Mawaziri wa JK wapeana kavukavu mbele ya wananchi: Ni Mkulo na Magufuli

Its ok, but sithani kama kukopi na kupest habari za magazitini kama zilivyo ni sahihi kwenye JF
Nyie wabongo hamueleweki, ukiletewa habari kavukavu utauliza source, ukiletewa live from the source napo mnaibua hoja. Habari zisipokuja humu ndani tutakosa burudani jamani, tuache watu waweke kila wanachokiamini
 
Tuwe wakweli hata kama mtu ana makando kando yake lakini Pombe Magufuli ni jembe, ni mtendaji haswaa! Wengi wanao mwandama au kumuhujumu, hasa viongozi wenzie, ni hofu juu ya uchapaji kazi wake. Tumwombe Mungu ili Jakaya amrudishe tena katika baraza la mawaziri hasa katika wizara aliyopo sasa au hata uwaziri mkuu.

Kibanga Msese
 
My take:
Hivi maadili kwa viongozi ya Ngurudoto yaliishia wapi au ndo nini: huku nje twaona haya huko ndani kukoje????????

baraza la ,mawaziri magufuli anajua mwenzie hawako naye na ndiyo maana kaanza kumponda...............kufa kufaana.........
 
Hazina yenyewe imefulia vibaya sasa sijui watatoa wapi za kulipa...nchi hiii kweishneeeee

Kaka nawe umeshadanganyika serikali haina pesa kama haina pesa hizo zinazoibiwa zimetoka wapi? Fedha ambazo hawana ni za kutoa huduma kwa walalahoi mimi na wewe tu mbona safari hazikwami usidanganyike tanzania ina fedha lukiki ndiyo maana bro Pombe anang'aka kilichoko huko juu ni urasimu tu pesa ipo kibao.
 
Nyie wabongo hamueleweki, ukiletewa habari kavukavu utauliza source, ukiletewa live from the source napo mnaibua hoja. Habari zisipokuja humu ndani tutakosa burudani jamani, tuache watu waweke kila wanachokiamini

Naye huyo asitusumbue hapa! Akiona habari ni ndefu si apite kimya kimya!
 
Ingekuwa hazina imefilisika rais asingekuwa anasafiri na bunge lisingeendelea maana posho ingekata.

Kaka mweleze huyo mawaziri wanaiba mabilioni kibao na nhayo tunayotangaziwa ni robo tu ambayo yameingia kwenye utaratibu rasmi fedha zingine zinapigwa juu kwa juu Tanzania fedha ipo jamani tusidanganyane na kuaminishwa eti sisi ni maskini sitaki kuubali ujinga huo
 
Watu wa pwani tuna imani kubwa sana kwa watu wenye vipala original maana vingine ni vya kutengeneza kwa vinyozi. Huwa wanafanya mambo exactly kama Mkulo. Ni magenius wa mambo yasiyoweza kuelezeka!
 
Acheni Magufuli afanye hivyo maana hata yeye anajua kuwa Mkulo ni mzigo kwa taifa na hakika anatulemea, hajui la kufanya zaidi ya kukwamisha utendaji wa wizara zingine.
 
Sasa kama serikali haina hela Magufuli analifahamu hili anategemea Mkulo afanye nini kama sio kujikosha kwa wananchi. Kwani akimsemea kwa JK kuna jipya litakalokuja au ni kujisemelesha kwa Magufuli ili wananchi tujue anafanya kazi akwende zake tushamchoka naye
 
Its ok, but sithani kama kukopi na kupest habari za magazitini kama zilivyo ni sahihi kwenye JF
Kweli mkuu kwani magezeti watu tumeisha soma sasa mambo ya kurudia yanini ni vizuri ndani ya JF tukapata habari mpya ambazo bado hazijatoka kwenye magazeti(za leo leo)
 
Hazina yenyewe imefulia vibaya sasa sijui watatoa wapi za kulipa...nchi hiii kweishneeeee
Una uhakika na unachokisema kumbuka mgodi mmoja tu wa Geita kwa wiki Dhahabu ya Tsh.850,000,000,000/= inasafirishwa fuatilia kiasi cha dhahabu kile ambacho kilitaka kuporwa na yale Majambazi.
 
Its ok, but sithani kama kukopi na kupest habari za magazitini kama zilivyo ni sahihi kwenye JF

Mkuu, mimi naona hakuna tatizo lolote, kumbuka siyo kila Mtazania ana access ya kusoma gazeti la kila siku; na wengine wako mbali sana na DSM kiasi kwamba inaweza kuchukua siku tatu kabla ya gazeti kuwafikia.
 
TRA inashangaza sana ngano na sukari za bakhresa na metl zenye misamaha inapita mara moja,vifaa vya ujenzi wanazuia

Mkuu, wafanya biashara wako very powerful nchini mtu unaweza kufikili labda na wenyewe ni tawi Serikalini - ndiyo maana Kambarage alikuwa afanyi utani NAO.
 
..huu sasa ni upuuzi.

..i dont care uko kwenye serikali ya CCM au CDM lakini mawaziri hawapaswi kulaumiana kwenye vyombo vya habari.

..huyu Magufuli ni domo kaya, hana nidhamu.
 
..huu sasa ni upuuzi.

..i dont care uko kwenye serikali ya CCM au CDM lakini mawaziri hawapaswi kulaumiana kwenye vyombo vya habari.

..huyu Magufuli ni domo kaya, hana nidhamu.

Hapa unenena shida hawataki kutofautiana na rais wao kila waziri anataka kujisafisha kwa wananchi nani amekwamisha wizara husika
 
Back
Top Bottom