Mawaziri matatani kwa kununua ndege mbovu ya rais

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
  1. Ni ndege ya rais wa Kameruni


    _59694328_105973085.jpg

    Rais Paul Biya na mkewe Chantal
    article-1063609-02CF990800000578-615_468x286.jpg

    Heri marais wa kiafrika wawe na ndege kama hizi ili kupunguza gharama na utapeli
    Mawaziri wawili nchini Kameruni wamejikuta matatani baada ya kugundulika kuwa ndege waliyonunua kwa ajili ya rais wa nchi hiyo aina ya Albatross kumbe ni ya zamani ingawa wao walisema ilikuwa mpya. Ndege hiyo yenye thamani ya dola 31,000,000 ililazimika kutua ghafla kwenye safari yake ya kwanza ya uzinduzi huku ikiwa imempakiza rais Paul Biya na mkewe Chantal. Waliotiwa nguvuni ni Marafa Hamidou Yaya ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani na Chief Ephraim Inoni a aliyekuwa waziri mkuu wa zamani. Ingawa rais Biya anasifika kwa uhovyo wake, angalaua amewakamata mafisadi wenzake tofauti na Tanzania ambapo si ajabu hata huu mdege wetu wa rais nao ni mkangafu kama ule wa Kameruni. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.
 
huu mkangafu wa cameroun una nafuu lile la jk mbona lilikuwa lipo kwenye mawe siu nyingi??
 
Usijali hata wetu tutawakata tu, ipo siku inakuja tena siyo mbali sana. Tutaanza na mzee wa utandawazi, Pesambili, AG mstaafu nk.
 
Back
Top Bottom