Mawaziri kujiuzuru

Magamba walikuwa wanaongea nini kwenye kikao chao?
Katika hali isiyo ya kawaida kutokana na upepo unaovuma ndani ya bunge kuhusu kutokuwa na imani na waziri Mkuu Pinda inawezekana serikali ya CCM haitokuwa tayari kukubali kwa mara nyingine kuvunja bunge baada ya bunge kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Waziri mkuu.

Hapa naona serikali lazima itawashinikiza mawaziri waliotajwa kusababisha au kutumia pesa za serikali hovyo kujiuzuru/kuondoka madarakani ili kuepuka aibu nyingine baada ya ile ya Richmond.
 
kwa nyakati tofauti wananchi,wanaharakati,wanasiasa au wabunge wamewataka mawaziri wafuatao kujiuzulu au kuwajibishwa.hebu tujikumbushe orodha ya mawaziri waliofanya blunders na hivyo kutakiwa kujiuzulu.

hawa ni baadhi tu......na blunders walizofanya



NGELEJA(sakata la mgao wa umeme)

NAHODHA(sakata la mauaji arusha,tarime,sumbawanga na ''sumu ya mwakyembe'')

MPONDA(skata la mgomo wa madaktari)

NKYA(sakata la mgomo wa madaktari)

MKULLO(alimpinga zitto juu ya hali ya uchumi nchini,deni la taifa limekuwa,ubadhirifu wa fedha za umma)

MKUCHIKA na MWANRI(ubadhirifu serikali za mitaa)



naomba uongeze au kupunguza orodha hii.je baraza la mawaziri litapona?
 
Hali ni tete chochote chaweza kutokea wakati wowote. Yale manamba ya mafedha yaliyotajwa Bungeni yanatisha. CCM inaweza kuamua kujitakasa kwa kuwamwaga mawaziri ama hata waziri mkuu. Hali si nzuri hata kidogo. Wananchi wamejaa hasira kila mahala na TV ziko hadi vijijini hivyo kila mtu amesikia yaliyotokea leo bungeni. Haitakuwa busara kwa serikali kuyanyamzia hayo.
 
Kujiuzulu peke yake haitoshi kwan wameshatuibia na kujilimbikizia mali na rasilimali za uma hivo wana uwezo wa kuishi hadi kufa kwao kwa mali na fedha walizojilimbikizia kwa kutuibia wananchi, hivyo licha ya kujiuzulu wafilisiwe kwanza then wachukuliwe hatua za kisheria mbweha wakubwa hawa!!
 
kwa mtazamo wangu hoja zito kutaka Pm aachie ngazi linaweza kuwa lime-originate kutoka kwa Jk mwenyewe.msingi wa mtazamo wangu ni jinsi zito alivyolieleza suala lile na jinsi alivyomtetea jk kuwa anapakaziwa tu tatizo ni mawaziri na Pm mwenyewe
 
sioni wa kushikilia wizara hata mmoja ndani ya ccm hata wanaopiga kelele nao wameoza bora na wabunge wa ccm nao wajiuzulu after 50 yrs of independence leo ndo wanaona madudu ya serikali? au ni hasira ya kunyimwa nyongeza ya posho? siku zote waliwazomea chadema leo nao (wamegeuka walokole?) shame on them

Wabunge wa Chichiem nao wamekichoka chama chao cha maganda, yani wanatamani kuhamia chama kingine ila wanaona noma!!!
 
hii nchi inaongozwa kisanii sana.lakini pamoja na hayo yote sisi kama wananchi tunaonekana kana kwamba hatuguswusi hata kidogo na huu ubaradhuli tunaozidi kufanyiwa au sijui tunasubiri hadi waje kuzifisadi nyumba zetu ndipo tuamke!!
 
Proble$ ni kwamba waziri lazima awe mbunge, na kwakuwa serikali ni ya CCM waziri lazima awe wa CCM sasa ukiangalia haraka haraka wabunge wengi pale uwezo wa kufanya kazi nzuri wizarani hawana! Mtu mwengine hajawahi kufanya kazi ya kueleweka mahala popote anapewa wizara sasa tutegemee nini hapo?
 
lakini si mpaka zipatikane saini 70 wabunge?
nina uhakika wa kupatikana kwa saini 40 s za cdm lakini zilizo bakia sijui
Du wamekutana Dodoma hotel usiku huu naona kura zitavuka 70 hawana utani J3 hapatakalika
Pinda asimuonee aibu Mkulo au Ngeleja la sivyo ataondoka yy
 
Hawa ghasia,sophia simba,omari nyundo,maghembe,wassira,mkulo,ngeleja,etc pls go home mkalime mihogo kama mimi
 
Back
Top Bottom