Mawakili Medium Mwale na Loom Ojare ni majambazi?

Ni kweli mbuzi hula usawa wa kamba yake, kwa hili la ujambazi kuhusishwa na hawa wanasheria hakuna jinsi maana ndio kazi walioichagua, kuhusu hukumu, humu hatuhukumu kwani anayejua yote ni Mungu, wote hawa kama wana pesa za damu wataendelea kuishi vizuri ili wafikie muda wa kujuta dhambi zao waokoke na kuanzisha makanisa.

Ngojeni Alex. M wa Arusha pesa zilishaenea anakaribia kuokoka maana ameishasitaafu, Zombe huyu dhamira imemuhukumu mapema hana raha, anasubiriwa na wanandugu wa Maenge wamfanye MSUKULE
 
Mtu Aliyekamatwa Live Kwenye Tukio, Tena Akirushiana Risasi Na Polisi, Kwa Nia Ya Kutaka Kuwaua.

Je ingekuwa wewe ni Wakili na ambaye umethibitishiwa hayo, ungeweza kumtetea simply ana haki hiyo kisheria? Hawa jamaa lazima wawe na ubia na hao majambazi, In One Way Or Another. After All Lazima Ueleze Mambo Openly Ili Wakili Aweze Kukusaidia.

Hivyo Hawa Mawakili Huwa Wanaelezwa Kabisa Na Haya Majambazi Kila Kitu, Halafu Ndiyo Wanachukua Hizo Facts And Figures Kwa Ajili Ya Kwenda Kuzitetea Mahakamani. Yaani Hata Ile Collaboration Yao, Kwa Maana Ya Kuwatetea Majambazi, Kunawaqualify 100% Kuwa Ni Majambazi. Hivi Kweli Tutafika?

Labda nieleze kidogo jambo hili.

Tanzania kama vile zilivyo nchi zote zinasimamia demokrasia na utawala bora (kama kweli inaheshimu) inatoa fursa ya mtu kutetewa mahakamani.

Fursa hii ni haki kamili ambayo mtu yeyote mwenye mashtaka ama ya madai au jinai anapaswa kupewa. Haki hii ni muhimu hasa inapokuja swala la

kesi za jinai kama vile murder, manslaughter (kuua pasipo kukusudia) au robbery (ujambazi). Hivyo hata kama umeshuhudia mtu akimmiminia mkeo

risasi, bado anayo haki ya kupata wakili.

Kwanini haki hii?

Presumption of innocence
Dhana hii ambayo ni ya kikatiba inamtaka mtu kuitwa mkosaji pale ambapo mahakama imesema hivyo. Kabla ya

hukumu mtu huyo atabakia kuwa mtuhumiwa. Ikumbukwe kwamba kosa haliwi kosa kwa sababu kila mtu anahisi ni kosa (rejea ya zombe) bali kwa

sababu sheria inasema hivyo na mahakama imetafsiri hivyo. hivyo ni vyema mtu akapata utetezi ili hukumu yake iwe kwa haki.

Justice demands fair hearing
Ili haki itendeke mtu anapaswa kupewa nafasi ya kusikilizwa ikiwemo wakili hodari. Ikumbukwe upande wa mashtaka

humshtaki mtu kwa kosa kubwa (ambalo inawezekana hakulifanya) na lile dogo as an alternative verdict (kosa jingine ikiwa lile la kwanza

halitathibitishwa pasipo shaka yeyote (beyond reasonable doubt)). Sasa wakili anakuwa muhimu kuhakikisha mteja wake anashtakiwa kwa kosa halali.

court technicalities
Kuna a lot of techniques ambazo mtu wa kawaida hawezi kuzitambua. Katika hali hiyo utakuta kwamba mtuhumiwa

asipokuwa na wakili anaonewa badala ya kuhukumiwa kwa haki!


Important Things to note

Advocates are judicial officers. Kwa maana hiyo wakili hayupo kwa ajili ya kusimama kinyume na mahakama bali kuisaidia mahakama kufikia maamuzi

sahihi. Hivyo ndo kusema wakili hapaswi kusema uongo katika utetezi. That is professional misconduct. Anapaswa kusema kweli kuisaidia mahakama.

Tatizo ni kwamba taaluma ya sheria inamfanya mtu afahamu mbinu nyingi sana hata kuweza kuidanganya mahakama. Tamaa ya pesa ni kubwa na

hivyo watu wapo tayari kumtetea jambazi asifungwe miaka 30 for exchange of 500milions which is professional misconduct too maana advocates

fees are prescribed by law!

Utashi binafsi unaomfanya wakili akatae kutetea watu wa namna hii (Prof Maina aliacha kupractice kwa sababu hii). Inawezekana kabisa hawa

mabwana wanaingia katika kundi hili, kwamba money first, justice later! No wonder hata bible inaona its hard kwa wanasheria kuiona mbingu!
 
Tanzania ni nchi inayoshangaza sasa hivi hawa jamaa wana kesi kwa kuwa na pesa nyingi kwenye bank wakati ni wafanyabiashara. Je tutawalaumu wafanyabiashara kuweka pesa nje sasa wakati wakiweka pesa nchini wanachunguzwa!!. Badala ya kuwafuata malawyer ni vema wangefuata wafanyakazi wa serikali wanaoficha pesa nje. Kama mtu ni mwizi asingeweka pesa kwenye account za Tanzania!!!
 
Mhh...kudadeki... nanusa mkono mrefu wa Rostam hapa, akitumia wakili maarufu(kama kawaida yake, mnakumbuka Kagoda na Maregesi) kufadhili kampeni za swahiba wake EL za uenyekiti wa chama 2012...

Hao interpol ni geresha tu... hapo ni game of chess between JK na Watuhumiwa wa Gamba...the trophy being CCM chair, 2012.

Kifupi Mwale kwa vile anahistoria ya ujasiri wa kifisadi, ametumiwa tu kama bangusilo.....nchi ina mabakhresa, mazakaria, kina mkono,
manji, mo dewji, na matajiri kibao wenye really fat accounts, hao interpol wafike bongo tu na kwenda arusha kwa wakili mmoja ambaye
hajulikani sana nje ya arusha. Si bure!!

BTW thats just my theory, dont read too much between the lines.
 
Inawezekana wanamegewa kidogo na hayo majambazi, ila siwalaumu sana mbona mkono naye anatetea mafisadi? Hivi sheria inaruhusu kumtetea mtu yeyote hata kama jamaa anarekodi ya ujambazi? Hawa wanasheria watajibu nini kwa Mungu siku ya hukumu?

It is more difficult for a camel to pass through the eye of a needle than for a lawyer to enter the kingdom of heaven
 
Kitakachomwokoa ni jinsi atakavyotoa maelezo ya namna alivyopata fedha hizo kama ni halali itakuwa kazi rahisi na kama sio halali ana kibarua kigumu kukwepa mkono wa fani yake ya sheria
 
Kithuku hawa jamaa kwanza ingekuwa vyema tukapata CV zao,Hivyo wana JF kama kuna watu wenye CV za hawa jamaa ni vyema zikaletwa manake umesema mambo mawili muhimu sana nayo ni "Nafahamu pia huu usemi: "A bright lawyer knows the law (might be LL.B Hons first class) but a smart lawyer knows the judge" (might have passed his law degree very poorly and by sheer luck, but wins cases by all means!) Hawa jamaa wako upande upi hapa?"

Cv zitatwambia hawa jamaa wako wapi,manake wakiwa bright [Intellectual] wasinge simama upande huo wa Majambazi kwa kuwa welevu wao uwa unawapa kile ambacho DK Mvungi amekisema ufahamu [consciousness is your mind and your thoughts.].Ukiwa mwelevu unazingatia mawazo ndani na ufahamu mkuu.

Ndio maana wanasema kuna aina tatu za watu dunian wale wanofanya mambo yatokee,wale ambao wanashaangaa yaliyotokea na wale wasiojua chochote kilichotokea [There are three kind of people in the world,those who make things happen,those who wonder wht happen and those who dont know wht happen].Waelevu wanasimama kundi la kwanza.Kwa kuwa uwa wanajua kuwa hata kama akimtetea Jambazi kanuni za maumbile yaani asilia [nature] itamuhukumu,ambayo ndio hiyo watu usema muda utasema [time will tell].Na hukumu ya nature inakula mpaka uzao wa kizazi chako.Jambazi kama jamabzai hukumu yake itatendwa na yeye mwenyewe na hata watoto wake wako salama kukanusha kuwa hawahusiki na tabia ya baba yao.Kwa ukatili wote wa Idd Amini lakini kuna watato wa amini wako na furaha.Je umeona Muhamar Gaddafi aliyemtetea Idd Amini leo hukumu yake imekula na inaendelea kula mpaka kizazi chake yeye.

Na kama jamaa hawa ni smart,basi ni kitu cha muda mfupi kwani wanachofanya wanajua nani ni nani [Its all about Connection] wanajua kila hatua kabla ya tukio na baada ya tukio na mwisho wa tukio lakini hawajui impact ya tukio na siku zijazo baada ya tukio.Ni muda mfupi wanao wa kuwa smart yaweza kuchukua miaka kumi mpaka ishirini kumilki uchafu huo lakini mwisho ni aibu na mzigo wa aibu daima kwa familia zao.Kwa kuwa master mind wa matukio hayo ya ujambazi ni wao.Kwa kuwa kabla ya wizi majambazi wanachofanya ni kupewa dondoo [Hints] wafanye kadha wa kadha ili waende sambamba na utetezi kama ikitokea kukamatwa basi ziwe ni nguzo za utetezi.wakiludi upande wa pili wa mahakama wanajua nani ni nani [who is who].

Lakin ni vyema kutujuza wana JF. waelevu kazi kwao,tayari sehemu ya kuonyesha kuwa mungu aliwapa uwezo kudhibiti walio smart na kuwahukumu ili jamii isonge mbele.
 
...........................Ndio maana kina Mkono walichukua kesi ya Ditopile "fasta" kwani kwake yeye falsafa yake ni "The End Justifies the Means", ndo sababu mpaka kwenye orodha ya mafisadi yumo. So kwa kina Ojare na mwenzake you knever know ...the world is full of surprises, but time will tell...
Kuna mambo hutakiwi kuwa Sheikh Yahya kuyaona, haya yalisemwa miaka takriban minne iliyopita, sasa yametimia, hujafa hujaumbika Mwale.


 
Wengi wameongea laikini hawajui nini kazi za wakili .

Hakika wakili kazi yake ni kuchambua sheria kwa nia ya kumrahisishia hakimu kutoa hukumu sahihi. Kwa msingi huo wakili anaweza kusimama upande wowote wa kesi (mshitakiwa ima mshitaki).

Hao mawakili wametenda kazi zao ipasavyo kama zilivyo katika viapo vyao
 
Kithuku hawa jamaa kwanza ingekuwa vyema tukapata CV zao,Hivyo wana JF kama kuna watu wenye CV za hawa jamaa ni vyema zikaletwa;



...Nimeipata hii; ''Prominent lawyer, Advocate Medium Mwale, an alumni of the Enaboishu having completed his O'Level studies at the school in 1987, pledged his personal contribution of Tsh. 4 million to help in the furniture part of the project. The money will buy 80 chairs and 80 tables''.

Na hapa chini anatuhumiwa kuwaingiza chaka watu,

1.
Application No. 5 of 2010: The Registered Trustees of the Sisters of Notre Dame versus Advocate Median Mwale & Ruwaichi John;
The Complainant allege that in February 2009, the Advocate (as Attornees of Abdallah Hassan) signed a Sale Agreement with the complaints respectively as Vendors and Purchasers in respect of Farm No. 131(CT No. 5584); and that on 13[SUP]th[/SUP] February 2010 the Complainants paid to the Advocates a sum of Tsh. 195,000,000/= Million as full consideration (purchase price). It is further alleged that the Advocates have ever since failed to complete the conveyance while at the same time refusing to refund the money. The Advocates have filed their Reply to the allegations stating that there were various stages and encumbrances to overcome before finalizing the process and that the Complaint is premature, vexations, and frivolous. They have also raised a preliminary objection challenging the jurisdiction of the Committee to entertain the matter. The matter is scheduled for mention on 24[SUP]th[/SUP] September 2010.
 
Wakubwa inasisimua jinsi hii mada ilivyokuja kuibuka upya tangu nilipoianzisha miaka 4 iliyopita.

Namshukuru Invisible kwa kuileta tena ikiwa imehuishwa.

Bado ninayo mashaka kuhusu dhamira ya hawa mawakili, japo kama nilivyosema mwanzo sina ushahidi wowote dhidi yao. Mazingira yanatia shaka sana. Na mji wetu huu ni mji wenye majambazi wanaofahamika waziwazi na huwa tunakutana nao sehemu mbalimbali wakitamba waziwazi.

Katika novels za John Grisham (The Partner, The Firm, The Client, A Time to Kill, The Testament) nimesoma jinsi mawakili wanavyoweza kuungana na majambazi na bado wote mbele ya sheria wakaonekana hawana hatia japo ukweli unaonesha vinginevyo, wanatumia udhaifu uilioko kwenye mfumo wa sheria.

Ninatamani kuona hali hii ikirekebika na kutuwezesha kuona tofauti ya wazi kati ya haki na sheria, tuiondolee jamii yetu uhitaji wa kulipiza kisasi pale haki inapokosekana.
 
Nimezisoma pia na tuhuma zinazomkabili za money laundering. Kwa background ya watu anaowatetea mara kwa mara na ambao hatimaye hujenga nao uhusiano wa kikazi, hili linawezekana kabisa. Tusubiri kusikia maujanja ya mawakili hapa.
 
Now i understand, what it it means " the world is full of surprise"
 
me nadhan jamaa wameamua kuwa experts ktk kesi za mtindo huo ambao wengi wanaziogopa na kwa kuwa wana risk maisha na taaluma ndo maana wana chaji ghali!au wamemaua kusimama upande wa solid minority ishu ya kwenda mbinguni ni la kiimani zaidi na wanajua mungu gani wanamuabudu na wana amini lipi!
 
Heko Interpol kwa kunusa ufisadi wa hao mawakili, serikali isaidie ili kuwatokomeza.Hao jamaa wako karibu sana na EL na majambazi yote wanayoyatetea kama Justine Nyari ni marafiki wa EL.Fanyeni utafiti mtagundua ukweli huo.JK usilegeze kamba mafisadi watyakusumbua sana maana wana mkono mrefu, ndio maana Pinda alisema hawakamatiki.
 
Back
Top Bottom