Tetesi: Mawaziri wa Kikwete: Lazaro Nyalandu, na Jumba la karibu milioni 600 Arusha!

Enigma

Senior Member
Feb 29, 2008
109
62
Baada ya mawaziri wawili wa JK kuhusishwa na umiliki wa majumba/makazi ya mamilioini ya shilingi muda mfupi tu baada ya kushika nafasi zao Waziri mwingine anatajwa kumilimi jumba kubwa ambalo vyanzo vyetu vinakisia thamani yake kuwa ni zaidi ya nusu bilioni. Kutokana na vyanzo hivyo vya kuamika jumba hilo liko kwenye Elkirevi, Kitongoji cha Olorukwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya ndani kabisa eneo hilo linadaiwa kuwa lilipatikana baada ya Bw. Nyalandu kununua ardhi yenye eneo la Eka 3 hivi kutoka kwa wanavijiji watano. Jumba lenyewe limejengwa chini ya mwaka mmoja na kukamilikama mwishoni mwa 2011. Jumba limezungushwa na ukuta wa karibu futi 10 na juu yake inadaiwa limewekwa waya wa umeme (electric fence)

Ni kwenye jumba hili ambapo Bw. Nyalandu alifanyia Sherehe ya Mwaka mpya na bila ya shaka ilikuwa ni 'house warming' party. Taarifa hizi zinaendana na zile za mawaziri wengine ambao tayari habari zao za umiliki wa majumba yenye thamani kubwa kuliko vipato vyao na walizopata ndani ya muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Mawaziri wengine ni Bw. Maige na Ngeleja ambao wote thamani ya nyumba zao zinakaribia shilingi bilioni 1!

Hata hivyo hadi hivi sasa Tume ya Maadili ya Viongozi haijaonesha kujua mambo haya wala kufuatilia na kuyaweka wazi kama wanazo taarifa na kama kweli vyote hivyo vinaendana na mishahara yao.
 
Mkuu Enigma dah longtime sijakuona jamvini humu, karibu tena! najua ukija huwa unakuja na vitu vizito sana. Hii nchi inahitaji kukombolewa haswa toka kwa hawa mafisadi, upepo unavumia upande mzuri atleast! kwa hiyo by 2015 tunahope tutajikomboa toka kwa hawa mafisadi na kuwapeleka wote mbele ya pilato!
 
Siyo jambo baya kwa mawaziri wetu kujenga au kununua majumba mazuri, ila tu pale majumba hayo yanapojengwa kwa kutumia raslimali za nchi kutokana na matumizi mabaya ya nafasi zao za uwaziri.

zaidi ya mshahara wa waziri na posho zake ambazo haziwezi zidi m7 kwa mwezi. Kuna kipato gani zaidi cha kumuwezesha mtu kujenga nyumba ya b1 kwa kuzingatia na maisha mengine yanaendelea?
 
mawaziri wana tabia ya kujilipiza allowance nyingi kupita vipato vyao vya halali. Allowance ya siku moja inazidi hata 7m
 
Speaker Anna Makinda upo hapo? Na hao ni miongoni wa uliotaka waongezewe posho? Unashindwaje kujua hizo hujuma ndiyo zinatufanya tuwe wakali dhidi yenu mnapoomba kuongezewa posho?
 
Mimi sishangai kwa huyu Lazaro kuwa jumba la thamani hiyo,kwasababu ana pesa ndefu kabla hata hajawa mbunge na hatimaye waziri,japo hili halimzuhii kufuja mali za umma.Na kama mchangiaji mmoja alivyododosa tatizo ni utumiaji rasilimali za nchi kufanya mambo binafsi kama hayo.kama mleta uzi ana ushahidi hata wa kimazingira tu,aumwage hapa ili huu uzi usikae kiswaziswazi.
 
Hii ni hatari,tunge msamwel doe huyu laana mkubwa jk.Jamani wtz tuungane kupinga ufisadi kwa vitendo.
 
Siyo jambo baya kwa mawaziri wetu kujenga au kununua majumba mazuri, ila tu pale majumba hayo yanapojengwa kwa kutumia raslimali za nchi kutokana na matumizi mabaya ya nafasi zao za uwaziri.

ni kweli kamanda, tatizo ni namna zinavyojengwa au kununuliwa na mahesabu halali ya kazi zao

kuna message mbili tu... either wanaiba, au wanalipwa pesa nyingi sana zilizo nje ya mfumo wa mahesabu ambao unatakiwa kurekebishwa
 
Baada ya mawaziri wawili wa JK kuhusishwa na umiliki wa majumba/makazi ya mamilioini ya shilingi muda mfupi tu baada ya kushika nafasi zao Waziri mwingine anatajwa kumilimi jumba kubwa ambalo vyanzo vyetu vinakisia thamani yake kuwa ni zaidi ya nusu bilioni. Kutokana na vyanzo hivyo vya kuamika jumba hilo liko kwenye Elkirevi, Kitongoji cha Olorukwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya ndani kabisa eneo hilo linadaiwa kuwa lilipatikana baada ya Bw. Nyalandu kununua ardhi yenye eneo la Eka 3 hivi kutoka kwa wanavijiji watano. Jumba lenyewe limejengwa chini ya mwaka mmoja na kukamilikama mwishoni mwa 2011. Jumba limezungushwa na ukuta wa karibu futi 10 na juu yake inadaiwa limewekwa waya wa umeme (electric fence)

Ni kwenye jumba hili ambapo Bw. Nyalandu alifanyia Sherehe ya Mwaka mpya na bila ya shaka ilikuwa ni 'house warming' party. Taarifa hizi zinaendana na zile za mawaziri wengine ambao tayari habari zao za umiliki wa majumba yenye thamani kubwa kuliko vipato vyao na walizopata ndani ya muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Mawaziri wengine ni Bw. Maige na Ngeleja ambao wote thamani ya nyumba zao zinakaribia shilingi bilioni 1!

Hata hivyo hadi hivi sasa Tume ya Maadili ya Viongozi haijaonesha kujua mambo haya wala kufuatilia na kuyaweka wazi kama wanazo taarifa na kama kweli vyote hivyo vinaendana na mishahara yao.

mimi binafsi sioni kuna tatizo gani kiongozi kumiliki nyumba sometime jameni punguzeni unafiki na hili ndio linalosababisha wengi wa tz wako tayari kujenga majumba nnje ya tz kwasababu ya mambo mambo yenu ,kwani waziri sianalipwa mshahara? vipi kuhusu marupu rupu kidogo kutokana na kitengo chake???hata wewe ENIGMA nikiamua ku folow up maisha yako hakuna chenchi chenchi za pembeni unazozipata hapo kazini??
 
chenchi chenchi !? Una maana gani !?, hata ile ya radar ni chenchi pia !
 
Hivi watanzania lini tutaendelea?, mlitaka waziri asijenge?, je, mtampangishia nyumba katika maisha yake yote hata akiwa nje ya uongozi? Acheni wivu wa kike. Naomba mawaziri wote wajenge majumba ya zaidi ya shilingi Bn 3 ili wachonga midomo wachonge zaidi hadi midomo itanuke.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Wewe ni chakula haswa!!
 
Wakuu,mimi binafsi sioni kujenga nyumba ni issue kwa hawa wateule wa jk,issue hapa ni gharama kubwa wanazotumia kujenga hizo nyumba.hii hali inanipa "question mark" ni kweli haya majumba wanayojenga wanaweza ku justfy pesa wanozojengea wanazipata wapi?
Je? Ni mishahara na posho tu kweli? Kamati ya maadili ipo wapi?
 
Back
Top Bottom