Mawaziri 7 wabunge 70 wa CCM kujiunga CHADEMA!

Kweli umenikumbusha kitu....yes Shibuda John Magalle..mbunge wa maswa kama sijakosea:

Alisifika sana bungeni akiwa ktk enzi za CCM...alipohama tukamsifu akatugeuka kwenye suala la posho CDM wote wamezikataa yeye akazibariki.

Ni mbunge aliyekuwa na misamiati kila alipowasilisha mada bungeni....Alimsumbua sana spika sita enzi zake kwa kauli zake tata bungeni mfano "Wabunge wote wamebakwa kwa wakati mmoja" bila kujali jinsia ndipo alipotakiwa kutoa ufafanuzi akatoa..Aliwahi kumnong'oneza spika kuwa asilimia 34 ya wabunge hupigwa na wake zao ila ni waoga kupresent hilo katika hoja binafsi.

Ndg yangu nakubaliana na wewe kuwa ni lazima pia wawe scanned kwanza.

Swali la nyongeza: Hivi mnavyomuona Mpendazoe Fred, naye alikuwa scanned kwanza?
 
Nafasi za kugombea nafasi yoyote na ngazi yoyote kupitia CHADEMA tayari zimeanza kubana kote nchini kama ambavyo tulivyowahi kulizungumzia huko nyuma. Dawa ni MATENDO MEMA kwa Umma wa Tanzania katika mienendo yako binafsi na pia KUJIUNGA NA CHADEMA mapema kabla Safina lango halijafungwa na safari ya 2015 kuanza rasmi kubila kusimama tena vituo vya kati kati isipokua tu mpaka Magogoni. Wewe hapo katafakari unachosubiri huko kwenye baridi na kwenda kinyume na matakwa ya Umma wa Tanzania ni ya kazi gani?
 
Hofu yangu hawa jamaa wasije amia na magamba . . .
Au na ukijani. . . .
Wao wakarudia mambo yao ya ndoa zao za kijanini uko
 
Kauli hii ya Mwenyekiti kuhusu mawaziri na wabunge wa Ccm, kujiunga na CDM. Ni muhimu sana na ya kupewa
kipaumbele, inatuhakikishia kama Ccm itayeyuka kama barafu muda si mrefu. Hao wahusika watajwa hapo
wasiwe na maswali ya kujiuliza na kuchukua muda, milango ya ukombozi ipo wazi kwenu, mnakaribishwa.
Kwani CDM ipo kwa kupigania haki ya wanyonge, kutokomeza umasikini na kuleta maendeleo, kikuu zaidi cha
kukamilisha hayo yote ni kuondoa ufisadi na rushwa katika mioyo na macho ya Watanzania.
Kwani ukichaguliwa kuwa na dhamana ya uongozi, tuchukulie mfano. Waziri, Katibu Mkuu na Mkurugenzi,
madhumuni ni kuongoza Wananchi na kuleta maendeleo, kwa wahusika wote watatu wasitegemee kutia mkono
na kuchukua hata senti tano, ambayo inaitwa pesa ya Serikali, bali ni kuilinda na kufanya kile kilichopangiwa.
hapo nina maana wawe na uhakika wa kuziba mianya yote ya ufisadi na rushwa katika sehemu husika.
na hapo ndio sifa ya Uwaziri, Ukatibu Mkuu na Ukurugenzi unapokuja, namalizia kwa kusema mwelekeo ni
Serikali mpya itakayoongozwa na CDM kabla ya 2015. DC wa Mbozi kesha kufungulieni milango na nyinyi amna
haja ya kuchelewa katika kuikomboa nchi.
 
Remember shibuda

shibuda is the problem because he had no intention of camming to chadema until he was chassed away by his part from contesting for Mp of maswa.

By the way he made his decision on the spot and that can not make it open as a good man or not
 
Vua GAMBA



Vaa GWANDA FLU!

Hata wanaodhaniwa ndio siku si nyingi itakuwa siyo.
Hiki kimbunga haitaacha mtu!
 
Ni bora wasubiri hadi 2015 kwa kuwa wakijivua magamba na kuvaa magwanda sasa hivi nchi haina uwezo wa kuitisha chaguzi ndogo vinginevyo serikali nzima ivunjwe na uitishwe uchaguzi mkuu mpya!
 
Katika hatua nyingine, Mbowe alisema kati ya wabunge 200 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) 70 wamekwishaomba nafasi/wamebuku nafasi Chadema. Pia alisema katika Baraza la Mawaziri aliloliteua Rais Kikwete juzi, mawaziri tisa nao wamekwishaomba nafasi Chadema. "Sasa tunawaambia wakichelewa tutafunga safina."

CCM kwa kauli hii watachanganyikiwa kabisa, maana yake Chadema imejihakikishia majimbo ya uchaguzi 80 kuwa mikononi mwake kutoka CCM uchaguzi ujao na hao wana wafuasi ambao wanakuja Chadema. Hakuna mchawi hapa zaidi ya Mkulu.
 
wanasiasa ni wajanja sana nafikiri chadema waweke deadline ni lini mwisho wa kupokea viongozi toka chama tawala wengi wameshasoma alama za nyakati kuwa ccm inachukiwa hivyo wanatafuta sehemu ya kujibanza vinginevyo chadema wakiwaruhusu tusitegemee jipya kwani wengi wao wameshiriki kupitisha miswada mibovu bungeni
 
Hii ni safi kwani ni mwelekeo wa nchi kuwa na vyama viwili vikubwa, IT IS BALANCE OF POWER. hofu yangu ni kusambaratika kwa CCM na kufa kabisa hili si jema. Kwa sasa CCM itoke madarakani lakini ibaki na nguvu ya kutoa upinzani
 
Hata Slaa alipobaizwa kwenye kura za maoni alikimbilia chadema. Taka taka na uozo wa uadilifu hatuukubali CCM.

Huyo msafi aliyebaki CCM baada ya Dr. Slaa kukimbilia CHADEMA yupo wapi leo?
Kwa CCM, watanzania maskini wanaotafuta haki kwa jasho lao ni Taka Taka, Watanzania walioamua kuyatoa maisha yao kuwatetea wanyonge nao ni Taka Taka.

Mafisadi na Wezi wa mali ya umma ndio wanaoonekana ni watu wasafi ndani ya CCM!
 
Nilishapata kuandika kuwa ni muhimu kwa CDM kuwa makini na watu hawa wanaohama. Ni vyema kuwa na strong scanning, tena iwe bayana kuwa hawaji ili wapate vyeo. Kwa kuwa wao waliokuwa tayari kushindia mrenda na kula kauzu ili kukijenga chama wataweza bado kufanya kazi nzito ya kukiimarisha, wao waliokuwa wakiangalia kwa pembeni wakija kudakia lazima watazamwe kwa jicho makini. Mbowe anasema wamejipanga kwa wanaohamia, how far wamejipanga, ni hatari mno kupokea watu ambao wana fanya timing ya kufanikisha maisha badala ya kupambana kwa haki za wengi. It should be now or NEVER.
 
CDM inatakiwa kuwa makini kuhusu hawa wanaotaka kuhamia. Swali ni kwamba siku zote walikuwa wapi? Si walichagua sera? kwa nini wasipiganie sera wanazoziamini wakiwa huko huko? Pengine hawa ndio wale waliokuwa wanagombea ubunge ili wapate uwaziri, kwa vile matumaini hayapo tena wanaamua kujaribu bahati zao wakiwa CDM. Hasa wakiona kwamba chama chao kimeanza kupungua mvuto wanaona wana nafasi ndogo kurudi bungeni kwa kupitia chama cha awali. Pili hiki ni kipindi cha CDM kujijenga na kutafuta vijana wapya walio na mawazo mapya ya uongozi hivyo hakuna haja ya kung'ang'ania watu ambao wameshindwa katika wakati wao. Naongelea na vyama vingine sio CCM tu. CDM virusi hivyo, kuweni makini.
 
Mwenyekiti wa chadema freeman Mbowe amasema amepokea maombi ya mawaziri7 na wabunge70 wa ccm kujiunga chadema.

Chanzo: Tanzania daima



Mwananchi:
by Candiscope,
Katika hatua nyingine, Mbowe alisema kati ya wabunge 200 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) 70 wamekwishaomba nafasi/wamebuku nafasi Chadema. Pia alisema katika Baraza la Mawaziri aliloliteua Rais Kikwete juzi, mawaziri tisa nao wamekwishaomba nafasi Chadema. "Sasa tunawaambia wakichelewa tutafunga safina."
 
Yesu alisema "Mwenye afya hamiutaji daktari". waache waje wapate tiba ya gambanyurosis, wakaeneze habari njema ya ukombozi wa mtanzania.:spy:
 
Back
Top Bottom