Mawakili wajitokeza kutetea wavuvi haramu wa kigeni

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
Nora Damian na Tausi Ally

MAWAKILI wawili wa kujitegemea, Erasmus Buberwa na Elias Nawela wamejitokeza kuwatetea watu 32 kutoka mataifa matano, ambao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya uvuvi haramu kwenye pwani ya Tanzania.

Kati ya mawakili hao, Buberwa anawatetea washtakiwa wawili wakati Nawela anawatetea washtakiwa 30. Washtakiwa wote bado wapo rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili kwa kila mshtakiwa.

Wakili wa serikali, Prospa Mwangamila alisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba mahakama iwaruhusu kumchukua mshtakiwa wa kwanza ambaye ni nahodha wa meli hiyo, Hsu Tai, 61, kwa ajili ya kufanya naye mahojiano katika kituo kikuu cha polisi na mahakama ilikubali ombi hilo.

Hakimu mkazi mkuu mfawidhi wa Kisutu, Addy Lyamuya aliamuru wakalimani wote wafike mahakamani Machi 27 wakati kesi hiyo itakapotajwa.

Maharamia hao kutoka nchi za China, Phillipines, Indonesi, Vietnam na Kenya walikamatwa wakiwa wanafanya shughuli za uvuvi kwenye pwani ya Tanzania kwenye Bahari ya Hindi kinyume cha sheria. Watu hao walikuwa wakitumia meli ya uvuvi ya Tawariq 1 wakati walipokamatwa Machi 8.

Kwa mara ya kwanza, maharamia hao walifikishwa mahakamani Machi 12, lakini hawakuweza kusomewa mashtaka kwa kile kilichodaiwa na upande wa mashtaka kuwa walikuwa hawajapata wakalimani kwa ajili ya washtakiwa wote.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Machi 8, mwaka huu walikutwa wakifanya shughuli za uvuvi katika ukanda maalumu wa kiuchumi wa Tanzania bila kuwa na leseni ya kufanya shughuli hizo.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 18(1), Sura ya 388 kikisomwa pamoja na kanuni ya 67 na 65 ya Mamlaka ya Uvuvi Baharini ya 2009, ambacho kinapinga uvuvi haramu.

Wanadaiwa kuwa tarehe hiyo wakiwa katika ukanda huo maalumu walipanga njama za kuficha taarifa za mwenendo wa chombo chao cha uvuvi kwa kufuta chati ya njia ya uvuvi .

Washtakiwa wote walikana mashtaka, huku mshtakiwa wa saba, Zhao Hunquing akiileza mahakama kuwa yeye hahusiki kabisa na makosa hayo kwa kuwa yeye ni wakala tu wa meli hiyo na kwamba alikuja tu baada ya kupata taarifa kuwa meli hiyo imekamatwa.
 
Kwa mujibu wa sheria zetu, legal representation ni haki ya kila mtu kama ilivyo Dhamana ni haki ya msingi ya mshtakiwa. Hata kama wangekuwa hawana uwezo wa kuweka mawakili, Jamuhuri ingewajibika kuwawekea mawakili.
Kesi hiyo ni ngumu kwa sababu inahusisha sheria za kitaifa na na kimataifa za meritime.
Hata wale samaki, tumewaharakisha bure, hakuna ushahidi wamevuliwa eneo gani, wapi na lini.
Watanzania tusihamanike na maharamia hawa kwa sababu samaki ni wa wote, na sisi hatuwezi kuwavua kwa sababu hatuna vifaa vya kihivyo. Tunachotakiwa kufanya ni kushirikiana na meli za kiharamia kwa kuwapatia vibali halali na kutafuta jinsi ya kuthibiti viwango ili tusiendelee kudhulumiwa.
Tunadhulumiwa kwenye Tanzanite, tunadhulumiwa kwenye Almasi, tunadhulumiwa kwenye dhahabu, shaba na chuma, sasa tunadhulumiwa hata kwenye samaki!.
 
Samaki bila shaka ni wakwetu hata kama walivuliwa katika maji ya bahari nyingine mbali na ya kwetu maana wamekamatwa kwenye bahari yetu, sijui wanaweza kushawishi nini ili tukubali samaki hao wamekuja nao kutoka maeneo mengine. Kama kuna kitu kimeniuma ni hao samaki. kweli hatuna vifaa vya kuvulia wala vya kulinda mipaka ya bahari yetu lakini washenzi wasitumie mwanya huo kutuhujumu ukizingatia wazawa wanakula vidagaa wakati samaki wenye akili wanakwenda nje ya nchi. Muhimu sheria ziangaliwe zinasema nini hasa unapowakamata wakiwa na shehena kubwa kama hiyo ya samaki, je warudishiwe au samaki wataifishwe? wanasheria tuambieni.
 
Back
Top Bottom