Maulamaa wa Kiislamu Denmark waharamisha mashambulizi dhidi ya Wakristo

CPU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
3,863
686
Maulamaa wa Kishia na Kisuni wa Copenhagen nchini Denmark wametoa fatuwa ya pamoja wakiharamisha mashambulizi ya aina yoyote yanayowalenga Wakristo na makundi mengine ya kidini.

Maulamaa hao walioshiriki kwenye mkutano uliofanyika katika mji mkuu wa Denmark wametaka kutolewe adhabu kwa watu wanaohubiri utumiaji mabavu na machafuko kati ya makundi ya kikabila na kidini na kueneza chuki na uhasama baina ya wafuasi wa madhehebu tofauti. Wasomi hao wa kidini pia wameitaka serikali ya Iraq kuliweka suala la kuwalinda Wakristo katika ajenda ya mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu uliopangwa kufanyika mjini Baghdad.

Mkutano huo uliotayarishwa na Denmark ikishirikiana na taasisi ya Uingereza ya Misaada na Suluhu Mashariki ya Kati umehudhuriwa na maulamaa wa Kishia na Kisuni na wanafikra wa Kikristo. Baada ya mkutano huo Kasisi Endrew White wa Kanisa la Kianglikana la Denmark amesema kuwa fatuwa hiyo iliyotolewa na maulamaa na wasomi wa Kishia na Kisuni wakilaani mashambulizi dhidi ya Wakristo inaonesha kwamba vitendo hivyo vya ukatili ni kinyume kabisa na mafundisho ya Qur'an.

Wakati wenzetu wanahubiri mshikamano na amani sisi tunahimiza UHASAMA!!!
 
Hakuna jipya kaka Uislam hauruhusu kumuua acha mtu hata mnyama bila sababu yoyote. Uislam ni dini ya amani tofauti na watu wanavyoichukulia baada ya kulishwa maneno na waamerika na kuzua vita vya "ugaidi" na kuficha ukweli kuwa wanavamia kuchukua utajiri wa mafuta wa nchi za kiarabu.
 
Mimi sio Muislamu ila naipenda sana dini ya Uislamu, hasa nikivaa kanzu na kofia yake baasi najiona ka Mtume fulani hivi. Hii habari nimeiweka hapa makusudi kulinganisha na tamko la 'WAISLAMU' wa Tanzania kuhusu Arusha. Kuna jamaa yangu Muislamu nilipompa highlight za tamko ALIWAKA BALAA MPAKA AKAWATOLEA MATUSI YA NGUONI HAO WALIOJIITA WAISLAMU.
Akasema sio Tamko wa Waislamu bali ni tamko la Wahuni
 
Nimepata CD ya kila kilichojiri Diamond Jubelee siku ya kutoa tamko tafadhali fatilia thread yangu usikie kwa masikio sio wewe umeambiwa then uka missquote ndio maana huyo jamaa yako akautukana uislam, nina wasiwasi na uislamu wake maana Muislam hatakiwi kutukana ila kurekebisha na kutoa nasaha.
 
Kamanda, nilivyomwelewa CPU amesema kwamba jamaa yake aligomba kwa gadhabu na hata kutoa matusi ya nguoni dhidi ya hao waliotoa tamko lile. Hajasema kwamba yule jamaa baada ya kumwonesha tamko alitukana Uislam moja kwa moja. Hebu mwenyewe fikiria, hivi baadhi ya vipengele vya lile tamko kweli (kwa jinsi lilivyotolewa kwa maandishi nasi kulisoma) vinawasilisha kila Muislam na Uislam??!
 
Ulifaa uwe sehemu ya kichwa changu, "SHIKAMOO" kwa ufafanuzi
 
Hakuna jipya kaka Uislam hauruhusu kumuua acha mtu hata mnyama bila sababu yoyote. Uislam ni dini ya amani tofauti na watu wanavyoichukulia baada ya kulishwa maneno na waamerika na kuzua vita vya "ugaidi" na kuficha ukweli kuwa wanavamia kuchukua utajiri wa mafuta wa nchi za kiarabu.

With a reason you can kill!! Nimeipenda hiyo
 
Back
Top Bottom