Maumivu kwa wenye magari: Utaratibu mpya wa kulipia road licence, Gharama za fire zaongezwa

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
275
Wana JF, Leo nimestuka na hii kodi mpya kwenye magari. Mbona sikusikia kama chanzo kipya cha mapato ya serikali kwenye bajeti ya mwaka huu?

Leo rafiki yangu kaenda TRA kulipia road licence katika kituo kimoja cha TRA. Alipofika kaambiwa anatakiwa alipie na gharama za ukaguzi wa mtungi wa fire extinguisher kwa gari yenye cc 1500 hadi 2500 ni elfu thelathini (30,000/=). Na utaratibu huu mpya umeanza tarehe 23/07/2012.

Katika utaratibu huo mtu unatakiwa kulipia gharama za ukaguzi TRA halafu ukimaliza kulipa unaenda na risiti na mtungi wako Fire. Ukifika fire unakaguliwa ndipo unapewa stika.

Ninajiuliza, je hiki chanzo kipya cha mapato kimekuja baada ya bajeti au kilikuwepo ila kilijificha kama kile kipengele cha SSRA?
 
ukiona tabu uza gari yako upande toyo..

Acha majibu ya ki-mramba mramba, ni majibu ya kishetani hayafai kuyatoa ikiwa ww ni bin-adam uliyo 'perfect'. Hili suala ni la msingi cz unatoa hiyo 30,000 au 40,000 then haupewi mtungi bali unanunua mwenyewe, so the questions are, What are we paying for? Why is such huge amount like that?
 
ujumbe ni kwamba kama hela yako haijatimia usinunue gari, otherwise unatoa wrong impression kuwa unazo kumbe kabwela tu. duniani kote wene kipato kikubwa ndio wanaolipa kodi kubwa..siitetei serikali lakini ukweli wa mambo ndio huo.
 
Mmh hapa tunakoelekea kutakuwa na gap kubwa kati ya wenye nayo na tusiokuwa nacho. Mbaya zaidi tusiokuwa nacho wengi ni wasomi wazuri
 
Eti wanadai hiyo ni gharama ya ukaguzi you pay in advance na kutokana kwamba wengi walikuwa hawalipii stika za faya wanadhani TRA ndiyo wanaweza kukusanya.

Abdulrahim acha majibu yenye mtazamo hasi na kukatisha tamaa, hata kwa kutumia kiasi kidogo cha pesa mtu anaweza kumiliki gari inayoendana na uwezo wake,
 
t
Tatizo c kulipa hizo 30000,ttz ni je zinatumika kufanyia kazi gani?.usikute zinaishia kwenye posho za safari na vikao visivyo na tija
 
Hapa mwanza sasa paking ni sh 900 gari imeshakuwa anasa na viongozi wanajitahidi kutuminya kila kona,gas,mafuta,umeme
 
Hii niliiona kwenye matangazo ya TRA wakiwa pamoja na watu wa fire, ili kupunguza usumbufu wa ukusanyaji wa mapato. Watu wa fire watakuwa wanachukua asilimia 70 nyingine zinabaki TRA. Kwa zoezi zima wanategemea kupata kiasi cha milioni kumi.
 
ujumbe ni kwamba kama hela yako haijatimia usinunue gari, otherwise unatoa wrong impression kuwa unazo kumbe kabwela tu. duniani kote wene kipato kikubwa ndio wanaolipa kodi kubwa..siitetei serikali lakini ukweli wa mambo ndio huo.

Ni kweli na huo ndo ukweli wenyewe lakini the way ulivyomjibu ndo ameshangaa!!!!! it was simple kumwambia kwa plain language ukiwa na nia ya kufikisha ujumbe wako kama ulivyodhamiria
 
Acha majibu ya ki-mramba mramba, ni majibu ya kishetani hayafai kuyatoa ikiwa ww ni bin-adam uliyo 'perfect'. Hili suala ni la msingi cz unatoa hiyo 30,000 au 40,000 then haupewi mtungi bali unanunua mwenyewe, so the questions are, What are we paying for? Why is such huge amount like that?

kaka bado pia unatakiwa kuwa na "stika ya Geneza"
 
Acha majibu ya ki-mramba mramba, ni majibu ya kishetani hayafai kuyatoa ikiwa ww ni bin-adam uliyo 'perfect'. Hili suala ni la msingi cz unatoa hiyo 30,000 au 40,000 then haupewi mtungi bali unanunua mwenyewe, so the questions are, What are we paying for? Why is such huge amount like that?

Mkuu huyu jamaa siyo kosa lake bali alibemendwa
 
Hata mimi nimekutana na hiyo kodi nikaishia kushangaa....

Tatizo la viongozi wetu ni kwamba wanataka kuishi bila kusumbua akili....Yaani hawakuni vichwa kutafuta vyanzo vingine vya mapato ambavyo kiukweli vipo vingi sana. Badala yake wanaangalia kodi kwa wafanyakazi (PAYE), kodi kwenye vinywaji baridi/bia na magari!
 
Seriously,thz 2oo much!Sticker 30,000 na bora na ukaguz ufanyikie hapo TRA,kupewa nayo itakuwa the other story...!Thz TZ...
 
Back
Top Bottom