Mawaziri Wakuu wa Zamani walonga!

MawazoMatatu

JF-Expert Member
Sep 6, 2008
505
61
Gazeti la Mwananchi la leo limepambwa na habari za mawaziri wakuu wastaafu wawili wa jamuhuri yetu ambao kwa nyakati tofauti wamezungumzia matatizo yanayoikumba Taifa letu.
Mawaziri wakuu hao wastaafu ni Jaji Joseph Warioba na Dr. Salim A Salim.
Ingawa vichwa vya habari ni tofauti lakini ukizisoma habari hizo utakuta wanazungumzia kitu kimoja nacho ni ombwe la kiuongozi ambalo hata sisi humu tumekua tukilijadili sana.

Pengine inaweza ikawa ni utaratibu wa kawaida kwa awamu hii ya uongozi (ya Nne) kwa viongozi wastaafu kuikosoa serikali tofauti na awamu zingine huko nyuma lakini hili la Dr Salim kuuvunja ukimya wake wa muda mrefu kidogo imenifanya nifikilie mambo mengi!

Je wachunguzi wa mambo ya Kisiasa hili lina tafsili gani? Je linaweza kuwa na uhusiano wowote na uchaguzi mkuu wa 2010? Tujadili..!
 
Last edited:
Gazeti la Mwananchi la leo limepambwa na habari za mawaziri wakuu wastaafu wawili wa jamuhuri yetu ambao kwa nyakati tofauti wamezungumzia matatizo yanayoikumba Taifa letu.
Mawaziri wakuu hao wastaafu ni Jaji Joseph Warioba na Dr. Salim A Salim.
Ingawa vichwa vya habari ni tofauti lakini ukizisoma habari hizo utakuta wanazungumzia kitu kimoja nacho ni ombwe la kiuongozi ambalo hata sisi humu tumekua tukilijadili sana.

Pengine inaweza ikawa ni utaratibu wa kawaida kwa awamu hii ya uongozi (ya Nne) kwa viongozi wastaafu kuikosoa serikali tofauti na awamu zingine huko nyuma lakini hili la Dr Salim kuuvunja ukimya wake wa muda mrefu kidogo imenifanya nifikilie mambo mengi!

Je wachunguzi wa mambo ya Kisiasa hili lina tafsili gani? Je linaweza kuwa na uhusiano wowote na uchaguzi mkuu wa 2010? Tujadili..!

Hata raia mwema nalo limepambwa na habari za Mheshimiwa Jaji Warioba kuikosoa serekali ya Muungwana.Jaji Warioba pamoja na mambo mengine pia ameunga mkono waraka wa kanisa katoliki.
 
Mkuu kinachonitatiza hapa ni its just a coincidence wameongea wote kwa pamoja au kuna mpango wa chinichini unaendelea kuhusu hawa wakuu na muungwana!
 
lakini mie alichokiongea Warioba hata sijakielewa labda nyie mnieleweshe alikuwa anamaanisha nini:confused:
 
lakini mie alichokiongea Warioba hata sijakielewa labda nyie mnieleweshe alikuwa anamaanisha nini:confused:

Amesema anashangaa serikali inapambana na rushwa badala ya kurekebisha mfumo (system) inayozaa rushwa, Ikumbukwe alikua kiongozi wa tume inayochunguza mianya ya rushwa serikalini. Na ndicho hicho anachokipigia kelele serikali kwanza izibe mianya ya watu kula rushwa kwanza badala la kuwaacha wale rushwa halafu ujaze makesi mahakamani kwa kifupi Prevention is better than cure.
 
Amesema anashangaa serikali inapambana na rushwa badala ya kurekebisha mfumo (system) inayozaa rushwa, Ikumbukwe alikua kiongozi wa tume inayochunguza mianya ya rushwa serikalini. Na ndicho hicho anachokipigia kelele serikali kwanza izibe mianya ya watu kula rushwa kwanza badala la kuwaacha wale rushwa halafu ujaze makesi mahakamani kwa kifupi Prevention is better than cure.

thanks mie hata sikuwa nimeelewa chochote
 
Katuni hii inaongea maneno 100...!
 

Attachments

  • kpleo.jpg
    kpleo.jpg
    15.5 KB · Views: 48
WAZEE na wafuasi mbalimbali wa muasisi wa taifa la Tanzania, hayati Mwalimu Julius Nyerere, wametuma ujumbe mzito kwa serikali ya sasa, wakisema aina ya uongozi anaoutumia Rais Jakaya Kikwete hauwezi kumfikisha alipokusudia katika kulijenga taifa hili.

Wakongwe hao ambao walifanya kazi na Mwalimu enzi ya utawala wake, walisema kwa nyakati tofauti hivi karibuni kwamba, kama Rais Kikwete hatajenga juu misingi mizuri aliyoiacha Mwalimu ya kuwajibika na kuwatumikia wananchi, hawezi kufikia ndoto yake ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

Wafuasi hao wa Mwalimu walisema, ili serikali iweze kuondokana na matatizo yanayotokea sasa, inabidi itenganishe kazi na urafiki.

Mzee Hassan Nassor Moyo, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi wakati wa serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, alisema Mwalimu Nyerere alifanikiwa kujenga uwajibikaji katika serikali kwa sababu, kamwe hakutegemea mawaziri wake wawe marafiki zake.

“Mwalimu alikuwa akitegemea mawaziri wake washirikiane naye kufanya kazi za watu kinyume na sasa ambako urafiki umetawala katika kazi,” alisema Mzee Moyo.

Kuhusu sifa za uongozi alizokuwa nazo Mwalimu, Mzee Moyo alieleza kuwa Nyerere alikuwa akijua usimamizi wa kazi na alikuwa akifuatilia kwa karibu sana.

"Alikuwa anajua kusimamia na kufuatilia kwelikweli. Akikupa kazi anakuita na kuuliza ulipofikia. Hali hiyo ilisaidia mawaziri wake kuwa wachapakazi. Walikuwa waaminifu kwa vile yeye mwenyewe (Mwalimu) alikuwa mwaminifu,” alisema Moyo.

Moyo alisema kiongozi huyo alifanya kazi kubwa kuliunganisha taifa lililokuwa limegawanyika kutokana na utawala wa kikoloni na kumfanya awe tofauti na viongozi wengi barani Afrika.

Naye mwanadiplomasia wa Kimataifa, Dk Salim Ahmed Salim ambaye pia alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania wakati wa serikali ya awamu ya kwanza baada ya kufariki dunia Edward Moringe Sokoine, akieleza jinsi anavyomkumbuka Mwalimu Nyerere. Alisema Tanzania imepoteza kiongozi shupavu asiye na ubaguzi.

“Ukweli ni kwamba, Mwalimu alikuwa ni kiongozi shupavu. Ni kiongozi ambaye alikuwa hajali mtu bali utu, alikuwa anathamini zaidi mchango wa mtu bila kujali ametoka wapi… Mwalimu hakuwa na ubaguzi, hivyo alifanikiwa kuifanya nchi yetu kuwa moja,” alifahamisha Dk Salim.

Kuhusu kuanguka kwa Azimio la Arusha ambalo Mwalimu Nyerere aliliasisi, Dk Salim alisema anaamini kuwa misingi ya azimio hilo bado haijafa bali watu wanalipuuzia tu.

“Azimio la Arusha lilikuja kwa wakati fulani na lengo lake lilikuwa ni uwajibikaji katika uongozi. Mtu achague kuwa kiongozi au kujilimbikizia mali. Siyo haramu mtu kuwa tajiri na wala Mwalimu hakupinga mtu kuwa na utajiri. Bali alichopinga ni mtu kutumia uongozi alionao kujitajirisha,” alifafanua mwanadiplomasia huyo.

Changamoto nyingine ilitolewa na Waziri Mkuu mwingine wa zamani, Jaji Joseph Warioba ambaye alisema: “Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa wa kufikia makubaliano juu ya jambo na uamuzi ukitolewa unakuwa ni wa vingozi wote. Kwa hivyo suala la uwajibikaji wa pamoja uliwezekana kwa sababu ya uwezo wa kiongozi wa juu wa kuwaweka watu pamoja na kuwa na kauli moja”.

Jaji Warioba alisema tofauti kubwa ya uongozi wa awamu ya kwanza na awamu zilizofuatia ni ile dhamira ya kutumikia umma.

“Mimi nafikiri kwa wakati ule kulikuwa na dhamira ya kutumikia umma. Sasa hivi siasa hizi zimekuwa za ubinafsi mno, yaani ule mkazo wa kutumikia umma umepungua,” alisema Jaji Warioba.

Naye Mzee Rashid Kawawa, maarufu kama Simba wa Vita, aliyemrithi Nyerere Uwaziri Mkuu wa Tanzania mwaka 1966, alisema wakati wao uongozi haukuwa lelemama kwa sababu viongozi wa juu walikuwa wakali sana na kwamba walisisitiza uwajibikaji na kuweka maslahi ya taifa mbele.

“Sisi tulikuwa wakali, ndiyo maana kwenye ahadi 10 za mwana TANU tulisema, ‘rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa’. Hatukuvumilia mtu anayechukua rushwa,” alisema Mzee Kawawa.

Naye Mzee Peter Kisumo aliyewahi kuwa Waziri wa Tawala za Mikoa, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ndani ya CCM enzi za Mwalimu alisema enzi zao kiongozi mbovu alikuwa havumiliwi ilikuwa lazima wamjadili na kumwajibisha.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema anamkumbuka muasisi wa Taifa hili, Julius Nyerere kwa kuongoza taifa kwa uadilifu tofauti na sasa ambapo viongozi wengi wanakiuka miko ya maadili ya uongozi.

"Uadilifu ni silaha inayowezesha kutunza raslimali za nchi, lakini kutokana na kwamba sasa hakuna uadilifu rasilimali zetu zimeanza kutoweka," alisema.

Naye Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alimtaka Rais Kikwete kuongeza kuandaa kuwa na mjadala kuhusu mwelekeo wa taifa, kuliko kusubiri nchi ikumbwe na umwagaji damu kama uliotokea visiwani Zanzibar mwaka 2001 na kusisitiza kwamba, muda wa kuyatekeleza kwa vitendo maneno yaliyozungumzwa na Mwalimu Nyerere umewadia.

Mbatia alisema tabia ya baadhi ya viongozi kuwa wabinafsi na kujiona wao wana haki kuliko watu wengine kutalipeleka taifa katika hatua mbaya.

“Hivi sasa mwitikio wa wananchi katika upigaji kura umeshuka kwa kiwango kikubwa kutokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi. Hivi sasa Tanzania kuna pengo kubwa sana kati ya walionacho na wasionacho,” alisema Mbatia na kuongeza:

“Nyerere alisisitiza suala la utu wa mwanadamu katika maslahi yake binafsi, hivyo suluhu ya nchi hii ni kila mtu kuwa na utu na huo ndiyo utakuwa utekelezaji wa yale aliyoyasema Mwalimu.”

Naye Mwenyekiti chama cha United Democratic (UDP), John Cheyo alisema umoja wa kitaifa ulioachwa na Mwalimu Nyerere umeendelea kutoweka kila kukicha.

“Mwalimu alikuwa mtu mwema sana, hakika tutamkumbuka kwa mambo mema aliyoyafanya hasa suala hili ya kujenga umoja wa kitanifa ambalo hivi sasa viongozi wetu wameendelea kulichafua,” alisema Cheyo.

Alisema nguvu ya umoja wa kitaifa ikishamiri katika nchi fulani, viashiria vya kiuchumi huonekana dhahiri kwani masuala ya ufisadi, maadili mabaya ya uongozi yanakosa nafasi kwa viongozi wenye nia ya kutafuta umoja wa kitaifa. Habari hii imeandikwa na Hawra Shamte, Rashid Kejo, Peter Edson, Fidelis Butahe, Zaina Malongo.
 
Back
Top Bottom