Mawaziri, wabunge waongoza kusamehewa kodi

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
SIKU chache baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwasilisha ripoti yake bungeni ikionyesha ongezeko la misamaha ya kodi, imebainika kuwa mawaziri na wabunge ni miongoni mwa vigogo wanajinufaisha na Sheria ya Msamaha wa Kodi kinyume cha taratibu.

Orodho ya majina ya watu waliosamahewa kodi na Serikali katika mwaka wa fedha 2009/2010 iliyopo katika tovuti ya Wizara ya Fedha, inaonyesha majina ya baadhi ya mawaziri, wabunge na wakuu wa taasisi za Serikali wakiwa wamenufaika na misamaha hiyo.

CAG Ludovick Utouh katika ripoti yake, anasema misamaha ya kodi iliyotolewa kwa taasisi mbalimbali, hadi kufikia Juni 30,2011 ni Sh1.02 Trilioni na kueleza kuwa eneo hilo la misamaha ya kodi linapaswa kutazamwa ili kuepuka kuwa na makusanyo pungufu ya kodi. Hatua ya Serikali kuruhusu kutolewa kwa misamaha ya kodi inayofikia asilimia 18 ya makusanyo yote ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewashtua wananchi, wasomi na wanasiasa ambao sasa wanahoji umakini wa Serikali.

Hata hivyo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Kijjah aliliambia Mwananchi Jumapili jana kuwa misamaha ya kodi ipo kisheria na kwamba kila mmoja ana haki ya kuipata.

Maoni yangu
Nchi nyingi za Ulaya na zilizoendelea zimeweza kufikia hapo kwaumakini wao wa kukusanya kodi na kuzitumia kodi kwa uadilifu mkubwa kwenye kuleta maendeleo kwa walipa kodi/wananchi wao. Hapa kwetu suala la makusanyo ya kodi limegubikwa na wingu kubwa la siasa na ubabaishaji. Hatuwezi kuwa na uchumi imara kama tax base yetu ipo porous kama ilivyo sasa. Misamaha ya kodi kwa sababu gani hasa hadi ifike 1 Trillion+???

Ni vyema sheria ya misamaha ya kodi ikaangaliwa upya. Zipo taasisi ambazo zinapewa misamaa ya kodi basically kwa ajili ya kupunguza gharama watakazo zitoa lakin matokea yake gharama zimekuwa doubled/tripled. Hii si sawa mana tunapoteza bure mapato ya serikali kwa kuwapa misamaa ya kodi watu walanguzi. Kwa mfano St. schools + seminary schools hizi zina misamaha ya kodi, lakin ndio zinaongoza kwa ada kubwa kuliko kawaida. Mimi nadhan ni bora walipe tu kodi na hayo maada yao hata wakiongeza tutajua huko huko mbele maana inaonekana msamaha wa kodi haujasaidia kushusha gharama za huduma zao.

Wabunge na mawaziri wanaongoza kwa misamaha ya kodi na ukwepaji kodi sababu posho ambazo ni mara tatu ya mishahara yao hazikatwi kodi. Hii ni dhuruma. Haiwezekan mtu analipwa mshahara kwa mwezi laki 2 na anakatwa kodi, mbunge analipwa posho ya TZS 5M kwa mwezi na haikatwi kodi. Kuna haja ya kuwa wakali kwa wakwepa kodi, vinginevyo kila mtu atakuwa attracted kukwepa kodi. Lipa kodi kwa maendeleo ya Taifa lako, ifike mahala watu waone aibu kwa kukwepa kodi. Wenzetu walioendelea suala la kulipa kodi limekuwa ni kama culture na mtu anajisikia vibaya asipolipa kodi, huku kwetu mtu akilipa kodi anajisikia vibaya. Kuna haja ya kuchange hii paradigm otherwise maendeleo tutayaona kwenye TVs.
 
Hivi ishu ni Utouh kweli???Mimi nadhani Serikali kwa ujumla wake haina nidham ya kukusanya mapato na kufanya matumizi. Na inawezekana hawajui linki iliyopo kati ya ukusanyaji wa mapato/kupanga na kusimamia matumizi na maendeleo ya taifa. Ingejua strong link iliyopo hapo, ingecapitalize hapo kutuletea maendeleo.
 
Unamwonea bure CAG, janga la kitaifa atakuwa huyu Katibu Mkuu anayetetea hii misamaha.

Na wewe utakuwa unamwonea huyo Katibu Mkuu ilihali yeye anatetea au anasimamia sheria. Wa kulaumiwa hapa ni hao waliopitisha hiyo sheria kwa sauti kubwa za NDIOOOOOOOOOOOOOOOOOO bila hata kutaka kujua zingekuwa na athari gani kwa taifa.

Juzi Mnyika kapendekeza mapato yote ya taasisi na mashirka ya umma yadhibitiwe lakini cha ajabu wabunge wa magamba wakapinga. Ndugu yangu, janga kuu la taifa hili ni Bunge na as long as majority humo wataendelea kuwa magamba nchi itaendelea kuteketea. Tumewapa mamlaka yote ya kuisimamia na kuiwajibisha serikali lakini hawaonekani kujua wanachotakiwa kukifanya.
 
Mbunge/waziri anatoa wapi moral authority ya kuilalamikia kampuni zinazoneemeka na msamaha wa kodi ikiwa na yeye ni miongoni mwao?yaani yeye anapata posho ambazo hazitozwi kodi huku tunaolipwa mshahara wa laki na nusu tukikatwa kodi halafu eti wanasema wanaenda bungeni kututetea?Hii nchi bado ina safari ndefu kuja kufikia kwenye maendeleo ya kweli.
 
ndo maana wanaingua kwenye siasa, ili kutetea maslahi yao, biashara zao na si kutetea wananchi......
 
Back
Top Bottom