Mauaji ya Profesa Jwani Mwaikusa: Kesi ni geresha tu?

Unajua kilichonisukuma kuandika thredi hii ni baada ya kusoma thredi moja kwenye jukwaa hili kuhusu ile kesi ya babu sea, sina uhakika lakini naona kama kesi yao ilikwenda haraka sana kulinganisha na hii, naomba mdau anayefahamu ile kesi ya wakina babu seya ilitumia muda gani atujuze, au hawa wakubwa wanapanga kulingana na matakwa yao?
Kesi ya babu seya ilichukua zaid ya mwaka mmoja! Labda uchunguzi haujakamilika!
 
Kesi ya babu seya ilichukua zaid ya mwaka mmoja! Labda uchunguzi haujakamilika!
asante mkuu, basi tuwe wapole na imani kwa serikali yetu labda tutajua ukweli, kwenye hili nadhani kufahamu fika ni nini kilitokea ndio muhimu zaidi
 
Hivi mdau, kuna uwezekano mtu mwenye umuhimu kwa serikali kama alivyokuwa prof mwaikusa akauwawa na serikali ya nchi jirani bila ya serikali yetu kupitia vyombo vyake vya usalama kupata fununu?
Mkuu Bongisa, kwani huko Usalama Wa Taifa unafikiri Wanyarwanda hawapo? Kwa taarifa yako Wanyarwanda wako kwenye taasisi zote nyeti ikiwepo Ikulu. Na Usalama Wa Taifa Wa sasa hivi usije ukaulinganisha na ule uliokuwepo wakati wa Baba wa Taifa yaani Aline marehemu Mzena na marehemu mzee Gama. Na do not be surprised ukisikia contract killers wamekuwa hired through ofisi hizo zinazopaswa kulinda usalama wa nchi.
 
Jana nilikuwa kunduchi salasala kwenye kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha profesa Jwani Mwaikusa aliyeuawa kwa kupigwa risasi katika mazingira ya kutatanisha nyumbani kwake kama mnakumbuka wadau.

Katika maongezi ya hapa na pale nikapata kuambiwa kuna watuhumiwa walikamatwa wamewekwa ndani, na kesi inaendelea.

Cha kushangaza tokea wakamatwe na kesi kuanza sasa ni mwaka mmoja, hiyo kesi hata mahakama kuu haijafika, bado ipo Kisutu kwa hivyo inatajwa na kuahirishwa tu hata kusikilizwa bado haijaanza kwani kesi za mauaji husikilizwa mahakama kuu.

Hii ina maana upelelezi bado haujakamilika sijui, hivi katika mazingira haya kuna haki kweli au maigizo?

Na sababu ya mauaji yale mpaka leo ni giza nene kwa mujibu wa wanafamilia.

Wadau hebu tuchangie mawazo kwenye hili.
Yametimia !
 
Sasa ndugu unataka tuchangie nini?

Wajua kifo hiki kinasikitisha sana, wewe mtu wa karibu wa familia na kama memba wa JF tupe in black and white kile ambacho wanafamilia wanasema juu ya chanzo cha kifo cha prof, hii itasaidia kwa baadhi ya watanzania kuepuka vifo vya aina hii where possible.

Pili tueleze ni kipi hasa kinachoendelea juu ya uendeshaji wa kesi ili members wazoefu watupe uzoefu wao bcos huenda mwenendo wa kesi niwa kawaida.

Na mwisho tetesi za vijiweni zinasema kuwa prof aliponzwa na utashi wake wa kukataa uhuni na ubabaishaji ulioko kwenye uendeshaji wa mahakama ya ICTR hivyo Rais wa Rwanda akaona atakuwa amevuliwa nguo- akaamua kumu.......................

Mwenye ukweki atujuze.
Sasa wameachiwa huru!! Mushen yao imeisha na Mwaikusa hayupo duniani! Bado Mungu yupo na anaona
 
Profesa Juani Mwaikusa alikuwa eliminated na nguvu za Paul Kagame ambazo tumeona zikivuka mipaka ya Rwanda na kuwafuata watu huko huko waliko kama akina Generali Kayumba aliye nusurika kufa baada ya kupambana na paid assassins.

Jiulize: Kwanini Profesa mwingine wa USA alivyokataa kuja Kigali kumwakilisha mteja wake kwa kuogopa kupatwa na yaliyompata Profesa Mwaikusa.

Fuata link hii Wakili Peter Erlinder na kifo cha Prof Juani Mwaikusa - JamiiForums
Panaweza kuwa sawa hapa ndo uzur wa jf ikitumika vizur na watawala watapa mahali pa kuanzia shida wanaipiga vita kwa kuwa haichagui wa kumulika
 
Jana nilikuwa kunduchi salasala kwenye kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha profesa Jwani Mwaikusa aliyeuawa kwa kupigwa risasi katika mazingira ya kutatanisha nyumbani kwake kama mnakumbuka wadau.

Katika maongezi ya hapa na pale nikapata kuambiwa kuna watuhumiwa walikamatwa wamewekwa ndani, na kesi inaendelea.

Cha kushangaza tokea wakamatwe na kesi kuanza sasa ni mwaka mmoja, hiyo kesi hata mahakama kuu haijafika, bado ipo Kisutu kwa hivyo inatajwa na kuahirishwa tu hata kusikilizwa bado haijaanza kwani kesi za mauaji husikilizwa mahakama kuu.

Hii ina maana upelelezi bado haujakamilika sijui, hivi katika mazingira haya kuna haki kweli au maigizo?

Na sababu ya mauaji yale mpaka leo ni giza nene kwa mujibu wa wanafamilia.

Wadau hebu tuchangie mawazo kwenye hili.
Wafukua makaburi
 
Back
Top Bottom