Mavazi yetu tunayovaa yanatuelezea sisi tulivyo.

Vimini vinasema nini kuhusu mvaaji?Suruale je?Kaptula?Gauni?Baibui?Tshirt??Suti?? Inawezekana ikawa kweli kwa kiasi kidogo ila huwezi kujudge mtu kwa vazi alilovaa maana vazi sio tabia binafsi ya mtu.Ni interest tu kama ulivyo mziki...kwasababu tu mtu anasikiliza reggae au rap haina maana anavuta bangi!Tujifunze kuangalia zaidi ya mavazi!

kha...i think u missed the point!!wewe umeingiza tabia wakati mtoa mada hajasema tabia. Yeye ameongelea 'namna ya mtu'. Tabia na 'namna ya mtu' ni vitu viwili tofauti!
 
Kuna ukweli ndani yake kwani kila vazi lina ashiria tabia ya mtu, jersey zinavaliwa na wanamichezo, kanzu ni vazi la kawaida la asili ya mashariki ya kati, joho ni makanisani na majaji na ni vazi la kawaida la watu wa afrika magharibi. Bikini huvaliwa beach na zipo za aina tofauti tofauti, Suruali zipo za jeans huwezi kuvaa Bungeni na haipendezi kuvaa kwenye nyumba za ibada. Overall ni nguo za mafudi, apron zinavaliwa na wapishi, magwanda yanavaliwa na askali nazo ziko aina aina kulingana na jeshi lenyewe. Vimini, vitop, vibano, nguo nyepesi na laini, vinavyo acha sehemu kubwa ya mwili wazi, mipasuo ya kutisha, milegezo na kata-K ni vya kutokea night kwenye starehe. Suruali za vitambaa ni vazi linalo kubalika sehemu nyingi. Mashati kwa wanaume mengi ni ya kawaida na hayana ukakasi kwa maeneo mengi.

Ukikosea kuvaa mavazi haya na ukavaa maeneo siyo, utaonekana una lako jambo! Watu watakushangaa na utaonekana kama kituko na utapachikwa majina ya ajabu ajabu kulingana na muonekano wako!

Nimekubali maelezo yako yenye ufafanuzi mpana.Nikweli haiwezekani kuingia kanisani ukiwa na baibui tena na ninja juu Utaonekana kituko cha karne yakhe! mavazi humtafsiri mtu alivyo
 
Nduyo maana katika vitabu vyote vitakatifu imeharamishwa Mwanamke kuvaa mavazi yanayomdharilisha kwa kumuonesha tupu zake na vitabu vyote havikuacha kupiga marufuku kwa mwanamke au mwanaume kuvaa mavazi ya jinsia tofauti na yeye. Msiba mkubwa umeyakumba makanisa kwani hawakemei uozo huo kiasi kwamba waumini sasa wanaenda wamevaa sox kanisani, wanavaa sket fupi kiasi kwamba ****** yote wakikaa kwenye benchi yanakuwa nje kiasi kwamba wanaenda kulinajisi kanisa. ukiwaangalia wanawake wakienda au kurudi kanisani utadhani wametoka cassino au wapo wanajiuza. inabidi hili lisimamiwe kurudisha heshima na utu wa mtanzania
 
yan mwanamke yeyote akivaa nguo ambayo geographia ya mwili wake inajidhihirisha especial trouse,min au hata gauni zingine wanasema ni new arrivols wakivaa wanaivuta upande mmoja wana bana na chupi yani kana kwamba ni defu labda halafu unamkuta m2 amebeba bible na mkono wa kushoto wale wanawatafutia waumin thambi 2 cz cthan kama kuna m2 anaweza kuvumilia hali kama hiyo
 
Je wanawake wanaovaa mawigi mnasemaje wadau? Au ni sawa tu kwa utukufu wa Mungu!! Mbona watumishi wa Mungu hawayakemei makanisani? Wanayavaa kwa kumtukuza nani?
 
Back
Top Bottom