Mauzauza - wewe ungefanyaje

meeku

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
569
108
True story.

Ni mtu mzima alitembelewa na baba mkwe wake (mtu mzima unaelewa kuwa ana watoto wakubwa).

Sasa ukafika wakati wa chakula.

Baba mwenye nyumba (mtu mzima) akamwambia mkewe apakue sahani moja wale na baba mkwe.
Mama akatekeleza maelekezo na kuwapelekea chakula kwenye kivuli nje na wao kubaki ndani.

Huku nje baba mwenye nyamba akachukua pilipili iliyowekwa pembeni, bila kumuuliza baba mkwe
akaanza kuikorogea kwenye ubwabwa ambao tayari umeshachanganya na mboga.

Du, noma, kumbe baba mkwe hatumii pilipili. Hasira zikamjaa balaa. Kumbe nae hutumia ugoro, alichofanya nae akachukua ughoro akamimina kwenye ubwabwa, akakoroga.

Ikawa noma zaidi ya noma. Hapa baba mwenye nyumba hakuuliza, ila yakaanza makonde, tuf! tuf! tuf! hadi akamvunja baba mkwe jino.

Wanashtuka ndani ndo wanakuta midamu na hali ndo hiyo.

Wewe ungefanyaje???

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom