Mawakili ni watetezi wa wanyonge au ni waporaji wa wanyonge?

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Gone are the days when the legal profession stood out as "the noble profession".Ilikuwa ni fahari sana kwa mtu kuwa mwanasheria hasa wakili wa kujitegemea maana ilikuwa inaaminika kuwa hawa ndiyo watu pekee waliosoma/kuelimika ( learned fellows!) nadhani kutokana na jinsi taaluma hiyo ilivyokuwa conservative ikishikilia miiko ya kitaaluma na kuwa na mifumo ya kuwaadhibu wale walioenda kinyume na maadili kupitia siyo tu chama cha mawakili bali hata jaji mkuu aliwachukulia hatua wale walioonekana na utovu wa nidhamu na kuwa strike out of the advocates roll.

Tuangalie historia kidogo ili tuweze kuelewa tatizo linakotokea:
Miaka ya nyuma ilikuwa kazi kwelikweli hadi kuingia katika uwakili wa kujitegemea na wakati wa Nyerere ilikuwa ndiyo kabisaaa mawakili wa kujitegemea wenye kufanya kazi kibinafsi ni kama " haikuruhusiwa!" it was kind of restricted.Mawakili wengi wakujitegemea walikuwa wale wa enzi za ukoloni na wengi walikuwa wahindi na wachache wazungu. Kulikuwa na shirika la sheria Tanzania Legal Corporation ambalo kama shirika la umma liliajiri mawakili kusimamia kesi za mashirika na kwa kiasi kidogo kusimamia mashauri ya watu binafsi.Nidhamu ilikuwa juu!

Polepole mawakili binafsi wazalendo wakaanza kusajiliwa lakini ilibidi kufanya usahili maalum ( bar exam) na mchujo ulifanyika ikiwa ni pamoja na kutaka maoni kuhusiana na credibility/conduct ya muombaji na kama alionekana hana maadili ilikuwa kigezo tosha kumnyima uwakili.

Miaka kama mitano sasa, usajili wa mawakili umekuwa kama umerahisishwa zaidi na idadi kubwa sana ya mawakili wamesajiliwa ikiwemo hata watu wasiokuwa na maadili.Wengi wao wamekuwa watu wakujali sana kujilimbikizia mali zaidi ya kutoa huduma.Hizi mbio za kusaka utajiri harakahara kumekuwa kunawaumiza watu kwa namna mbalimbali ambazo labda wachangiaji wanaweza kuchangia. Ndiyo tunaona na kusikia mawakili wakiwaibia na kuwadhulumu wateja wao kama ilivyotokea hapa karibuni ambapo wakili ametiwa mbaroni kwa kumuibia mteja kiasi kikubwa cha pesa ( about 400 million) na mpaka sasa yuko rumande.Zamani mawakili walikuwa wakijiheshimu na kuchunga mienendo yao hata in public. Not anymore! Ndiyo tunaona mawakili kama Magai wakipigana hadharani!
Maswali ya kujiuliza ni:
1. Je code of conduct ya mawakili imetupiliwa mbali na hivyo kuwafanya kuwa huru ku behave kama wahuni?
2. Je tatizo ni mchakato wa kuwasajili au ni mfumo wa kuwamulika mienendo yao?
3. TLS na Council of Legal education hawaoni iko haja kujizatiti na kuionyesha jamii kuwa nidhamu ni sifa moja wapo ya kuwa wakili na si kule kujua sheria tu?
4. Can we compromise on discipline hadi fani hii idharaulike na kuonekana ya wahuni?
5.Jamii inaweza vipi kuwawajibisha hawa watu?
Naomba kutoa hoja ili ijadiliwa kwa undani zaidi
 
Uwakili wa leo ni kula na mafisadi tu, kuwa mwangalifu na yeyote anayejiita wakili kwani unamlipa fedha halafu mdaiwa wako naye anamlipa! hapo utakuwa umeliwa, sasa cha ajabu zaidi na kushangaza wakili anayefanya hivyo unakuta Rais anamchagua kuwa Jaji
 
Una-evidence yoyote ile juu ya swala hili?????
 
Kite,
Hayo ni mawazo yako na una haki nayo....,
Ila suala la msingi - unadhani wananchi wenyewe wanaelewa wajibu wao katika na wao wenyewe kuhakikisha haki inatendeka hata kama wamelipa wakili? Unajua kwa siku hizi bongo kwa mfano wagonjwa huwaelekeza madaktari ni jinsi gani watibiwe! Ukisema unamwachia moja kwa moja utajikuta hupati tiba stahili.Ni makubwa maana professions nyingi siku hizi zimeingiliwa.
Ukiweka wakili halafu ukalala usingizi utakuta haki zako zilishauzwa na wakili huyohuyo na sijui utamlaumu nani! Angalizo: Nikisema hivi simaanishi mawakili wote wanauza haki.Wako ambao bado ni waadilifu.
 
Kubwa saaaaaana! na usinikumbushe machungu yangu!

Uwakili wa leo ni kula na mafisadi tu, kuwa mwangalifu na yeyote anayejiita wakili kwani unamlipa fedha halafu mdaiwa wako naye anamlipa! hapo utakuwa umeliwa, sasa cha ajabu zaidi na kushangaza wakili anayefanya hivyo unakuta Rais anamchagua kuwa Jaji

Tatizo huo ushahidi mnaukalia, unadhani kama ungeuweka wazi huyo JAMAA angechaguliwa kuwa JAJI basi?

Anyway UWAKILI ni professional kama ziloivyo nyingine, hata tax consultants huwa ni kuhakikisha mteja wao analipa kiasi kidogo iwezekanavyo kwa kuangalia loop hole.

Pamoja na hayo yooote mnyonge anahitaji huduma ya wakili na wakili anahitaji hela za mnyonge aweze kuishi, haijalishi ni upande gani kila binadamu ana haki ya kupata msaada wa sheria ndio maana hata wale jamaa wezi wa samaki wamepata mawakili toka nchi waliyokuwa wanajaribu kuiibia. nk nk nk.......

kwa muda huu ni hayo tuu
 
Well as long as anashinda kesi yangu sidhani kama nitajali hayo mambo mengine.
 
Well as long as anashinda kesi yangu sidhani kama nitajali hayo mambo mengine.
Good attitude..
but umewahi kufikiria ..je pale umeshinda kesi kwa mfano ya madai..na milioni zako kadhaa zikaingia kwenye account ya wakili wako..halafu asikupatie ...utafanyaje?
 
Kite umeshindwa kujificha kuwa ni wakili na kama sio,basi baba yako alikuwa wakili-ahaaah!
WomenofSubstanc kasema Ukweli mtupu. na ni vyema mkajua siku hizi TZ ukipata case kama ya zaidi ya 500M,ma advocate wanapishana mlangoni kuja kuomba kukutea na sio wewe kuwafuata?Na wanafanya upepelezi kwanza kujua kama umeiba kweli na bado unazo au umesingiziwa,wakiona hizo pesa huna basi wanajua you are not hotcake.Kite ninayo evidence-what next?Hivi mtu anashikwa na kiungo cha Albino anakwenda mahakamani kushinda case -hii inataka mtu kusomea sheria?Mafisadi kina Yona,Mramba etc baba zao hakuwahi hata kufanya biashara ya karanga leo hii wana pesa ambayo hata kama tangu waanze kazi jumlisha posho zao,mishahara yao yote,bila kutumia hata senti 5,hazifiki na wanazitangaza hadharani? Mimi siku nchi hii ikiwa ya sheria mkononi sitoshangaa!Maana vitabu vya sheria havifanyi kazi!
 
Cha msingi tunachopaswa kujua ni kuwa, ukiwa na shauri, ukaweka wakili usibweteke na kufikiri kuwa umefika!
Jisumbue kidogo kufuatilia mwenendo mzima wa shauri lako.Msumbue wakili wako kwa maswali na umfanye ajue kuwa umemuajiri na ndiyo sababu umemlipa.Weka kumbukumbu pia za kila tukio, ikiwa ni pamoja na kiasi cha malipo uliyotoa maana hii itakusaidie mbele ya safari.Kama ni msomi, basi jitahidi kutafuta habari au taarifa zinazohusiana na shauri lako na sasa kuna internet, ingia browse upate info.KISHA pata muda ujadili na wakili wako.Ukiona ana mwenendo unaotia mashaka, hoji mara moja na usiogope kabisa.
Ikitokea una ushahidi kabisa wa mal practice au wakili kuuza haki yako ( compromise your interests) basi kamshtaki kwenye kamati ya nidhamu ya mawakili.
N.B. Kabla ya kuajiri wakili, pata kwanza rekodi ya utendaji wake - je ni mtu rahisi kurubuniwa? je ni mtu anayependa kutumia mbinu chafu ili ashinde kesi? je ni mtu mwadilifu? vyote hivi vitakufanye uamue na kufuatilia kwa ukaribu shauri lako.
MWISHO WA SIKU ELEWA KUWA KIENDACHO KWA MGANGA HAKIRUDI!
 
Good attitude..
but umewahi kufikiria ..je pale umeshinda kesi kwa mfano ya madai..na milioni zako kadhaa zikaingia kwenye account ya wakili wako..halafu asikupatie ...utafanyaje?

Huo mtihani kweli, hopefully nitakua na account yangu mwenyewe. Otherwiser violence itabidi itumike.
 
Mimi nafikiri kuna haja ya serkali kuanzisha sheria na kanuni mpya kuhusiana na masuala ya 'malpractice' ya hawa mawakili. Mfano mzuri ni hapa Marekani wakili inabidi akate insurance kujilinda kabisa kama akichemka anaweza kushtakiwa na kutakiwa kulipa mapesa mengi sana. Hili suala kwa sasa hipo haja kuwepo Tanzania ili kulinda haki za hasa wanyonge.

Shadow.
 
Huo mtihani kweli, hopefully nitakua na account yangu mwenyewe. Otherwiser violence itabidi itumike.

Ndgu yangu....
haiendagi hivyo.Hayo mahesabu siyo kama kuweka fedha yako benki!
Ukitumia violence ujue the fraternity will deal with you si unajua tena?
 
Mimi nafikiri kuna haja ya serkali kuanzisha sheria na kanuni mpya kuhusiana na masuala ya 'malpractice' ya hawa mawakili. Mfano mzuri ni hapa Marekani wakili inabidi akate insurance kujilinda kabisa kama akichemka anaweza kushtakiwa na kutakiwa kulipa mapesa mengi sana. Hili suala kwa sasa hipo haja kuwepo Tanzania ili kulinda haki za hasa wanyonge.

Shadow.
Shadow,
Thats the whole point why I brought up this issue.Kuna vitu vingi watu hawavijui na kwa sababu hiyo unakuta wanyonge na hata wenye zao wasio makini huishia kupata hasara hata pale ambapo wana haki kabia kisheria.
 
Jamani mimi kama muelewa wa fani hii ya sheria naomba niseme haya yafuatayo labda nitasaidia kutoa mwanga kuhusu hii fani. Nitatumia quotes za women of substance.

Gone are the days when the legal profession stood out as "the noble profession".Ilikuwa ni fahari sana kwa mtu kuwa mwanasheria hasa wakili wa kujitegemea maana ilikuwa inaaminika kuwa hawa ndiyo watu pekee waliosoma/kuelimika ( learned fellows!) nadhani kutokana na jinsi taaluma hiyo ilivyokuwa conservative ikishikilia miiko ya kitaaluma na kuwa na mifumo ya kuwaadhibu wale walioenda kinyume na maadili kupitia siyo tu chama cha mawakili bali hata jaji mkuu aliwachukulia hatua wale walioonekana na utovu wa nidhamu na kuwa strike out of the advocates roll.

Katika hili hali bado ni ileile. Uwakili no noble profession na ndio maana ndio hotcake proffesion in Tanzania. Kila mwanafunzi Tanzania anataka kusomea sheria. Kila chuo kikuu kinatoa mafunzo ya sheria. Some are basically half cooked. (wengine wanathubutu kuiba mitihani ili wawe wanasheria). Kwa hiyo hawa wanakuwa rotten toka huko walikotoka. Sasa sijui unatumia kigezo gani kuilaumu fani ya sheria wakati ni systematic failure ya huko walikotoka.

Lakini nikufahamishe kuwa mawakili wanaoenda kinyume na maadili wanaadhibiwa pale inapokuwa proved kuwa wametenda kosa. na hili huwa linafanywa kwa uwazi kabisa. (Kwa ufahamu zaidi ningekushauri uende pale Tanganyika Law Society wakupe ripoti zao za mwaka uone ni mashauri mangapi wanayafanyia kazi). Pia ningekushauri uende pale kwa mawanasheria Mkuu uombe kuonana na Mama Munisi akupe list ya mawakili wanaofukuzwa au kusimamishwa uwakili kwa kukiuka maadili. mifano michache ninayoweza kukupa kwa sasa ni kuhusu wakili Lamwai aliyefungiwa mwaka mzima na kuna wakili mmoja anaitwa Rutagatina (kama sikosei) amefutwa kabisa kwenye orodha ya mawakili kwa kula shilingi 200,000 tu ya mteja akisingizia anampelekea jaji.

Tatizo lililopo ambalo pia ni tatizo lenu watanzania ni kuwa mmekuwa watu wa kulalamika na kuwa watu wa hearsay badala ya kuwa proactive. Kama kuna mtu ana malalamiko genuine kuhusu mawakili basi ayapeleke katika chamam chao, au kwa kamati ya nidhamu ya mawakili au kwa jaji mkuu au jaji yoyote. hawa niliokutajia wan uwezo wa kuwaadhibu mawakili maana mawakili pia ni maofisa wa mahakama.

Tuangalie historia kidogo ili tuweze kuelewa tatizo linakotokea:
Miaka ya nyuma ilikuwa kazi kwelikweli hadi kuingia katika uwakili wa kujitegemea na wakati wa Nyerere ilikuwa ndiyo kabisaaa mawakili wa kujitegemea wenye kufanya kazi kibinafsi ni kama " haikuruhusiwa!" it was kind of restricted.Mawakili wengi wakujitegemea walikuwa wale wa enzi za ukoloni na wengi walikuwa wahindi na wachache wazungu. Kulikuwa na shirika la sheria Tanzania Legal Corporation ambalo kama shirika la umma liliajiri mawakili kusimamia kesi za mashirika na kwa kiasi kidogo kusimamia mashauri ya watu binafsi.Nidhamu ilikuwa juu!

Polepole mawakili binafsi wazalendo wakaanza kusajiliwa lakini ilibidi kufanya usahili maalum ( bar exam) na mchujo ulifanyika ikiwa ni pamoja na kutaka maoni kuhusiana na credibility/conduct ya muombaji na kama alionekana hana maadili ilikuwa kigezo tosha kumnyima uwakili.

Miaka kama mitano sasa, usajili wa mawakili umekuwa kama umerahisishwa zaidi na idadi kubwa sana ya mawakili wamesajiliwa ikiwemo hata watu wasiokuwa na maadili.Wengi wao wamekuwa watu wakujali sana kujilimbikizia mali zaidi ya kutoa huduma.Hizi mbio za kusaka utajiri harakahara kumekuwa kunawaumiza watu kwa namna mbalimbali ambazo labda wachangiaji wanaweza kuchangia. Ndiyo tunaona na kusikia mawakili wakiwaibia na kuwadhulumu wateja wao kama ilivyotokea hapa karibuni ambapo wakili ametiwa mbaroni kwa kumuibia mteja kiasi kikubwa cha pesa ( about 400 million) na mpaka sasa yuko rumande.Zamani mawakili walikuwa wakijiheshimu na kuchunga mienendo yao hata in public. Not anymore! Ndiyo tunaona mawakili kama Magai wakipigana hadharani!

Swala la utovu wa maadili ya watu wachache ukilichukulia kwa mtazamo wa kimethali kuwa mmoja akioza wote wameoza hautakuwa sahihi. Angalia track record ya mawakili ndio utakuwa na uwezo wa kusema. Pia naomba ufahamu some of the advocates are impilcated siyo kwa sababu wameiba bali wameatest document ambayo ilifikiriwa kuwa ni genuine lakini siyo. (here i am specifically addressing issue ya wakuli wa milioni 400. Kaletewa document ya title ambayo ni genuine na record za ardhi zinaonyesha hivyo. ametumia kila jitihada kuhakikisha kuwa everything is legal lakini kumbe matapeli wameshirikiana na watu wa ardhi. Eventually wakati wa ushahidi itakuwa proven kuwa hayuko guilty lakini ndio hivyo naye yuko ndani na amekataa kwa hiari yake kuwekewa dhamana kama form ya protest yake kuwa hayuko guilty.) Kama mnahitaji formal details niombeni nitawapa lakini zisiwe zile zinazoingilia mwenendo wa kesi hii.

Maswali ya kujiuliza ni:
1. Je code of conduct ya mawakili imetupiliwa mbali na hivyo kuwafanya kuwa huru ku behave kama wahuni?

Kwa taarifa tu tanzania hatuna code of conduct ya mawakili. tunatumia common law principles. (just incase you didnt have the information). Code of conduct ya chama cha mawakili ilikuwa declared inoperative katika kesi ya Mkono versus Ladwa.

2. Je tatizo ni mchakato wa kuwasajili au ni mfumo wa kuwamulika mienendo yao?
Mchakato wa kuwasajili hauangalii nidhamu na mwenendo bali unaangalia competence. Sheria ya mawakili imeweka mamlaka ya kuchunguza nidhamu ya wanaotaka kuwa mawakili kwa jaji mkuu. jaji mkuu hana muda kwa kuwa ana mambo mengi. Hutumia dakika tano tu kumsaili mtu. kwa hiyo watanzania msipomsaidia hawezi kujua tabia ya binadamu (amabyo kwayo wakili mtarajiwa rotten anaificha).

3. TLS na Council of Legal education hawaoni iko haja kujizatiti na kuionyesha jamii kuwa nidhamu ni sifa moja wapo ya kuwa wakili na si kule kujua sheria tu?

Sitaki niwasemee TLS kwa kuwa wana watu wao wa kusema lakini nafikiri wanafanya kazi nzuri na wanashughulikia malalamiko wanayoyapata kwa ufanisi. Tatizo kubwa ni watu wenyewe kutojua uwakili unaendeshwaje na nini kifanyike. Wakili ni spokesperson wako katika kesi hivyo si lazima afuatilie mabo yanayoendelea nje kuhusu hiyo kesi zaidi ya yale yaliyo kwenye mwenendo wa kesi.

4. Can we compromise on discipline hadi fani hii idharaulike na kuonekana ya wahuni?

from the above the answer is no. take action. ripoti kwa wahusika. hatua zisipochukuliwa nenda kalalamike.

5.Jamii inaweza vipi kuwawajibisha hawa watu?
Naomba kutoa hoja ili ijadiliwa kwa undani zaidi

take action. ripoti kwa wahusika. hatua zisipochukuliwa nenda kalalamike.
 
Shadow,
Thats the whole point why I brought up this issue.Kuna vitu vingi watu hawavijui na kwa sababu hiyo unakuta wanyonge na hata wenye zao wasio makini huishia kupata hasara hata pale ambapo wana haki kabia kisheria.

Ukisoma Report ya chama cha mawakili ya mwaka 2008 utaona kuwa huu mchakakto unaendelea. Kutakuwa na compulsory insurance soon. Ila kwa ufahamu tu makampuni mengi ya uwakili yameshachukua hizo insurance. (Sisi lawfirm yetu tunayo). Ila kama mtu anataka kupata legal services cheaply kutoka kwa cheap lawyer asitegemee kupata best of legal services standards. (Rules za economics haziruhusu).
 
Chaumbeya,
Points noted.Ila ukweli bado utabakia palepale kuwa kadri siku zinavyoenda, heshima kwa mawakili na hata wanasheria inapungua kwa kasi ya ajabu.
Unayosema yapo na yatakuwepo ila hayaondoi ukweli.
 
Ukisoma Report ya chama cha mawakili ya mwaka 2008 utaona kuwa huu mchakakto unaendelea. Kutakuwa na compulsory insurance soon. Ila kwa ufahamu tu makampuni mengi ya uwakili yameshachukua hizo insurance. (Sisi lawfirm yetu tunayo). Ila kama mtu anataka kupata legal services cheaply kutoka kwa cheap lawyer asitegemee kupata best of legal services standards. (Rules za economics haziruhusu).

Umeleta points nzuri sana zinazoonyesha mwelekeo au mstakabali wa legal practice.Sijui nyie firm yenu ina umri gani, lakini najua kabisa kuwa miaka mingi nyuma kabla ya kuwa na utitiri wa mawakili, walikuwepo mawakili kama akina marehemu Kesaria ( babake na Kesaria alie kwenye practice sasa hivi) na wengine waliokuwa wakitenda kazi zao kwa uadilifu mkubwa sana ikiwa ni pamoja na kukata bima kama unavyosema.Pia walikuwa wakiwashauri wateja pale ambapo waliona kuwa wateja hawana kesi nzuri itakayoshinda mahakamani hata kama wateja walikuwa na pesa nyingi kiasi gani. Mwakili wengi wa sasa wanajali zaidi kupata pesa nyingi na si kusimamia haki kama inavyotegemewa.

Hao cheap lawyers with cheap services ndiyo akina nani? Nadhani wana JF watafurahi sana kujuzwa hili ( for all I know every practicing lawyer anatakiwa awe amepata mafunzo ya sheria ( law degree) na pia kufaulu usaili through the council of legal education ( bar exam) - hii "categorisation ya cheap lawyers/expensive lawyers inafanyika" kivipi maana they are all supposed to be competent.
 
a lawyer with a breakfast at hand,can steal more than 1000 armed soldiers!
 
Back
Top Bottom