Mawaziri 6 sasa mikononi mwa TAKUKURU!

Takokuru ni tatizo huyo CEO wa taasisi hiyo amekuwa mwanasiasa badala ya kuwa mtendaji. Miaka ya nyuma ilikuwa ni utendaji tu sio bla bla kwenye vyombo vya habari. JK anatakiwa aifumue hiyo taasisi walete CEO mwingine anayejua maana ya investigation na afanyiwe interview na bunge kama wale jamaa waliokuwa wanataka ubunge wa Afrika mashariki.
 
William,

Kwa vile mawaziri/manaibu waliokuwa na tuhuma wazi wazi ni ktk wizara 8, tunafahamu nusu ya hao mawaziri wamerudi na nusu wametolewa.

a) Je una maanisha hata wateule wa Rais wako mpendwa wapelekwe mahamani?

b) Unafikiri hilo litawezekana (muda huu) wangalipo kwenye madaraka?

c) Iwapo kesi hizo zitagusa maslahi ya chama chenu kitukufu, kweli unadhani haki itatendeka upande wa Taifa/wananchi?

d) Huoni pamoja na kutoa hoja hizo kuwa umeegemea zaidi upande wa chama, na sio wa Taifa?
 
Wakuu JF heshima mbele sana,

- Well, kitendo cha Rais kuwabadili mawaziri waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na upotevu wa hela za wananchi na ripoti ya CAG, kina maana moja tu kwamba hata na yeye ameridhika kwamba kuna ukweli au FACTS katika tuhuma walizokuwa wakituhumiwa nazo, ninasema great second day kwa Taifa, kwanza ilikuwa kuweka ripoti wazi to the public na kuruhusu mjadala wa public!

- Sasa ifike mahali pa kufanya kweli, yaani Watuhumiwa wote kufikishwa kwenye mkondo wa Sheria, haki itakua imetendeka na sio otherwise, kwanza haki kwao mawaziri maana wanahitaji kuwa wasafi mbele ya public na pili Serikali kulinda heshima yake kwamba sasa ipo serious, ama sivyo kuitoa ripoti ya CAG to the public itakuwa ni kazi ya bure, I mean mawaziri na viongozi wetu wakijua kwamba madhara ya kuiba ni kujiuzulu tu na kuachiwa ukale mihela ya wananchi tutakua tunajenga taifa la kusadikika, na itakuwa kazi kubwa kumpitisha Rais wa CCM 2015!

- MHESHIMIWA RAIS, UBARIKIWE KWA KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI, SASA TWENDE MBELE ZAIDI TUFIKE KWENYE SHERIA NA WOTE WENGINE HAO MAKATIBU NA WAKURUGENZI ULIOSEMA KWENYE HOTUBA YAKO KUWA WANAHUSIKA NA WAO PIA UWE MWENDO WA KUELEKEA KWENYE SHERIA!, NI SHERIA TU NDIO INAWEZA KUTUSAFISHA WOTE, SERIKALI NA MAWAZIRI WALIOACHWA!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!



William @DSM CITY!

Mkuu William,

Tatizo kubwa lililopo ni mfumo mzima wa utawala kuwa mbovu. Watu hawaajibiki na hakuna maadili ya kuwajibika. Mawaziri hawa walipaswa kujiachia ngazi siku nyingi sana. Serikali haisikilizi kilio cha wananchi kwa mfano wizi wa EPA watuhumiwa wanazidi kutembea huru tu. Wananchi tuliambiwa serikali itawachukulia hatua hakuna kilichotokea isipokuwa gelesha ya akina Yona, Mramba tu.
 
Ona Wile, you have no room down there, Fulsa ipo wazi if you fighty nje ya system, wengi wamejaribu na kushindwa, ni sawa kabisa na pia hata mimi naheshima wazo lako na kwa utawala wa sheria ingeliweza kupitia katika stage hiyo,Ok fine fanya utachoamini and wish you all the best, lakini uko ndani ya gari bovu and no voices for the Youth.
Tacktics wapo wengi wanafanya hivyo within the system bado wanafeli, i can see you unavyotamani sheria ifuate mkondo but at the end of the day unbased judgement, Vijana taifa la kesho ndani ya ccm, Alama pia za nyakati ni vema ukazingatia, ona ukombozi wa bili taifa letu unavyokuja kwa kasi, your dream will success if you change a move, Hawatakupa Chance, Dady was trying lakin proved fature, all in all kila la kheri:baby:
 
Hao TaKAKURA ni wastage of national resource,haiingii akilini kwa taasisi kama hiyo yenye dhamana ya kulinda rasilimali za nchi isubiri taarifa za AG ndio wafanye kazi.Kwani kazi za Takukuru ni zipi,wanatia aibu sana,kazi yao ni kuvizia mahakimu wa primary courts,wafanyakazi wa weigh bridges na traffic ambao hawana effect kwenye uchumi wa nchi.Hao mawaziri ,makatibu wakuu etc waliwaona siku nyingi lakini sio siri kuwa hakuna watu wanaongoza kwa rushwa kama TAKAKURA,unadhani hawawaoni TRA staff wanavyojineemesha,hata kama mishahara ni mizuri iweje watu wa TRA wengi wana utajiri wa kutisha na TAKUKURU wapo,au wasubiri AG awaonyeshe,wafanyakazi wa halmashauri nyingi nchini hasa DTS na wahasibu na hiyo mpaka AG awaonyeshe?President amuwajibishe Dr Hosea.Pia iundwe tume nje ya PCCB ichunguze utajiri wa watumishi wa PCCB all over the country wameupataje?otherwise tunacheza mchezo wa kitoto hapa.
 
Iundwe independent elimination squad.

Inachunguza, inahukumu, ina eliminate kila afanyae madudu awe ni waziri au tarishi. Siku anayokuwa eliminated, anawekewa na hukumu yake na ushahidi kamili wa madudu aliyofanya.

Wakifika watano tu! ukimpa mtu hata soda atakataa! wacha "takrima" na "ten percent".

Siku hiyo ikifika...na yoyote atakayeifanya siku hiyo iwe kweli ipo atakuwa hero wa watanzania. Mbona inawezekana tunachosubiri ni nini?
 


- kwanza ilikuwa kuweka ripoti wazi to the public na kuruhusu mjadala wa public!



- MHESHIMIWA RAIS, UBARIKIWE KWA KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI,

William ni nani kakwambia ripoti ya CAG huwa inakua siri kwa public, Haijawahi kuwa siri nashangaa kwanini kusifia kitu ambacho kipo wazi miaka yote.

Rais hasikilizi mawazo ya wanachi kwa kupenda, nguvu ya umma inamlazimisha kutenda na hata kufikiri.....
 
Takukuru gani? Hawa hawa wa Dr. Hosea? Ngoja ninywe chai yangu taratibu. Hao hawana jipya...wanatupozea muda na kula hela zetu walipa kodi. Hakuna lolote wanalolifanya. Kama lipo watuonyeshe maana hakuna tuliloliona
 
Iundwe independent elimination squad.

Inachunguza, inahukumu, ina eliminate kila afanyae madudu awe ni waziri au tarishi. Siku anayokuwa eliminated, anawekewa na hukumu yake na ushahidi kamili wa madudu aliyofanya.

Wakifika watano tu! ukimpa mtu hata soda atakataa! wacha "takrima" na "ten percent".
Sheria za China hizo hawangalii nyani usoni, rushwa, ufisadi, wizi wewe unakwenda tuu,hakuna mjadala!!! Kiuchumi wako juu kweli kweli!!!!

 
William,
Tafadhali utafafanulie njia inayotumika (maana ipo) ya namna ya Taifa linawarudishia hao viongozi utumishi wao.
You've just dropped a very useful hint.

- Jamani no matter how much rotten the system is, bado haitukatazi wananchi kutoa maoni yetu, nimetoa haya maoni nikijali utawala unaoheshimu sheria, Waheshimiwa Ngeleja na Maige ni my very good close friends ninasikitika sana kuwaona wakituhumiwa on this stuff and I hope they are clean ndio maana ninasema kwamba ningependa kuona Sheria inawasafisha ili waweze kuwa in the position ya kushika nafasi kubwa huko mbele ya safari, sasa dawa ni kwa hawa washikaji zangu sana ni kusafishwa na Sheria tu!

- Ninajua kwamba wote wawili wanapita hapa kila siku, hope wamenisikia ni pamoja na wao kudai kwenda kwenye haki ili wasafishwe na sheria, ni sheria tu ndio inaweza kuwasafisha!

William.
 
Ingekuwa ni enzi za kina JKN na EMS watu hawa wangepatikana na hatia ya kuhujumu uchumi, lakini kwa tanzania hii ya sasa inayoongozwa na nguvu ya mafisadi watashinda kwa kuonekana kuwa hawana hatia.

- Kwa mfano ni Viongozi wapi wa level ya uwaziri unaowakumbuka waliowahi kwenda Jela hizo enzi, please naomba majina ili tuongee na FACTS!

William.
 
Malecela,
Nakushauri uandike kitabu ukiite ::UWAJIBIKAJI NA MAENDELEO YA TAIFA;; Elezea uwajibikaji wa hiari bila shurti na dhana ya kuridhisha wanachi kwa kuwajibisha wasiotaka kuwajibika. Halafu kitabu kirushe humu ili tupate matazamo wako juu ya kule tuendako na huu mfumo wa kiini macho wa sasa.
 
Malecela,
Nakushauri uandike kitabu ukiite ::UWAJIBIKAJI NA MAENDELEO YA TAIFA;; Elezea uwajibikaji wa hiari bila shurti na dhana ya kuridhisha wanachi kwa kuwajibisha wasiotaka kuwajibika. Halafu kitabu kirushe humu ili tupate matazamo wako juu ya kule tuendako na huu mfumo wa kiini macho wa sasa.

- Tanzania tuna tatizo moja kubwa sana, nalo ni wananchi wenye maneno mengi sana bila FACTS wala EVIDENCE, for some reasons tumekuwa waridhikaji sana wa mambo madogo madogo, we don't care about details even small ones, no courage, siku zote tunasubiri wengine watufanyie!

- I mean nimekusikia sana mkuu, one thing ni kwamba nina nia kubwa sana mbele ya safari kuandika kitabu on my experience na EAC run, na mengine mengi sana ninayoyajua kuhusu siasa ya bongo na utawala wa Sheria, wananchi tunaonekana tume kata tamaa sana hivyo kuwapa watawala nafasi ya kutuchezea, we need to stand up tena kwa pamoja bila kujali vyama vyetu hasa tunapodai utawala wa Sheria!

William.
 
hakuna jipya hapo naona ni usanii tu tangu lini serikali ikashinda? naona nikutundanganya tu ili tuwape kura tena 2015 naomba tuwe macho haswa kijijini maana huko wanaamini ccm inafanya kazi kumbe usanii
 
Mkuu Malecela,,c ulisema report ya CAG haina meno huoni facts, haiwezi sababisha mtu aende mahakamani? leo unaiamini na kuitegemea tena?
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom