Maudhui ya shairi la wanafunzi yamchefua DC

Ukweli woote tunaujua na tunajua kuwa shule za kata bado duni saana,
Tunajua hakuna walimu
Hakuna madawati
Hakuna maabara
Umeme hakuna
Hakuna computer japo 1 tu
Hakuna maktaba
Hakuna Vitabu
kwa hiyo ni kweli kuwa ni shule za walala hoi ukizingatia watoto wao hawasomi shule hizo
Ilikuwa haki watoto kuandika yooote hayo, hakuna haja ya kuwa mkali.
Kama Baba tafuta njia yakuyakabili hayo.
 
mKuu wa wilaya hajajibu swali. Yeye akiulizwa maswali magumu anasingizia siasa.
Sijui huu mchezo utaisha lini.
Halafu huyu kima anasema ana degree mbili wakati haweza hata ku-calculate percentage kutoka shule 4 mpaka 22 ni 22/4=5.5 which is 550% Hawa ndo tunawaita vilaza! Shule ni walimu na vifaa, hatujakataa shule zimejengwa lakini kama hamna vitabu, vifaa wala walimu ni kupotezea watu mida.
Poleni sana wanafunzi mnaokabiliana na yeboyebo, changamoto yenu kubwa ni kuwang'oa mafisadi, kuweni chachu ya mabadiliko kwa kuelewesha jamii inayowazunguka.
 
Walimu nao wanakimbia kufundisha mwalimu anapangiwa shule mshahara anapata kwa mbinde eti jina halijaingia kwenye computer wanaamua kukacha kufundisha.
ndo hapo sasa, miezi 6 mtu huna mshahara na uko bush! bado tuna safari ndefu sana aiseee!
 
naweza kupata hilo shairi? kwa kweli hawa watoto juu zaidi. niliwai kuandika hapa shule za kata zinawawapotezea watoto wenye vipaji muda. badala ya kuja pugu, mazengo au tosamaganga wanabaki huko wakifundishwa na mtendaji wa kijiji. nchi inaelekea wapi? watu mahiri hupatikana toka vijijini na siyo mjini
 
HUYU DCALIACHA BRAINS ZAKE NYUMBANI. ANATAKA SANA HIO KAZI YA KUHUTUBIA:glasses-nerdy:NA NDIO MAANA ANAKASIRIKA:mad2:,
IMAGINE WITH TWO DEGREES AND REASONING NDIO HII KWA KWELI ..... I THINK AND AGREE YOU NEED THE THIRD AND FOURTH AND YOU WILL STILL THINK SHULE KUA NYINGI NDIO ELIMU BORA, WHAT IS WRONG :confused2: .................. :playball:
 
Hivi vi-DC uchwara ndiyo vina matatizo sana. Kazi kujikombakomba kuwalinda wakubwa zake. Alitaka serikali ipewe sifa hata ambapo hapastahili. Kuambiwa ukweli wanaona ni matusi, maana ya ke huyu hataki kukosolewa ili ajisahihishe, anatufaa huyu kweli? naona 31 october mbali mno.
 
"Mchapakazi
Re: Maudhui ya shairi la wanafunzi yamchefua DC
mKuu wa wilaya hajajibu swali. Yeye akiulizwa maswali magumu anasingizia siasa.
Sijui huu mchezo utaisha lini.
Halafu huyu kima anasema ana degree mbili wakati haweza hata ku-calculate percentage kutoka shule 4 mpaka 22 ni 22/4=5.5 which is 550% Hawa ndo tunawaita vilaza! Shule ni walimu na vifaa, hatujakataa shule zimejengwa lakini kama hamna vitabu, vifaa wala walimu ni kupotezea watu mida.
Poleni sana wanafunzi mnaokabiliana na yeboyebo, changamoto yenu kubwa ni kuwang'oa mafisadi, kuweni chachu ya mabadiliko kwa kuelewesha jamii inayowazunguka."
Mchapakazi, ukiachilia mapungufu mengine ya wazi kumhusu huyu DC, kimahesabu yuko sahihi. Kutoka shule 4 hadi 22 kujua ongezeko lake kiasilimia ni sawa na:-
(22-4)/4*100=450%.
Hata hivyo hili sio jambo la kujivunia hata kidogo kwa sababu wanachoambulia huko shuleni ni sifuri. Na kwa kweli wako busy kudandia magari ya mchanga asubuhi na jioni wakionekana wanaenda na kurudi shuleni, lakini mwisho wa siku wanakuwa wameshafikia umri wa kuoa/kuolewa, na maisha yanaendelea.
 
Ukweli woote tunaujua na tunajua kuwa shule za kata bado duni saana,
Tunajua hakuna walimu
Hakuna madawati
Hakuna maabara
Umeme hakuna
Hakuna computer japo 1 tu
Hakuna maktaba
Hakuna Vitabu
kwa hiyo ni kweli kuwa ni shule za walala hoi ukizingatia watoto wao hawasomi shule hizo
Ilikuwa haki watoto kuandika yooote hayo, hakuna haja ya kuwa mkali.
Kama Baba tafuta njia yakuyakabili hayo.



HAZITAKI KURA ZENU

Hazitaki amesema, kwa hakika hazitaki,
Mbona mna muandama, kwa kisa kile na hiki,
Kikwete mtu mzima, na wala msihamaki,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Pendo kitu cha hiari, hakina lazima katu,
Ni vema kujihadhari, msizidi kuthubutu,
Si kwa kero nazo shari, mumwache mwana wa watu,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Mapenzi kweli maua, huweza ota popote,
Bali huhitaji nia, kuyahudumia yote,
Bila maji kumwagia, Hunyauka kwa vyovyote,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Wafanyakazi hataki, mwataka nini zaidi?
Msitumie mikiki, hali mu watu weledi,
Binadamu ana haki, kupima na kukaidi,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Mbona hamna simile, huria kumuachia,
Mmeng'ang'ana na lile, hamtaki kusikia,
M-bembeleze milele, hataki kawaambia,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Mmejawa na hiana, kwa jibu alilotoa,
Kawaeleza bayana, wazi amewaambia,
Mwalitafuta laana, msilolitarajia,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Kwa uvumba na ubani, kesha sema hazitaki,
Zaidi mwataka nini, awaeleze rafiki?
Tulia mkae chini, muwaze na kuhakiki,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Hazitaki kakataa, kura zenu kasusia,
Japo mlete gitaa, na nyimbo kumuimbia,
Mumtembeze mitaa, kwa manoti mia mia,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Hazitaki si ajabu, kura zisizo na soko,
Msiitafute tabu, kujipendekeza mwiko,
Bure mwajipa aibu, kwa kumpa mialiko,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.


Kaditamati shairi, kura zenu hazitaki,
Kila kitu ni hiari, shuruti haina haki,
Kuchagua ni fahari, lazima haipendeki,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.
 
kutoka shule 4 hadi 22! ongezeko la 450% na walimu wameongezwa %ngapi? si ni siasa hizo!

Nakumbuka mama 6 wakati waziri wa elimu alikuwa anachakata kupata walimu wa fasta fasta sijui aliishia wapi
 
shule za kata wamejengewa masikini, watoto wa wakubwa hawaonekani, maisha mitaani magumu, wanafunzi wanafeli, nyumba za kupanga, wengi wanakatisha masomo yao, wazazi wengi masikini, hakuna walimu tabu nyingi wanapata mitaani, wazazi hawana uwezo wanategemea mashamba. Serikali itupe suluhisho la matatizo haya
hiki ndicho kizazi kitakacho kuja kulia juu ya makaburi ya Kikwete , Makamba, na mafisadi wao.
 
If all the rich people should send their children to the public schools they would feel bound to concentrate their money on improving these schools until they met the highest ideals
 
Back
Top Bottom