Mauaji ya mfanyakazi TRA Tarakea

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,481
1,364
Wiki hii huko huku Rombo TRA wamekua wakipita katika masoko kutokana na siku za masoko zilivyopangwa na wamekua wakikagua magari na pikipiki ambazo bado hazijalipiwa pamoja na leseni ambapo wamekua na gari pamoja na polis mmoja ambae amevalia vazi la kipolice pamoja na bunduki huku wenzake wa TRA wakiwa wamevalia kiraia na pindi wanapokamata pikipiki wamekua wakizitumia kuzunguka nazo kwaajili yakusaka pikipiki nyingine na pindi wanavyokamata huvamia mtu bila kujua ni watu gani kwavile hawajavalia mavazi rasmi na huwa hawajitambulishi kwanza ndipo wakague na baada yakuendelea na utaratibu huo kwa masoko kadhaa kwa wiki hii hapojana alipigwa mmoja wao na kujeruhi vibaya na kupelekwa hospital akiwa na hali mbaya na kuripotewa kupoteza maisha yake na police leo hii ndio wanajikusanya kutoka vituo tofauti ili kufuatilia suala hili.<br />
Yafaa TRA kutumia njia ambayo haimpi shaka mwenye mali kama kujitambulisha kabla ya kukagua. Mwenyekujua zaidi kuhusu suala hili atujuze.<br />
<br />
Nawakilisha
 
Pole zao. Wajue tu hamna mwenye hasira kama mtu aliye na njaa. Sasa sometimes unakuta wale manyoka wa bodaboda na ugumu huu wa maisha, hajaweka kitu mdomoni, then unamvamia kienyejienyeji... wanategemea nini...
 
Back
Top Bottom