dm2000inter
Member
- Oct 27, 2010
- 29
- 10
Naandika mwili ukitetemeka baada ya kushuhudia miili minne ya marehemu. Jamaa mmoja wa Mamba kokirie Moshi Vijijini,Macmilan Msami (49) amemchinja mama yake mzazi kama kuku kwa kutumia panga. Hakuishia hapo akawaendea watoto wake wawili Emanuel (9) na Ezekiel (12) akawachinja kwa tyle hiyo hiyo. Kisha akazikusanya maiti katika chumba kimoja akapiga usingizi hadi asubuhi. Dada yake alipofika akamkuta amekaa mlangoni anamuuliza vipi mama yupo akamjibu we ingia ndani ujionee mwenyewe. My God! ni maiti ndani ya madimbwi ya damu. Tukio hili si hadithi wala usifikiri unaota la hasha limetokea jana saa 2:00-4:00 usiku. Maiti zipo Kilema Hospital. Kibaya zaidi Wananchi wenye hasira kali nao wakamkamata jamaa wakamchinja na kuchoma moto mwili wake. Kafa na siri yake moyoni ya kiini cha kutekeleza unyama huu. Mungu aziweke roho za marehemu(si na ya muuaji) mahali pema peponi,Amen.