Mawaziri waghushi vyeti

Tatizo la mawaziri wa JK ni kujieleza na kuwaridhisha wananchi kwa level ya elimu yao waliyonayo. kila siku waziri mmoja anaburunda kwa kushindwa kufanyia analysis maelezo yake kabla ya kuyatoa
 
Pia ningemshauri mheshimiwa waziri achukue darasa la Kiingereza na Public speech. He is lacking in both.

Mkuu sio Speech tu....Huyu Bwana Mkubwa kamala mambo haya yakiendelea yatamuweka wazi,Nilishindwa kuelewa kabisa ilikuwaje akapata nafasi hii ya Uongozi,Ni mgumu kujieleza hata kwa Resume yake mwenyewe,Kuna ziara walifanya US wakiandamana na Chiligati,Masha,Nchimbi na RC Kandoro,alishindwa kabisa kujieleza,Nilipata Mshtuko kuona kuwa inakuwaje Viongozi wanakuja kwenye Mikutano na wanakuwa hawajajajiandaa kabisa,inatudhalilisha kwa hawa wanaoandaa hii mikutano,na matatizo ya kiongozi mmoja yanatoa picha ya anaowawakilisha...
 
Mwawado,

Si ndo wanajifunza? Rome was not built in a day...sasa wote wawe kama Mwapachu wa EAC? ila mzee huyu ni kiboko ktk kukata issue..namkumbuka akiwa Chair wa Council UDSM mid 90's! Lo! Wakati wa miaka 25 ya UD na Mwalimu ndo alikuwa mwongeaji rasmi!

Mwapachu aliongea safi bila hata kudesa hata Mwalimu akampigia makofi!

Turudi ktk mada..kweli Hawa Viongozi saa ingine hawajiandai! sijui usiku au asbuhi kwa nini asitumie 1 or two hours kujiweka sawa?
 
Hapo kwenye kiingereza, jamani watanzania tuna tatizo tupende tusipende. Elimu tunaweza kuwa nayo ila lugha ya malkia inautata. Nilishuhudia phd defence ya mtz ambaye nilikua nam-admire academically kumbe kuunganisha sentensi zilizonyooka kwa mtiririko ni taabu nikabaki kusinyaa kwenye kiti kwa niaba yetu sote. Saa nyingine wa-KE wakitusema kuna kaukweli

Mke wa mangi(Nkamangi),

Mimi sioni shida mtu kama hawezi kuzungumza kiingereza hata kidogo awe na pHD ama bachelor. Mimi nadhani ni sisi watanzania tu tunataka kuzungumza kiingereza kama waingereza, jamani tembeeeni muone

Nenda Poland, France, Ujerumani, Denmark, Sweden, Russia na nchi nyingine za ulaya na hata zilizokaribu na uingereza, wanazungumza kiingereza kibaya kuliko hata sisi na wala hawajisikii vibaya maana watakuambia its not our first language. Wala hawatumii nguvu nyingi kujifunza maana anakuambia akiweza tu kupeleka ujumbe aliokusudia unatosha.

Lakini napata shida saaaaaaaaaaaana ninapoona mtu anaongea kiswahili broken. Mbona hamjivunii kuongea kiswahili safi kuliko swahili speakers wengine? Wakenya kweli wanatucheka maana wao wako better-off ukilinganisha nasi, lakini wanakiri sisi tuko mbali zaidi yao kwa kiswahili tena lugha yetu sisi waafrika.

Je lini tutajivunia lugha yetu kiswahili? Ni kwanini tunaabudu vya kizungu????

Kinachoniudhi zaidi unakutana na mmbongo huku ugaibuni bado anakusemesha kwa lugha ya wenyeji wakati tunaweza kuzungumza kiswahili saaaaaafi.....

Kidumu Kiswahili, Idumu lugha yetu ya kiafrica idumu lugha yetu ya Taifa
 
Professor Mayunga Nkunya, kiongozi waTanzania Commission for Universities anasema hawa wenye vyeti feki feki wamekuwa "trapped." Hawakupata "ushauri wetu."

Sio kosa lao!

So, what you got here, is a kilaza professor leading a battle against vilaza scholars.

Kuhani nadhani most of these guys wakati wanafanya hizo Phd zao TCU either ilikuwa haipo au ilikuwa kwenye drawing boards, why ...kwa sababu inaonekana TCU imezaliwa na Universities Act, No. 7 ya 2005.....Bofya TCU Website

Kwa hiyo huyu Profesa Nkunya either alikuwa anapayuka au alitaka kujizolea ujiko tu kwenye hii issue.
 
Mke wa mangi(Nkamangi),

Mimi sioni shida mtu kama hawezi kuzungumza kiingereza hata kidogo awe na pHD ama bachelor. Mimi nadhani ni sisi watanzania tu tunataka kuzungumza kiingereza kama waingereza, jamani tembeeeni muone

Nenda Poland, France, Ujerumani, Denmark, Sweden, Russia na nchi nyingine za ulaya na hata zilizokaribu na uingereza, wanazungumza kiingereza kibaya kuliko hata sisi na wala hawajisikii vibaya maana watakuambia its not our first language. Wala hawatumii nguvu nyingi kujifunza maana anakuambia akiweza tu kupeleka ujumbe aliokusudia unatosha.

Lakini napata shida saaaaaaaaaaaana ninapoona mtu anaongea kiswahili broken. Mbona hamjivunii kuongea kiswahili safi kuliko swahili speakers wengine? Wakenya kweli wanatucheka maana wao wako better-off ukilinganisha nasi, lakini wanakiri sisi tuko mbali zaidi yao kwa kiswahili tena lugha yetu sisi waafrika.

Je lini tutajivunia lugha yetu kiswahili? Ni kwanini tunaabudu vya kizungu????

Kinachoniudhi zaidi unakutana na mmbongo huku ugaibuni bado anakusemesha kwa lugha ya wenyeji wakati tunaweza kuzungumza kiswahili saaaaaafi.....

Kidumu Kiswahili, Idumu lugha yetu ya kiafrica idumu lugha yetu ya Taifa

Mkuu Kichakoro....
Sema wewe kiazi... mimi mhogo nitaambiwa nina mizizi..
Ahsante sana kwa mchango wako. Unajua Nkamamangi anawakilisha asilimia karibu 90% ya mawazo ya Watanzania = Kujua kuzungumza Kiingereza ni usomi. Mara nyingi ninaposafiri nchi kama France, Sweden, Germany.. asilimia kubwa ya maafisa uhamiaji ninaokutana nao wanaongea Kiingereza cha kubabaisha! Tanzania tuna nini na Kiingereza.... Naona itachukua karne nyingine mbili makovu ya utumwa kufutika.....
 
Huyu Kamala anadanganya, anajua wazi hicho chuo hakitambuliwi na NARIC.

Waandishi si fuatilieni NARIC na kujua ukweli wote?

Unafikiri Commonwealth Open University ingelikuwa inatambuliwa na NARIC wangeshindwa kuonyesha kwenye website yao?

Details hizi hapa kama kuna mtu anataka kuwasiliana nao.

UK NARIC - Contact Us
 
Kwa vyovyote vile nashindwa kuelewa uamuzi wake wa kufanya PhD nyingine MU. Kama kweli Kamala anaamini PhD yake ni safi (genuine) kwa nini anaanza kufanya nyingine haraka haraka? Kwa mtu anayejua PhD nini, sioni kama anaweza kukimbilia chuoni kusoma tena akiwa na majukumu makubwa kama ya uwaziri! Hapa anatuongezea mashaka juu ya shule yake. Uwezo wake naukubali toka akiwa sekondaru ila sijamwelewa na inanipa shida kuamini kwa nini aliamua kutafuta PhD ya dezo ambayo sasa inamwingiza kwenye kashfa!
Baada ya ile thread ya Mzumbe jamaa kakomalia kusafisha PhD yake huko? Huyu jamaa naona anapenda kuitwa Doctor of philosophy lakini naona ataishia na MPhil.
 
Mke wa mangi(Nkamangi),

Mimi sioni shida mtu kama hawezi kuzungumza kiingereza hata kidogo awe na pHD ama bachelor. Mimi nadhani ni sisi watanzania tu tunataka kuzungumza kiingereza kama waingereza, jamani tembeeeni muone

Nenda Poland, France, Ujerumani, Denmark, Sweden, Russia na nchi nyingine za ulaya na hata zilizokaribu na uingereza, wanazungumza kiingereza kibaya kuliko hata sisi na wala hawajisikii vibaya maana watakuambia its not our first language. Wala hawatumii nguvu nyingi kujifunza maana anakuambia akiweza tu kupeleka ujumbe aliokusudia unatosha.

Lakini napata shida saaaaaaaaaaaana ninapoona mtu anaongea kiswahili broken. Mbona hamjivunii kuongea kiswahili safi kuliko swahili speakers wengine? Wakenya kweli wanatucheka maana wao wako better-off ukilinganisha nasi, lakini wanakiri sisi tuko mbali zaidi yao kwa kiswahili tena lugha yetu sisi waafrika.

Je lini tutajivunia lugha yetu kiswahili? Ni kwanini tunaabudu vya kizungu????

Kinachoniudhi zaidi unakutana na mmbongo huku ugaibuni bado anakusemesha kwa lugha ya wenyeji wakati tunaweza kuzungumza kiswahili saaaaaafi.....

Kidumu Kiswahili, Idumu lugha yetu ya kiafrica idumu lugha yetu ya Taifa

Kwanza naomba nijaribu kurekebisha kama sijakosea ni Nkamangi ni Binti wa Mangi na si Mke wa mangi.
Back to the point ni kwamba nakubaliana na wewe kwa kiasi flani lakini bado kuna pointi nataka nigusie(rejea highlights)
Kwanza masomo hayo ya phd watakuwa wamepata kwa lugha ya kiingereza na hivyo kuweza kuilewa topic ni lazima ailewe lugha la sivyo itakuwa ni cramming.
Wenzetu wa mataifa hayo uliyoyataja mitaala yao ni kwa lugha zao kutokana na maendeleo waliyofikia,sisi sivyo kabisa na unaelewa kuwa ni kiswahili hadi std 7 then ndio english.
Pia kwa kumalizia licha ya kwamba na mimi nakifagilia kiswahili kwasababu inaonyesha utambulisho wa mwafrika kwani inaunganisha jamii kubwa ya kiafrika...Hata hivyo si kweli kwamba kiswahili ni lugha ya kiafrika...Kibantu ndo kiafrika asili lakini kibantu plus kiarabu ndio unapata kswahili.
 
Mke wa mangi(Nkamangi),

Mimi sioni shida mtu kama hawezi kuzungumza kiingereza hata kidogo awe na pHD ama bachelor. Mimi nadhani ni sisi watanzania tu tunataka kuzungumza kiingereza kama waingereza, jamani tembeeeni muone

Nenda Poland, France, Ujerumani, Denmark, Sweden, Russia na nchi nyingine za ulaya na hata zilizokaribu na uingereza, wanazungumza kiingereza kibaya kuliko hata sisi na wala hawajisikii vibaya maana watakuambia its not our first language. Wala hawatumii nguvu nyingi kujifunza maana anakuambia akiweza tu kupeleka ujumbe aliokusudia unatosha.

Lakini napata shida saaaaaaaaaaaana ninapoona mtu anaongea kiswahili broken. Mbona hamjivunii kuongea kiswahili safi kuliko swahili speakers wengine? Wakenya kweli wanatucheka maana wao wako better-off ukilinganisha nasi, lakini wanakiri sisi tuko mbali zaidi yao kwa kiswahili tena lugha yetu sisi waafrika.

Je lini tutajivunia lugha yetu kiswahili? Ni kwanini tunaabudu vya kizungu????

Kinachoniudhi zaidi unakutana na mmbongo huku ugaibuni bado anakusemesha kwa lugha ya wenyeji wakati tunaweza kuzungumza kiswahili saaaaaafi.....

Kidumu Kiswahili, Idumu lugha yetu ya kiafrica idumu lugha yetu ya Taifa

Mkuu Kichakoro usichanganye issues, suala ni ile PhD hata angeipeleka "TBS" haina viwango vinavyo stahili.Bahati nzuri chombo kinacho shughulikia suala hili TCU kimesha toa msimamo wake.
Inatia shaka zaidi kwa kuwa tumemsikia Mh Kamala mara nyingi akizungumza incoherent english kwenye luninga.
Nchi ya Tanzania bado ni Anglophone, toka secondary hadi Chuo kikuu.Kwa kile anacho display mheshimiwa ni kichekesho kwani hiyo PhD aliifanya kwa kiswahili?, na hii ni licha ya kuwa sikipondi kiswahili.
Viwango vya vyuo vinavyoheshimika Uingereza au Commonwealth vinajulikana.
 
Nani kakupa mamlaka hayo?
Fuatilia wewe umwage data hapa......

Hivi hata kama huna cha kuongeza kwenye mjadala lazima uandike?

Kama hutaki link niliyotoa lala mbele, toka lini kutoa link au kuwaambia waandishi wafuatilie kunahitaji authority?
 
arrg kutoa link ndio umefuatilia? wewe vipi aisee?
 
What PhD are you talking about here?
...is that Pombe Haina Deni? or
...Poor Hair Ditribution?
Mjadala hauna mantiki hasa kwani tunachotakiwa ni kujua kama hao PhD holder walizipata PhD zao kwa kufuata taratibu halali za Chuo au Taasisi husika
Pili, iko haja pia kujua nini maana ya 'fake Phd'
Vinginevyo huu mjadala utajifia bila ya conclusion yenye maana yoyote dhidi ya muda utakaokuwa umetumika.
 
Last edited:
Wahenga husema.."kwenye kundi la mamba na kenge wamo".....inauma sana ndugu zangu wana JF..watu tunalala darasani tunavimba macho kwa kusoma (Masters & PhD)..lakini wanatokea wajanja kama hao wanatafuta Masters & Phd Feki..then wanaanza kuitambia jamii...

Wengi wao wanatembea na mabango ya PhD usoni mwao ili kila mtu afahamu kwamba wana PhDs...Lakini watu ambao wamesomea taaluma zao kwa njia halali wala hawana muda wa kuinadi elimu yao.....kwani wanafahamika tu.

Mtu anaenda kusoma Masters kwa tarumbeta na vinubi (Mrema)..utafikiri anaenda kuchukua bingo...kama si ukanyabwoya ni nini???

Sasa wameishajijua kwamba tumewatambua...hii itapunguza mbwembe na mikogo yao kwenye jamii.......
 
Mi nafikiri huku si kudefend ila ni kutolea maelezo, kudefend alitakiwa kuomba "Viva" TCU. Yaani asubmit thesis yake TCU halafu wakamu examine in form of interview. Akiweza kutoa maelezo ya kuridhisha na wakayakubali na kumtambua hapo atakuwa amedefend PhD

I dont think kama TCU ni academis institution ambayo inaweza kukupa PhD. Kwani sio chuo. Je iwe kwa akila aliyepata Shahada nje a defend Thesis TCU?
Angetoa maelezo na ikiwezekana kama msomi basi hata aelezee kwa kina alifanya utafiti juu ya nini na na wapi. Hata aoneshe Real Thesis. Na utendaji wake uonekane kama msomi sio kukurukupuka tu na majibu ya kisiasa na ujanjaujanja tu.
 
I dont think kama TCU ni academis institution ambayo inaweza kukupa PhD. Kwani sio chuo. Je iwe kwa akila aliyepata Shahada nje a defend Thesis TCU?Angetoa maelezo na ikiwezekana kama msomi basi hata aelezee kwa kina alifanya utafiti juu ya nini na na wapi. Hata aoneshe Real Thesis. Na utendaji wake uonekane kama msomi sio kukurukupuka tu na majibu ya kisiasa na ujanjaujanja tu.

Tupo ukurasa mmoja kama TCU imeweza kupigia kelele viwango na kuwataka wahusika warudi vyuoni kusoma tena ni dhahili kuwa itabidi wapitie mkondo niliotoa hapo juu. Sikutaka kumpeleka UDSM najua uwezo wake ni mdogo hata chomoka na huko Mzumbe anakosoma wanaomsimamia wana sifa kama zake.

Kwa kuwa yeye sasa hivi si academician basi hawa hawa TCU ambao wamediscredit PhD yake wanaweza kumfanyia hiyo viva, kwani watendaji wake karibu wengi ni Academicians pale UDSM.
 
Mke wa mangi(Nkamangi),

Mimi sioni shida mtu kama hawezi kuzungumza kiingereza hata kidogo awe na pHD ama bachelor. Mimi nadhani ni sisi watanzania tu tunataka kuzungumza kiingereza kama waingereza, jamani tembeeeni muone

Nenda Poland, France, Ujerumani, Denmark, Sweden, Russia na nchi nyingine za ulaya na hata zilizokaribu na uingereza, wanazungumza kiingereza kibaya kuliko hata sisi na wala hawajisikii vibaya maana watakuambia its not our first language. Wala hawatumii nguvu nyingi kujifunza maana anakuambia akiweza tu kupeleka ujumbe aliokusudia unatosha.

Lakini napata shida saaaaaaaaaaaana ninapoona mtu anaongea kiswahili broken. Mbona hamjivunii kuongea kiswahili safi kuliko swahili speakers wengine? Wakenya kweli wanatucheka maana wao wako better-off ukilinganisha nasi, lakini wanakiri sisi tuko mbali zaidi yao kwa kiswahili tena lugha yetu sisi waafrika.

Je lini tutajivunia lugha yetu kiswahili? Ni kwanini tunaabudu vya kizungu????

Kinachoniudhi zaidi unakutana na mmbongo huku ugaibuni bado anakusemesha kwa lugha ya wenyeji wakati tunaweza kuzungumza kiswahili saaaaaafi.....

Kidumu Kiswahili, Idumu lugha yetu ya kiafrica idumu lugha yetu ya Taifa

Hao unaowasema wamepata elimu zao kwa lugha zao; na wana haki kabisa kujivunia lugha zao. Suala hapa kwetu elimu tangu Sekondari hadi PhD ni kiingereza; inaleta shida kujifunia hiyo elimu kwa sababu hukupata kwa lugha ya kiswahili. Lugha ni msingi wa Elimu yoyote ile, kama huna ufasahaa na uelewa wa lugha, utamudu vipi unachosoma?
 
Mimi naona kama kuna tatizo sehemu fulani.....maana kama UK wanavitambua na sisi Tz hatuvitambui nini ni nini hapo??mbona napata kigugumizi kujau nani anasema ukweli na nani ana viwango sahihi???anyway inabidi tujiridhishe na viwango toka kwenye accredition office ndani ya nchi......ila vigezo vijulikane.maana nami nataka kusoma Masters yangu natafakuri nisije nikaingia mkenge
 
Back
Top Bottom