembe ya Wilaya tuwe tunashawishi chini ya kamati zao wawe na kitu cha kufanya na kazi za mbunge unakuwa unapita na unaona wanavyofanya na wakiwa wana matatizo unawasaidia, ukipata msaada unawapelekea, hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa uzoefu wenu kama vyombo vya habari ukichunguza wabunge waliopo pale bungeni wale wabunge ambao wako karibu sana na wapigakura wao na wanajishughulisha na hizi kazi ambazo wananchi wanafanya kuna vuguvugu la maendeleo. Ukikuta wale wabunge ambao wanakwenda siku moja, wakishachaguliwa hawarudi tena wanakaa mjini huku na kuuliza serikali itafanya nini hapa, utaona hakuna kitu kinachofanyika.

Mimi niliungana na wale wenzangu ambao walikuwa wanamotisha wilaya zao, wako wengi utaona kama kule wilaya ya Njombe, Mufindi, Lushoto mahali kama Ruvuma sehemu kama Songea, mobilization imekuwa ni kubwa sana na watu wamefanya mambo mengi, mobilisation kama ya kilimo na kadhalika.

Wale ambao wanajua historia, zamani Ruvuma haikuwa kitu lakini katika mobilisation ile Gama na nani wamemobilise watu sasa iko katika Big Four, wanazalisha mahindi, wanazalisha tumbaku, watu wamejenga nyumba nzuri. Kwa hiyo mobilisation inafanya kazi, wenzetu wa Rukwa wanafanya hivyo hivyo. Kwa hiyo hicho ndicho nilichofanya, kwa hiyo hii shutuma inayokuja kuwa ooho ametumia nguvu zake..., mimi tena kila wakati nilikuwa nikiomba hao wenye shutuma hizo waende wakakague ni vitu gani hivyo?
 
''Mwaka 1977 Kawawa aliondolewa uwaziri mkuu; tukio ambalo wengi waliliona kama matokeo ya ‘laana' kwake kutokana na jinsi alivyoendesha kwa matumizi ya nguvu, zoezi la kuhamisha watu kujiunga na Vijiji vya Ujamaa, na lile la "Operesheni Maduka", kwa kufunga maduka ya watu binafsi ili kutoa nafasi kwa maduka ya ushirika. Matukio hayo mawili yalimpunguzia kwa kiwango kikubwa sifa na umaarufu kwa wananchi wengi.
Kwa kushtushwa na kasi ya Kawawa ya "Operesheni Maduka", Nyerere alilaani akisema: "Kiongozi yeyote anayefunga maduka ya watu binafsi kwa nguvu na kusababisha usumbufu kwa watu wasipate mahitaji; ni adui wa Ujamaa. Maduka binafsi yatakufa kifo cha kawadia vitakapotokea vyama vya ushirika makini na vyenye nguvu, vitakavyosimamiwa vizuri".


Hebu nisaidieni bandugu, mbona hapo naona JKN alikosea? kwa nini wasingemalizana na mheshimiwa ofisini mpaka aseme hayo maneno kwa wananchi?
 
''Mwaka 1977 Kawawa aliondolewa uwaziri mkuu; tukio ambalo wengi waliliona kama matokeo ya ‘laana’ kwake kutokana na jinsi alivyoendesha kwa matumizi ya nguvu, zoezi la kuhamisha watu kujiunga na Vijiji vya Ujamaa, na lile la “Operesheni Maduka”, kwa kufunga maduka ya watu binafsi ili kutoa nafasi kwa maduka ya ushirika. Matukio hayo mawili yalimpunguzia kwa kiwango kikubwa sifa na umaarufu kwa wananchi wengi.
Kwa kushtushwa na kasi ya Kawawa ya “Operesheni Maduka”, Nyerere alilaani akisema: “Kiongozi yeyote anayefunga maduka ya watu binafsi kwa nguvu na kusababisha usumbufu kwa watu wasipate mahitaji; ni adui wa Ujamaa. Maduka binafsi yatakufa kifo cha kawadia vitakapotokea vyama vya ushirika makini na vyenye nguvu, vitakavyosimamiwa vizuri”.


Hebu nisaidieni bandugu, mbona hapo naona JKN alikosea? kwa nini wasingemalizana na mheshimiwa ofisini mpaka aseme hayo maneno kwa wananchi?
Waberoya,
JKN ilibidi aseme hayo hadharani kwa sababu he was politically responsible. hasira za wananchi zingeelekezwa kwake badala ya Kawawa.
 
Back
Top Bottom