Mawasiliano.....!

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,778
59,138
Natumaini wote mmekua na jumapili njema!

Nwy kwa ndugu/jamaa/marafiki na mwenzi wako nini unachukia sana linapokuja swala la mawasiliano (simu au hata email) ?!

Binafsi sipendi
1) unapompigia mtu alafu asipokee kwa sababu yoyote ile alafu hata baadae ashindwe kukupigia au hata kukutext for no reason at all (hamna matatizo ya charge wala credit) mpaka umtafute tena mwenyewe.
2)Unapompigia mtu anakwambia yuko bize atakutafuta akimaliza mambo yake alafu hafanyi hivyo.
3)Mtu anaejibu text/email ndefu ya maana kwa neno moja...Owkey..Poa..Sure and the likes !Mara moja moja mi hua nadondoka hapa!
4)Mtu asiyepokea simu hata kutwa bila kukupa sababu ya kuacha kupiga...pokea sema huwezi/hutaki kuongea.Hapa kama sio kawaida mtu anaweza patwa na wasiwasi!
5)Mtu anaekasirika ukimwambia kuna simu nyingine unahitaji kupokea/piga mara moja!6)Mtu anaebeep bila sababu ya msingi.
7)Mtu anaeforwad email/text ndeeefu zisizo na maana.
8)Mtu anaeomba kutumia simu yako alafu anaanza kuangalia salio au kuchungulia msg zako(huyu sio mpenzi)...rafiki tu au ndugu.
9)Mtu aaetoa namba yangu ya simu kwa mtu anaeiulizia bila kuniuliza mimi kwanza.
10)Mtu asiejua kujibu msg za watu wengine ila yake ukiipotezea tabu.

Chache zinazonihusu naanza kujirekebisha!!
So wewe zipi sinakuhusu na zipi hupendi..........?!
 
kuna baazi ya nchi kuna simu za bure, kuna huu uzembe mtu anakupigia simu wala hana la kuongea utakuta masaa mawili mzembe anabwabwaja tu, inauzi ajabu. Yaani DNA za kiswahili wakipata bure wee acha tu.
 
Zote mi hazinihusu na nilishajicondition kuwa individual katika suala la mawasiliano maana madhara yake huwa makubwa ni heri uunguze mboga jikoni. Unaweza kuiosha upya ukatia viungo ikavutia na kulika vizuri. Lizzy nyc rest!
 
Zote hizo zinanikera ila binafsi napenda mtu anitumie msg kuliko anipigie. Sipendi kuongea ongea na simu.
 
kuna baazi ya nchi kuna simu za bure, kuna huu uzembe mtu anakupigia simu wala hana la kuongea utakuta masaa mawili mzembe anabwabwaja tu, inauzi ajabu. Yaani DNA za kiswahili wakipata bure wee acha tu.

isitoshe klorokwini haya mambo ya promotion ni huku kwetu tu matokeo yake watu wanaacha kuwajibika makofisini na kubaki wakichati Na CHEKA TYM kama unamgonjwa hospitali anaweza kufia reception lo!
 
Inategemea, kuna wengine unamuambia sitaki mawasiliano hakuelewi, anapiga tu. Kuna wengine siyo kujibu msg tu, hata kusoma huwa hawasomi.
Cha muhimu ni kuangalia unataka kuwasiliana na nani? Huyo huwa anapendelea mawasiliano ya namna gani?
Na siyo lazima kila mtu awe vile unapenda,
ndo maana tumeumbwa binadamu,
pamoja na mabilioni tuliopo duniani hatufanani exactly, lazima kuna tofauti tu!
 
1.inabidi uwe mvumilivu na msamehevu linapotokea swala la mawasiliano,vinginevyo utagombana na kila mtu.
2.hakuna alie na akili timamu akaachakupokea simu wakakati anapigiwa,lazima ipo sababu.
 
Zote hizo zinanikera ila binafsi napenda mtu anitumie msg kuliko anipigie. Sipendi kuongea ongea na simu.

Kweli husninyo most of txt sms huwa rahs kuinterpret kuliko maongezi mtu anataka kukwambia tuonane muda fulani anaanza na salamu zenye porojo mingi anaulizia hadi vile viatu ulivyovaa Katka graduation ya advance.
Lo!
 
isitoshe klorokwini haya mambo ya promotion ni huku kwetu tu matokeo yake watu wanaacha kuwajibika makofisini na kubaki wakichati Na CHEKA TYM kama unamgonjwa hospitali anaweza kufia reception lo!
Yaani mkuu wewe bana mswahili akiona cha bure hata kama hana umuhimu nacho atatumia tu, kuna mshkaji wangu si mnywaji lakini kuna siku alikuta pombe za bure nilishangaa mjomba aliondoka na nyagi kuliko aspirin wa JF.
 
Zote hizo zinanikera ila binafsi napenda mtu anitumie msg kuliko anipigie. Sipendi kuongea ongea na simu.
<br />
<br />
Hus mie sipendi sms kabisa nazichukia halafu huwa sijibu ukituma sms nakutwangia simu tumalizane
 
Kweli husninyo most of txt sms huwa rahs kuinterpret kuliko maongezi mtu anataka kukwambia tuonane muda fulani anaanza na salamu zenye porojo mingi anaulizia hadi vile viatu ulivyovaa Katka graduation ya advance.
Lo!

kabisaaa! Mara nyingine unaweza ukawa kwenye mazingira ambayo huwezi kupokea simu, kama mtu anakupigia halafu network nayo inasumbua huwa ni balaa.
 
Sipendi kupigiwa simu binafsi ndani ya muda wa kazi, pia sipendi kutumiwa meseji zisizo na msingi (forwarded messages)

Copy and pest sms then husaidia sana kukamata wasaliti. Mfano jamaa yangu alitunga sms akamtumia girlfriend wake nae akaedit kidogo tu akanitumia jamaa hakuwah kunambia kama wanamahusiano alipochukua simu yangu acopy sms yoyote itakayomfurahisha akaikuta aliniuliza nikamwambia ukweli akanambia yule binti ni shem wangu ila aliniudhi alipoenda kumpiga eti anajipendekeza kwangu inamaana hajaridhika nae.
 
<br />
<br />
Hus mie sipendi sms kabisa nazichukia halafu huwa sijibu ukituma sms nakutwangia simu tumalizane

duh! Kweli tunatofautiana. Mi ukinipigia naweza nikaiangalia simu yako hadi inakatika sipokei. Lol
 
kabisaaa! Mara nyingine unaweza ukawa kwenye mazingira ambayo huwezi kupokea simu, kama mtu anakupigia halafu network nayo inasumbua huwa ni balaa.
Mazingira gani? toa mifano. Hapa unaongea na magreti thinka bana sio unakata kata majibu tu
 
Back
Top Bottom