Maumivu ya kiuno na mguu kufa ganzi kwa vipindi

Magehema

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
428
27
Wana JF habarini.

Napata maumivu makali ya kiuno hasa ninapotembea au kusimama kwa muda mrefu na pia nina tatizo la mguu mmoja huwa kama natembelewa na wadudu kwa ndani/kufa ganzi hasa wakati wa usiku na pia asubuhi ninapoamka.

Ni tatizo ambalo nimekuwa nalo kwa muda wa miezi kama miwili na nusu sasa.

Nimepiga xray na kufanya kipimo cha mkojo lakini hapajaonekana tatizo lolote. Ni mfanyaji mazoezi mzuri (kucheza mpira wa miguu) ila sijawahi kuumia mazoezini.

Msaada tafadhali.
 
Matatizo kwenye figo huweza pelekea kiuno kuuma, lakini kama mkojo ulionesha hakuna matatizo basi that means tatizo huenda siyo figo
Sababu nyingine inaweza kuwa ni kufanya kazi za kukaa muda mrefu (kupiga L) daily, na kama hiyo ndiyo source ya tatizo lako, basi inabidi ufanye mazoezi ya kukunja mgongo kwa nyuma na kutumia dawa za kuchua.
Kufa ganzi kwa mguu kuweza kutokana na tatizo lako la kwenye kiuno kwa kuwa mishipa ya fahamu/damu ya miguuni imepitia kiunoni.
Onana na Dr kwa maelezo zaidi

NB: Wengine wanadai ukikwiba mke ya mtu na mwenyewe aking'amua nayo inaweza kuwa source....hehehe
 
Thanks C4All for ur resourceful info, inawezekana ni sababu ya kukaa kwa muda mrefu. Thanks again.
 
Pole sana ndugu Magehema. Maumivu ya kiuno na ganzi miguuni yana sababishwa na tatizo kwenye sehemu ya chini ya mgongo. Hasa pingili za lumbar na sacral za mgongo zinapoungana huwa zinagandamiza baadhi ya mishipa ya fahamu ndo maana huwa unasikia kama wadudu wana kutembelea miguuni au wakati mwingine husikia kama mtu anakuchomachoma na pini. Ni tatizo linalowapata watu wanaonyanyua vitu vizito lakini pia huwapata watu ambao umri umesogea kidogo. Matibabu yake ni mazoezi maalum ya mgongo lakini pia ni vizuri ukaenda MOI kuna wataalamu wazuri wa mgongo.
 
Mganga wa Jadi thanks a lot for ur advice, najitahidi sana kufanya mazoezi ya mgongo, nashukuru Mungu sinyanyui vitu vizito (vyuma/magunia), ingawa nina uziti kiasi, I weigh about 78 kg ingawa ni mfanyaji mzuri wa mazoezi (retired footballer).
 
Habari wapendwa wa JF,

Naombeni uelewa wenu juu ya tatizo linisumbuali.kiuno kinauma upande wa kushoto haswa maeneo ya paja na kiuno.

Tatizo nini wapendwa?
 
Hii nishaielezea kitambo humu.
Tiba yake ni rahisi sana!
Saga tangawizi mbichi na mizizi ya tula tula(ndulele,matula) kisha changanya na asali au mafuta ya nyonyo au mafuta ya kondoo.
Chua kuanzia mgongoni hadi kiunoni na hata huko kwenye paja! Kaa saa zima kisha kaoge na maji ya moto.
Fanya hivyo asbuhi na jioni kwa siku 3 mfululizo.
Usipo pona aisee itakuwa ni ajabu isiyo kweli.
Usisahau kuleta mrejesho hapa usaidie na wengine.
 
hii dawa itaweza kunisaidia mkuu mimi natatizo la kuchomwa chomwa mgongo na ganzi mguu wa kulia
 
Wana JF habarini.

Napata maumivu makali ya kiuno hasa ninapotembea au kusimama kwa muda mrefu na pia nina tatizo la mguu mmoja huwa kama natembelewa na wadudu kwa ndani/kufa ganzi hasa wakati wa usiku na pia asubuhi ninapoamka.

Ni tatizo ambalo nimekuwa nalo kwa muda wa miezi kama miwili na nusu sasa.

Nimepiga xray na kufanya kipimo cha mkojo lakini hapajaonekana tatizo lolote. Ni mfanyaji mazoezi mzuri (kucheza mpira wa miguu) ila sijawahi kuumia mazoezini.

Msaada tafadhali.
mkuu tatizo hili ulipata ufumbuzi? nami natatizo hili
 
Back
Top Bottom