Maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa mama mjamzito: Fahamu visababishi, ushauri na tiba

Next Level

JF-Expert Member
Nov 17, 2008
3,153
176
1588480196649.png
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA KUHUSU TATIZO HILI
Jamani naomba wataalam mnisaidie:

Mke wangu anamimba ya mwezi mmoja hivi lakini occassionaly huwa analalamika kwamba anasikia maumivu kwenye eneo la chini ya kitovu chake lakini pia huwa anatapika sana baada ya kupata maumivu hayo! Je hii hali inasababishwa na nini kitaalam? Au itakuwa unique kwa yeye tu?
---
Heshma yenu doctoz na members wote,

Mimi ni mjamzito wa meizi 4 na siku 12, tatizo langu ni kuumwa tumbo mara kwa mara anzia kwenye kitovu kuelekea chini. Nimeshaeleza tatizo langu KCMC wakaniambia nipunzike nisifanye kazi yoyote lakini bado tatizo halijaisha. Wakati mwingine nahisi km nimebanywa na haja kubwa nikienda chooni haitoki na maumivu yanaendelea.

WAPENDWA WANGU NISAIDIENI JAMANI MANA NAOGOPA SANA. MUNGU AWABARIKI.
---
Habari humu ndani,

Wife anapata maumivu makali sehem za nyonga hasa upande wa kulia, hasa usiku wakat anapotak kulala. Ni mjamzito miez 7.

Baada ya kumpeleka zahanat Ucku alipew amoxilin 2x3, phenobabitone 1x2, na diclofenac, alvotumia Ucku zilimpa nafuu japo nkawaza sana kuhusu dawa hzo, nkawa na hofu Sana ckumpa tena. Tatzo limejirudia Ucku uliofuata. Vp aendelee kunyw hz dawa?

Hofu dawa c nzuri saaana kwa mjamzito hasa diclofenac
===
UFAFANUZI WA JUMLA KUHUSU TATIZO HILI
SABABU 10 MAUMIVU YA TUMBO KWA MJAMZITO
WAJAWAZITO wengi huugua wakati wakiwa na ujauzito. Zipo Sababu zinazofanya kutokea kwa maumivu ya tumbo wakati wa miezi mitatu ya kwanza ya mimba.

Kuna matatizo mengi ambayo yanahusiana tu na mimba, hata hivyo ni muhimu kukumbuka kwamba hali yoyote ambayo husababisha maumivu kwa mgonjwa asiyekuwa na ujauzito inaweza pia kutokea kwa mama mjamzito.

Tofauti kati ya watu hao wawili hupatikana baada ya uchunguzi. Maumivu ya tumbo kwa mjamzito ni changamoto kwa sababu wengi hupatwa na kichefuchefu, kutapika na maumivu ya tumbo hujitokeza mara nyingi. Mfuko wa uzazi unapotanuka unaweza kusukuma viungo vingine kando ndani ya tumbo.
Upungufu wa damu na leukocytosis ni kawaida katika mimba ya kawaida na si viashiriwa vya upungufu wa damu au maradhi.

Kiinitete kinapojipandikiza katika kuta za ndani za mfuko wa uzazi kinaweza kusababisha maumivu ya tumbo, ambayo huchukua muda wa siku mbili au tatu na kiasi kidogo cha damu ukeni hutoka. Mara nyingi kiasi hiki cha damu huwa ni kidogo na hutokea kati ya siku saba au 12 baada ya tarehe inayohisiwa mimba kutungwa, mara nyingi kipindi hiki hukaribiana na siku ambayo mwanamke alikuwa anatarajiwa kuingia hedhi.

Hivyo, wagonjwa mara nyingi hufanya makosa kwa kufikiri kuwa wameingia katika siku zao kama kawaida. Mimba iliyotunga nje ya mfuko Tatizo hili husababisha maumivu kwa akina mama wengi walio na mimba nje ya mfuko wa mimba. Tatizo hili linaweza kubainika kwa kutumia Ultrasounda na kipimo cha homoni cha HCG.

Uzuri ni kwamba tatizo hili linatibiwa kama dharura kwa mama kufanyiwa upasuaji. Kutoka kwa mimba Mimba inaweza kutoka yenyewe au kutolewa kwa makusudi. Tatizo hili huambatana na maumivu pamoja na kuvuja damu. Utoaji wa mimba usiokuwa salama unaongoza kusababisha vifo vya akina mama katika nchi zinazoendelea. Uvimbe kwenye mirija ya mayai (Ovarian cyst) Wakati mwingine uvimbe huu hupasuka au kujizungusha.

Hata hivyo, unaweza kupungua na usipopungua unaweza kuondolewa kwa njia ya upasuaji hasa wakati wa muhula wa pili wa ujauzito. Kujizungusha kwa mirija ya mayai (Ovarian torsion) Hii hujitokeza mara chache. Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi pia husababisha maumivu hasa unapokuwa mkubwa. Tatizo hili linaweza kusababisha ujauzito kutoka hasa katika miezi ya awali.

Kidole tumbo (Appendicitis) Kidole tumbo hujitokeza kwa uwiano sawa kama wanawake ambao hawana ujauzito. Matibabu ya ugonjwa huu ni upasuaji. Mara nyingi wanawake wengi hupata uchungu baada ya upasuaji. Mawe kwenye mfuko wa nyonga Lakini pia kutokana na mabadiliko ya homoni wanawake wengi hupata tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo.

Tatizo hii huweza kugunduliwa kwa njia ya kupimwa na kipimo cha Ultrasound na matibabu yake hutegemea na dalili alizonazo mgonjwa. Uvimbe (Inflammation) kwenye mfuko wa nyongo Hili ni tatizo la ghafla linalosababisha maumivu makali ambalo pia hujitokeza wakati mwanamke ana mimba. Tatizo hili mara nyingi husababishwa na mawe kwenye mfuko wa nyongo.

Matibabu yake hutumika dawa za kuua bakteria yaani Antibiotics. Wanawake wengi wakati wa hujauzito hupata maambukizi kwenye njia ya mkonjo mara kwa mara. Hii ni kutokana na mabadiliko yanayojitokeza wakati wa mimba. Sababu nyingine ya maumivu husababishwa na Round Ligament.

Ligament hii ndiyo inayoshikilia mfuko wa uzazi. Mfuko wa uzazi unavyozidi kukua, ligament hii huvutika na kusababaisha maumivu.

Dawa za maumivu husaidia kwa tatizo hili. Ultrasound hutumika katika uchunguzi wa maumivu ya tumbo wakati wa ujauzito. Kongosho, mfuko wa nyongo na kidole tumbo vyote huonekana kwa mama mjamzito. Vipimo vinavyotumia mionzi vitumike tu pale inapohitajika kwa mama mjamzito.
===

BAADHI YA MAJIBU NA USHAURI ULIOTOLEWA NA WADAU

Nimeona nitoe feedback ili na mwingine akijapatwa na issue asihangaike sana,

Kufupi nilimpeleka wife Aghakhan Hospital, pamoja na vipimo vingine vya kawaida, amefanyiwa ultrasound na matokeo yake ni kama ifuatavyo;
1: Maji yapo ya kutosha (wataalam mnajua umuhimu wake hapo)
2: Foetus kimeonekana
3: Hicho kifoestus kinaonyesha uhai
4: Na kifeotus hicho ni wiki 9=2.5months

Zaidi ya hayo, wamekuta ''Plenty of fluid collection in Pod'' ambalo ndicho chanzo cha maumivu chini ya kitovu (kufuatana na Dr husika) na kitaalama wanaita kuwa ni PID problem '' PID in pregnancy''!

Matibabu:
Dr. Amerecommend Erythromycin (7/7) kwa siku saba, kufuatana na yeye tatizo linaweza kwisha!

Wazazi wenzangu take note please. Hujafa hujaumbika and thanks MAMA kwa ushauri!

Cheers
---
PID ni Pelvic inflammatory Diseases- yaweza kusababishwa na vijidudu vya aina mbalimbali, ingawa PID zingine zasababishwa na STI (sexually transmitted infections) ni muhimu ku-note kuwa kuna zingine haziwi sexually transmitted.

Mwanamama aweza kuji-infect peke yake na vijidudu kutoka njia ya haja kubwa eg. kwa mfano wakati anachamba! Kwa hiyo, mke kuwa na PID haina maana kuwa kaambukizwa kwa ngono, ama kuwa na umuhimu wa mme kupima!

Kwa hiyo ni imani yangu hayo maumivu ni kwa ajili ya hiyo PID, ikishatibiwa mambo yatakuwa murua, cha muhimu ni follow up ya karibu, ndio kusema usicheze mbali na aga khan.

Mungu awajaaliye.
---
Heshima mbele kwako (Chinkala) na wengine wote walio changia hapa!

Naona mkuu Chinkala upo interested sana kujua my status, yaani kama na mimi ni similar infection or not! na pia kujua infection aliyonayo mamsapu imetokana na nini?

1. As of now, mimi sina infection yoyote .....nifanyiwa urinalyisis (two weeks ago)
2. PID kwa wife niliambiwa of course ni infection iliyo sababishwa na mkusanyiko mkubwa wa liquid kwenye POD.......nikaambiwa pia tatizo hili ni common kwa wanawake wenye mimba...ndo maana hata likaitwa ''PID IN PREGNANCY. Sikuishia hapo, nilimuuliza Dr. source ya huo mkusanyanyiko wa liquid ambao later umesababisha infection...akaniambia simply.....

''hayo ni matatizo ya wanawake'' akaendelea kusema.....''sababu zinawezakuwa ni nyingi...moja wapo ni logistics (hope has to do with vitambaa, always etc) zao wakati wa breeding'' etc na ofcourse akaniambia kuwa tatizo hilo alikuwa nalo kabla ya kupata ujauzito ila limekuwa speeded up na pregnancy!

Hope mkuu Chinkala, umenipata vilivyo though ushauri wake nitaendelea kuufanyia kazi, cause have nothing to loose!

Cheers
---
Pole sana kwa maumivu unayoyapata, nahisi huu ni ujauzito wako wa kwanza! Haya maumivu unayo yapata yanasababishwa na mvutano unaotokea ndani ya tumbo na misuli ya kizazi, lakini pia mlalo na activities za mtoto awapotumboni hii pia hutokea.

Kina mama wenye retroverted uterus pia hupata maumivu kama haya. Ni vizuri ukaanza mazoezi sasa badala ya hiyo bedrest uliyopewa. Unapolala tumia zaidi ubavu wa upande wa shoto hii pia husaidia. Otherwise nakutakia kila la kheri na Mungu akujalie mtoto kwa usalama.
---
Habari yako Henya,
Una tatizo linaloitwa PPGP(Pregnancy-related pelvic grindle pain) ambalo husababisha maumivu kwenye maeneo ya fupa la mbele au nyuma(pelvic bone).
Dalili za tatizo hili ni:

  • pain over the pubic bone at the front in the centre
  • pain across one or both sides of your lower back
    [*=left]pain in the area between your vagina and anus (perineum)

Maumivu haya huongezeka pia ukiwa una tembea,unapanda ngazi,ukisimama kwa mguu mmoja au ukigeuka kitandani.

Hali hii husababishwa na kuonegezeka kwa uzito wa tumbo(ujauzito) au kama ulikuwa na historia maumivu ya mgongo na nyonga kabla,ajali au kuanguka na kufanya kazi nzito.

Hali hii utaiepuka vipi:
- Kufanya mazoezi ya kwenye maji au mazoezi kwaajili ya hio pelivic bone
- Kukandandwa
- Epuka kufanya kazi nzito na kubeba vitu vizito,kusimama muda mrefu,kutembea muda mrefu
- Pumzika vyakutosha
- Ukigeuka kitandani jaribu kugeuka na magoti pamoja,unaweza pia kujaribu kuweka mto kati kati ya miguu
- Usivae viatu virefu

Haya mazoezi yatakusaidia kupunguza maumivu
  • Get on your hands and knees with your back straight. A mat can help cushion your knees.
  • Try to pull your abdominal muscles in. Tuck in your buttocks. This will tilt your pelvis up. As your pelvis tilts, your back will rise toward the ceiling.
  • Hold and count to 5, then relax.
Leg Lifts

This strengthens the muscles of your back, buttocks, and abdomen.

  • Get down on your hands and knees. Put your arms directly under your shoulders. Keep your knees shoulder-width apart.
  • Round your back. Then lift your left knee and gently bring it toward your elbow. Look at your knee as you raise it. (Stop moving your knee if you feel pressure in your abdomen.)
  • Keeping your knee slightly bent, extend your leg. Lift your leg until you feel a stretch in your low back. Dont lift your leg higher than your hip.
  • Hold for 5 counts, then lower your left leg. Repeat the exercise with your right leg.
Au jaribu mazoezi haya:

Lala kawaida,kunja magoti (60 degrees),miguu ikiwa sakafuni,then jaribu kujiinua sehemu ya kiuno/mgongo, unaweza kujaribu mazoezi haya mara 8-10 kwa siku
---
Maumivu ya tumbo wakati wa miezi mitatu ya kwanza ya mimba ni mojawapo ya matatizo yanayolalamikiwa na kina mama wengi. Kuna matatizo mengi ambayo yanahusiana tu na mimba, hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba hali yoyote ambayo husababisha maumivu katika mgonjwa asiyekuwa na ujauzito inaweza pia kutokea kwa mama mjamzito, ingawaje historia na uchunguzi vinaweza kuwa tofauti.

Kwa asili kutathmini maumivu ya tumbo kwa mama mjamzito ina changamoto kwa sababu kichefuchefu, kutapika, na maumivu ya tumbo hujitokeza mara nyingi kwa wajawazito wengi . Mfuko wa uzazi unapotanuka unaweza kusukuma viungo vingine kando ndani ya tumbo, upungufu wa damu na leukocytosis ni kawaida katika mimba ya kawaida na si viashiriwa vya upungufu wa damu au maradhi. Mgonjwa ambaye mimba imetunga nje ya mfuko kipimo cha ultrasound kinaonyesha majimaji na uchafu ndani ya mfuko wa uzazi bila ushahidi wa mimba.

Kiinitete kinapojipandikiza katika kuta za ndani za mfuko wa uzazi inaweza kusababisha maumivu ya tumbo , ambayo huchukua muda wa siku 1- 2 na kiasi kidogo cha damu ukeni. Mara nyingi kiasi hiki ni kidogo na hutokea kati ya siku 6 -12 baada ya tarehe inayohisiwa mimba kutungwa , mara nyingi kipindi hiki hukaribiana na siku ambayo mwanamke alikuwa anatarajiwa kuingia hedhi. Hivyo, wagonjwa mara nyingi hufanya makosa kwa kufikiri kuwa wameingia katika siku zao kama kawaida.

Mimba iliyotunga nje ya mfuko ni tatizo linaloongoza kusababisha maumivu kwa kina mama wengi sehemu mbalimbali duniani. Tatizo hili linaweza kubainika kwa kutumia Ultrasounda na kipimo cha homoni HCG. Hata hivyo tatizo hili linatibiwa kama dharura kwa mama kufanyiwa upasuaji.

Sababu nyingine ni kutoka kwa mimba. Mimba inaweza kutoka yenyewe au kutolewa kwa makusudi. Tatizo hili huambatana na maumivu pamoja na kuvuja damu. Utoaji wa mimba usiokuwa salama unaongoza kusababisha vifo vya kina mama katika nchi zinazoendelea.

Uvimbe kwenye mirija ya mayai (Ovarian cyst). Wakati mwingine uvimbe huu hupasuka au kujizungusha. Hata hivyo unaweza kupungua na usipopungua unaweza kuondolewa kwa njia ya upasuaji hasa wakati wa muhula wa pili wa ujauzito.

Sababu nyingine ni kujizungusha kwa mirija ya mayai (Ovarian torsion). Hii hujitokeza mara chache.
Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi pia husababisha maumivu hasa unapokuwa mkubwa. Tatizo hili linaweza kusababisha ujauzito kutoka hasa katika miezi ya awali.

Kidole tumbo (appendicitis) hujitokeza kwa uwiano sawa kama wanawake ambao hawana ujauzito. Matibabu ya ugonjwa huu ni upasauji. Mara nyingi wanawake wengi hupata uchungu baada ya upasuaji.

Kutokana na mabadiliko ya homoni wanawake wengi hupata tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo. Tatizo hii huweza kugunduliwa kwa njia ya ultrasound.Matibabu hutegemea na dalili

Uvimbe(inflammation) kwenye mfuko wa nyongo ni tatizo la ghafla linalosababisha maumivu makali ambalo pia hujitokeza wakati wa mimba. Tatizo hili mara nyingi husababishwa na mawe kweny mfuko wa nyongo. Antibiotics hutumika katika matibabau ya uchongo huu.

Wanawake wengi wakati wa hujauzito hupata maambukizi kwenye njia ya mkonjo mara kwa mara. Hii ni kutokana na mabadiliko yanayojitokeza wakati huu wa mimba.

Sababu nyingine ya maumivu husababishwa na ROUND LIGAMENT. Ligament hii ndio inayoshikilia mfuko wa uzazi tumbo. Mfuko wa uzazi unavyozidi kukua, ligament hii huvutika na kusababaisha maumivu.
Dawa za maumivu husaidia kwa tatizo hili.

Ultrasound hutumika katika uchunguzi wa maumivu ya tumbo wakati wa ujauzito. Kongosho, mfuko wa nyongo na kidole tumbo vyote huonekana kwa mama mjamzito. Vipimo vinavyotumia
mionzi viyumike tu pale inapohitajika kwa mama mjamzito.

View attachment 146311View attachment 146312View attachment 146313

PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HIZI:
- Fahamu mambo haya muhimu kuhusu afya ya mama mjamzito - JamiiForums

- Mama mjamzito : mambo ya kufanya na mambo ya kuepuka kufanya - JamiiForums

- Dalili hatari kipindi cha ujauzito ambazo si za kupuuzia
 
Mpeleke hospitali! usije ukaleta balaa.

Mkuu nilimpeleka lakina daktari aliyemchunguza, kasema ni hali ya kawaida lakini mimi inanisumbua kidogo kwani mimba yake ya kwanza hakupata shida hiyo! Please yoyote anayefahamu daktari bingwa wa kina mama in Tanzania anipe contact may be through PM.

Thanks Kang kwa ushauri!
 
Jamani naomba wataalam mnisaidie: Mke wangu anamimba ya mwezi mmoja hivi lakini occassionaly huwa analalamika kwamba anasikia maumivu kwenye eneo la chini ya kitovu chake lakini pia huwa anatapika sana baada ya kupata maumivu hayo! Je hii hali inasababishwa na nini kitaalam? au itakuwa unique kwa yeye tu?

Mbali na maumivu hayo, je anasikia baridi, au anapata homa, au ana bleed?
 
Mbali na maumivu hayo, je anasikia baridi, au anapata homa, au ana bleed?

Hasikii baridi, homa wala habreed! yeye anadai eneo la chini ya kitovu linakuwa kama kapigwa sana, akiwa anapata maumivu hayo kutembea amenyooka hawezi bali hutembea kama kikongwe fulani hivi! cha ajabu pain hulast kama kwa dakika 20 mpaka 30 hivi! then anakaa kama hata masaa matano, hali hiyo hujirudia tena!

Thanks mama
 
Mpeleke tu hospitali haraka, mimba zina mambo yake.

Vingineyo waweza mpeleka afanye ultrasound (TMJ ya mjini karibu na Burhani Hospital). Kama kuna problem atawaelekeza mumwone daktari.
 
Mpeleke tu hospitali haraka, mimba zina mambo yake.

Vingineyo waweza mpeleka afanye ultrasound (TMJ ya mjini karibu na Burhani Hospital). Kama kuna problem atawaelekeza mumwone daktari.

Asante kwa ushauri, tajaribu kwenda huko!
 
Mpeleke tu hospitali haraka, mimba zina mambo yake.

Vingineyo waweza mpeleka afanye ultrasound (TMJ ya mjini karibu na Burhani Hospital). Kama kuna problem atawaelekeza mumwone daktari.

Nimeona nitoe feedback ili na mwingine akijapatwa na issue asihangaike sana,

Kufupi nilimpeleka wife Aghakhan Hospital, pamoja na vipimo vingine vya kawaida, amefanyiwa ultrasound na matokeo yake ni kama ifuatavyo;
1: Maji yapo ya kutosha (wataalam mnajua umuhimu wake hapo)
2: Foetus kimeonekana
3: Hicho kifoestus kinaonyesha uhai
4: Na kifeotus hicho ni wiki 9=2.5months

Zaidi ya hayo, wamekuta ''Plenty of fluid collection in Pod'' ambalo ndicho chanzo cha maumivu chini ya kitovu (kufuatana na Dr husika) na kitaalama wanaita kuwa ni PID problem '' PID in pregnancy''!

Matibabu:
Dr. Amerecommend Erythromycin (7/7) kwa siku saba, kufuatana na yeye tatizo linaweza kwisha!

Wazazi wenzangu take note please. Hujafa hujaumbika and thanks MAMA kwa ushauri!

Cheers
 
huyo doktari alikwambia kirefu cha PID?? kama ni pelvic inflammatory dx. je ni infection gani hasa inayoendelea (unaweza ku-mute)...wewe umepima na kupewa dawa? nadhani usibweteke, endelea kutafuta opinions nyingine kadri uwezavyo na haraka!!

Sidhani kama ni PID unayofikiria. Itakuwa imesababisha na hiyo fluid accumulatin kwenye pod.
 
hapana, key hapo ni matumizi ya erythromycin ambayo ni abx....lazima kuna amniotitis flani ambayo imesababishwa na PID ndio ina lead kwa hiyo poly hydramnios!!! maji kuwa mengi sio accident, lazima kuna sababu na hiyo ndio issue ya kufikiria....ni nini underlying cause ya tatizo hili? i suggest jamaa nae akapime kunaweza kuwa na STD hapo! sorry....

Soma maelezo yake vizuri. Huyo dr aliyewaattend angetoa ushauri huo kama kungekuwa na possibility hiyo. Kuna mengi sana katika obs.
 
Erythromycin is a macrolide antibiotic that has an antimicrobial spectrum similar to or slightly wider than that of penicillin, and is often used for people who have an allergy to penicillins. For respiratory tract infections, it has better coverage of atypical organisms, including mycoplasma and Legionellosis. It is also used to treat outbreaks of chlamydia, syphilis, acne, and gonorrhea.

Nadhani jamaa anauliza hiyo infection imetokea wapi?
 
huyo doktari alikwambia kirefu cha PID?? kama ni pelvic inflammatory dx. je ni infection gani hasa inayoendelea (unaweza ku-mute)...wewe umepima na kupewa dawa? nadhani usibweteke, endelea kutafuta opinions nyingine kadri uwezavyo na haraka!!

Ni muhimu kupata opinion kutoka kwa daktari mwingine. Kila la heri na ujauzito wenu.
 
PID ni Pelvic inflammatory Diseases- yaweza kusababishwa na vijidudu vya aina mbalimbali, ingawa PID zingine zasababishwa na STI (sexually transmitted infections) ni muhimu ku-note kuwa kuna zingine haziwi sexually transmitted.

Mwanamama aweza kuji-infect peke yake na vijidudu kutoka njia ya haja kubwa eg. kwa mfano wakati anachamba! Kwa hiyo, mke kuwa na PID haina maana kuwa kaambukizwa kwa ngono, ama kuwa na umuhimu wa mme kupima!

Kwa hiyo ni imani yangu hayo maumivu ni kwa ajili ya hiyo PID, ikishatibiwa mambo yatakuwa murua, cha muhimu ni follow up ya karibu, ndio kusema usicheze mbali na aga khan.

Mungu awajaaliye.
 
Asante...well, mie nilikuwa nimeweka possibility tu ya STI/STD na mume kupimwa...kwani infos hapa kidogo hazipo clear kihivyo!! mie bado nipo interested na muhusika kutuambia ni infection gani alokutwa nayo mkewe ili tuweze kutoa mawazo zaidi.

lol...watu wachambe (hasa wa mama) kutoka mbele kuelekea nyuma na si vice versa...

wkend njema.

Heshima mbele kwako (Chinkala) na wengine wote walio changia hapa!

Naona mkuu Chinkala upo interested sana kujua my status, yaani kama na mimi ni similar infection or not! na pia kujua infection aliyonayo mamsapu imetokana na nini?

1. As of now, mimi sina infection yoyote .....nifanyiwa urinalyisis (two weeks ago)
2. PID kwa wife niliambiwa of course ni infection iliyo sababishwa na mkusanyiko mkubwa wa liquid kwenye POD.......nikaambiwa pia tatizo hili ni common kwa wanawake wenye mimba...ndo maana hata likaitwa ''PID IN PREGNANCY. Sikuishia hapo, nilimuuliza Dr. source ya huo mkusanyanyiko wa liquid ambao later umesababisha infection...akaniambia simply.....

''hayo ni matatizo ya wanawake'' akaendelea kusema.....''sababu zinawezakuwa ni nyingi...moja wapo ni logistics (hope has to do with vitambaa, always etc) zao wakati wa breeding'' etc na ofcourse akaniambia kuwa tatizo hilo alikuwa nalo kabla ya kupata ujauzito ila limekuwa speeded up na pregnancy!

Hope mkuu Chinkala, umenipata vilivyo though ushauri wake nitaendelea kuufanyia kazi, cause have nothing to loose!

Cheers
 
@chinkala,
Agreed, yale majibu si ya kitaalam! But the good news ni kwamba lile tatizo limekwisha baada ya wife kutumia Erythromicin kwa siku saba....hasikii maumivu tena!

When a need arises will even PM u man

Cheers!
 
Heshma yenu doctoz na members wote,

Mimi ni mjamzito wa meizi 4 na siku 12, tatizo langu ni kuumwa tumbo mara kwa mara anzia kwenye kitovu kuelekea chini. Nimeshaeleza tatizo langu KCMC wakaniambia nipunzike nisifanye kazi yoyote lakini bado tatizo halijaisha. Wakati mwingine nahisi km nimebanywa na haja kubwa nikienda chooni haitoki na maumivu yanaendelea.

WAPENDWA WANGU NISAIDIENI JAMANI MANA NAOGOPA SANA. MUNGU AWABARIKI.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom