Mauaji ya Morogoro, Iringa, Chadema hawawezi kukwepa lawama

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wana JF,
Hivi karibuni katika miji ya Morogoro na Iringa iligeuka uwanja wa mapambano baina ya wafuasi wa Chadema na askari wa jeshi la polisi na kusababisha mauwaji ya raia wawili Ally Nzona alifariki Morogoro na Mwandishi wa habari Daudi Mwangosi alifariki Iringa.

Jeshi la polisi lilizuia maandamano na mikutano kwa msingi kwamba siku hizo kutakuwa na zoezi la sensa nchini kote na kwamba muda huo wa mchana miji hiyo itakuwa na pilipilika nyingi, jeshi la polisi likataa kuruhusu kufanyika kwa mikutano na maandano.

Katika akili ya kawaida Chadema kilifanya makosa kwa kufanya maandamano kwa nguvu licha ya kupigwa marufuku, ili polisi waingilie kati kuwatawanya hivyo damu imwagigike waituhumu serikali kuwa inawanyima uhuru, tumeona mauji ya makusudi yanayosabishwa na ukaidi na ukaidi na tabia ya kutotaka kufauata sheria kwa viongozi hawa wa Chadema ili wapate sababu ya kuilaumu serikali.

Tunaamini kuwa bila Chadema kuandamana kibabe? Ni dhahiri kuwa kusingekuwa na mauji ukaidi wa makusudi wa Chadema dhidi ya jeshi la polisi ili damu imwagike si wa mara ya kwanza ulishawahi kutokea Arusha watu watatu walifariki dunia.
 
Hebu nisaidie, ni nini hasa ambacho kinaweza kuniconvice nitupie lawama zangu kwa cdm????
 
"Tunaamini kuwa bila Chadema kuandamana kibabe? Ni dhahiri kuwa kusingekuwa na mauji ukaidi wa makusudi wa Chadema dhidi ya jeshi la polisi ili damu imwagike si wa mara ya kwanza ulishawahi kutokea Arusha watu watatu walifariki dunia."

Baada ya kufikiria, ukawaza, ukafikiria tena ndio ukaamua kuja hapa jamvini na hili hitimisho...kweli nimeanini kuna watu huwa wanawaza na wengine huwa wanafikiria
 
wee kweli mchuzi wa bata tena ule usio na ndimu, shombo kibao
 
Sio bure utakuwa umetumwa wewe,kusoma hujui hata picha huioni? Kwa ishu ya Iringa polisi wanalao muulize Kamuhanda atakuambia,waambie waliokutuma itabidi waagize risasi na mabomu ya machozi ya kutosha ndio tumeshaamka hatulali tena. M 4 C for all.
 
Siasa za maji ya chooni zinaigharimu ccm.
Tanzania ya leo sio ya mwaka 47.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
mi ninavyo fahamu siku hiyo walikuwa kwenye ofisi zao na pia polisi ndio chanzo cha hizo fujo zote bila wao yasingetokea hayo yaliyotokea.
Tufanye siku moja wajaribu kuruhusu waandamane bila polisi escort tuone kama fujo itatokea.
 
naamini mleta mada hajamaanisha haya aliyoyaleta. kama alimaanisha naye atakuwa ana matatizo makubwa ya kufikiri au atakuwa muwazaji mzuri sana.
 
Back
Top Bottom