Mauaji ya polisi yakimbiza wanaume kijijini

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
MSAKO mkali wa wahusika wa mauaji ya askari Polisi yaliyotokea katikati ya wiki katika Kijiji cha Mwakashanhala, Kata ya Puge wilayani Nzega, yamewalazimu wanaume wakazi wa kijiji hicho kuyahama makazi yao na kuwaacha wanawake, watoto na mifugo. Imeelezwa kwamba, tangu kuuawa kwa askari PC Joseph aliyekuwa na namba za usajili E 9530 aliyekuwa katika msako wa watu wanaojihusisha na kilimo cha bangi, ni nadra kumuona mwanamume kijijini hapo.

Mbali ya kumuua kwa mapanga PC Joseph, walimjeruhi vibaya askari mwingine, Juma Hussen mwenye namba G246 ambaye amelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Ndala anakotibiwa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora anayeongoza msako huo akiwa na kundi la askari zaidi ya 60, amethibitisha wanaume wa kijiji hicho kuyahama makazi yao.

Kamanda Barlow ameliambia gazeti hili kwamba, walikwenda kijijini hapo na kushindwa kufanikisha azma ya kuwakamata watuhumiwa kutokana na kuelezwa na wake zao kuwa, wanaume wamekimbilia msituni kwa hofu ya kukamatwa. Hata hivyo, Kamanda Barlow aliwataka wananchi waliokimbia makazi yao kurudi majumbani mwao huku akisisitiza wanayemsaka ni Jiliwa Mpelema na kwamba wakirudi watalirahisishia Jeshi la Polisi kupata maelezo ya kina kuhusu sakata hilo kwa ujumla.

"Ninachowaomba wananchi warudi majumbani mwao wasikimbie makazi yao, Jeshi la Polisi halina ugomvi nao hata kidogo," alisema na kuongeza; “Kama tu wananchi watarudi tutaweza kupata taarifa sahihi ya chanzo cha tukio hilo ili tubaini nina wamehusika na nani hajahusika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake," alisema Kamanda Barlow.

Mauaji ya askari huyo yalitokea Aprili 20 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi, baada ya wananchi wa Kijiji cha Mwakashanhala kuwashambulia polisi wawili na kumuua mmoja wakati walipokwenda kijijini hapo kufanya msako wa walima bangi.
Askari aliyeuawa amezikwa jana huko Kilanda, Nkasi katika Mkoa mpya wa Katavi ambapo imeelezwa kwamba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema aliongoza mazishi hayo.

HabariLeo
 
hili jambo halileti picha nzuri kabisa kwani inaonekana kama vile wananchi wenyewe wana-support kilimo cha bangi aidha kwasababu ndo kinawalisha au wanajaribu kuji-protect ....kwa kweli haipendezi hata kidogo....je,tutafika kama polisi wanaosaka wakulima wa bangi wanapigwa na wananchi ambao hao polisi wanawa-protect?:angry:
 
hili jambo halileti picha nzuri kabisa kwani inaonekana kama vile wananchi wenyewe wana-support kilimo cha bangi aidha kwasababu ndo kinawalisha au wanajaribu kuji-protect ....kwa kweli haipendezi hata kidogo....je,tutafika kama polisi wanaosaka wakulima wa bangi wanapigwa na wananchi ambao hao polisi wanawa-protect?:angry:

Haya mambo ni matokeo ya mfumo mbovu wa ulinzi hasa wa jeshi la polisi, inafkia muda wananchi wanakosa imani na jeshi hilo-kutokana na vitendo vya askari wao kuwadhaau nakuwatenda vibaya wananchi. Vitendo kama vya bulyankuru na tulawaka ni unyanyasaji unaojenga chuki kubwa. Kama mfumo wa jeshi utaendelea kuwa wa kulindana na askari wahalifu kutiwa kiburi na kutowajibishwa hasira za wananchi zitazidi kujidhihirisha.
 
Back
Top Bottom