Mauaji ya Nyamongo: CCM wawaunga mkono Chadema

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
Wenyeviti wa vijiji vitatu vilivyopo Kata ya Nyamongo, wilayani Tarime wametua jijini Dar es Salaam na kueleza wanaunga mkono viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutetea haki za wananchi wa eneo hilo. Wakizungumza katika kikao cha pamoja na wananchi wa Nyamongo wanaoishi jijini Dar es Salaam juzi, Wenyeviti hao Elisha Marwa wa kijiji cha Nyangoto (CCM), Tanzania Omtima wa Kewenja (Chadema) na Otembe Nyamhanga (CCM), walisema kudai haki hakuna itikadi ya vyama, hivyo wanaungana na Chadema katika kusimamia katika kufungua kesi dhidi ya Jeshi la polisi kwa kufanya mauaji ya watu wanne.
Hivi karibuni watu wanne walikufa kwa kupigwa risasi na Polisi kwa kile kinachodaiwa kuvamia Mgodi wa North Mara Gold Mining unaomilikiwa na Kampuni ya African Barick Gold kwa nia ya kutaka kuiba mchanga wenye dhahabu.

Katika Kikao hicho kilichowakutanisha na wanachama wa Wananchi wa Nyamongo wanaoishi jijini hapo (Nyada), Mwenyekiti wa kikao hicho Elisha Marwa, alisema kimsingi chanzo cha mauaji ya watu hayo hayakutokana na uchochezi wa kisiasa bali ni kutokana na wananchi kuchoshwa na hali ngumu ya maisha. Marwa alisema chimbuko la mgogoro ni wamiliki wa Mgodi kukiuka mkataba waliowekeana baina yao na vijiji hivyo, ambapo ulielezea mgodi huo utawajibika kurudisha asilimia moja ya mapato kwa kupitia mfuko wa dhamana kwa kila kijiji kwa ajili ya maendeleo. Alisema mkataba huo pia uliweka wazi kwamba mgodi pia ungewajibika kusaidia wachimbaji wadogowadogo kwa kuwatengea eneo pamoja na kuwasaidia nyezo bora za uchimbaji.

Hata hivyo, mgodi huo baada ya kuanza kazi hawakutekeleza mkataba huo na badala yake wananchi wa vijiji vitano vinavyozunguka mgodi huo, Kewanja, Nyamwaga, Kerende, Ngekuru na Nyagoto wamezidi kuwa na hali ngumu baada ya kuzuiwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo biashara na uchimbaji mdogomdogo.

Marwa alisema wao kama viongozi wa vijiji walijaribu kufuatilia utekelezaji wa mradi lakini walikatishwa tamaa baada ya kutakiwa kuchukua dola za Marekani 100,000 kwa masharti ya kufutwa kwa mkataba wa awali. Mwenyekiti wa Kewanja, Tanzania Ontima, alisema vurugu zilizotokea baada ya mauaji hayo, zilisababishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele kukataa kuwasikiliza na kuwafukuza ofisini kwake walipoenda kumtaarifu juu ya mauaji hayo.
Alisema kimsingi kama Tarime inatakia kuwa tulivu lazima Rais afikirie upya juu ya Mkuu huyo wa Wilaya akieleza anafanya kazi kwa ubabe bila kuwasikiliza wananchi.

Naye Otembe Nyamhanga (CCM), alisema kuja kwao kuonana na wananchi hao ni kutafuta namna ya kusaidia familia zilizoathirika kwa kufiwa na ndugu zao pamoja na kudai haki za Wananyamongo.
 
Hata wanaCCM wameanza kuamka na kuona kazi nzuri ya viongozi na wabunge wa Chama cha Chadema na kuanza kujenga hoja ya kuwatetea
 
wana 'magamba' CCM ambao wanapinga harakati za kutetea haki za wananchi na kupinga harakati za kudai haki wengi wao ni mamluki. Na kama sio mamluki basi ni wale wale ambao hajui kwamba TANU ilileta uhuru na CCM ya baada ya Mwl.Nyerere imeleta ushuru.
 
Back
Top Bottom