Mawaziri wagundua namna ya kuliteka bunge na kupitisha hoja kirahisi.

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
2,293
1,170
Kwa mtizamo wa bunge la sasa ambalo wabunge wengi wameamua kuingia likizo ya kufikiri, sasa uwaziri ni mteremko kabisa. Hata kama kuna mambo ya msingi ya kujadili yanayoweza kujadiliwa, wazili akiamua, anatengeneza skandali ya uzushi au ya kweli, wabunge wanapokea na kujadili bila kurudi kwenye mambo mengine ya msingi. Sasa jiulizeni wana jf, kama waziri hajatengeneza agenda mawaziri hawa watajadili nini? Mfano mzuri ni wizara ya nishati na madini. Asilimia karibu mia moja ya waliochangia bungeni waliishia kujadili tuhuma za rusha bungeni wakiacha nadhani kwa umbumbu wao mambo ya msingi yanayolitafuna taifa kama mikataba ya iptl, na mingine mingi. Hata kama tuhuma za rushwa zipo kulikuwa na haja gani kila mbunge kurudia hayohayo kama kasuku? Kweli hawa wabunge walikuwa wamejiandaa kuchangia ili kuleta ufumbuzi katika wizara hii yenye utata mkubwa? Hapa ndo muhongo alichansi na kuonyesha kweli ni profesa. Ukitaka kuiba unamtupia mbwa mfupa anahangaaika nao anasahau majukumu yake unapita kiulaini unaiba. Wabunge walitupiwa mfupa.
 
Walioyajadili ndio wapiga kura tunataka kuyasikia I mean tunapendezwa na umbeya nasio fact hehehehe mtu hunyimwa hela sio maneno babu eeeh
 
Yaani 'case' moja tu ya bajeti kupitishwa kirahisi ndiyo inabeba 'conclusion' kuwa mawaziri wote wamepata njia ya kupitisha bajeti zao kirahisi?
 
hapa ndipo mtarudi muelewe zitto kabwe ni injini kubwa, serikali imefanya ujanjanja wa kuhamishia attention ya bunge zima kwenye ishu ya rushwa wakaacha kujadili mambo ya msingi ya nishati na madini , namuunga mkono zitto kwa kuibua hoja ya ukiukwaji wa sheria uliofanywa na waziri kuhusu manunuzi ya umma ipo siku mtaona gharama ya hiyo inayoitwa maslahi ya umma , wabunge wanaendeshwa na upepo hili ni janga lingine la kimataifa
 
Back
Top Bottom