Mauaji ya Daud Mwangosi: Mkurugenzi wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Aongea...

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
1.jpg



( Huu ni mchango wa Bw. Karsan kwenye Facebook ya Mjengwa)

Watanzania wenzangu, nachukua fursa hii kuwajulisheni kuwa sisi viongozi wa UTPC, tunakichukulia kitendo hiki katika daraja ya aina yake na katu hatutanyamaza kama baadhi watu wanavyodhani.

Hili ni shambulio la kwanza katika historia ya tasnia
ya habari Tanzania ambapo mwandishi wa habari anakufa mikononi mwa maafisa wa umma, anauawa akiwa kazini.

Sasa kwanza tumemtuma Rais wetu Kenneth Simbaya aende huko kulikotokea tukio hili na kufanya uchunguzi ambao utatupa picha kamili na ataileta taarifa hiyo kwenye kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa UTPC kitakachofanyika trh 5 Septemba.

Kwenye kikao hicho tutatoa msimamo juu ya jambo hili. Kwa sasa nnawaomba Wastanzania wenzangu,waandishi wenzangu tutulie, lakini nawaambia Hamkani si shwari tena.


Wakatabahu,
Abubakar Karsan
Mkurugenzi Mtendaji
Union of Tanzania Press Club
 
Hamkani si shwari tena tena, No Longer At Easy agree with you! hiyo kesho kutwa tutausikia huo msimama!
 
Tuko nyuma yenu.
Full support..

TUZIDISHE MAOMBI NA SALA.
 
Tumewasikia ndugu wana UTPC. Wasiwasi wetu rupia inaweza kupenyezwa na ikawa ndio mwisho wa jambo hili.

Ila ninachukua wasaa huu kuwaasa ndugu wana habari, hususani viongozi wa UTPC, kama jambo hili hamtalichukulia kwa uzito wake au mkaruhusu rupia kuwapumbaza basi dhambi yake itawatafuna ninyi, vizazi vyenu pamoja na taaluma yote kwa ujumla.

Tuko nyuma yenu na tunategemea muongozo wenu katika kuhakikisha damu ya wanataaluma kama ninyi hamwagiki katika mazingira ya kipumbavu kama haya ya kulinda serikali dhaifu na viongozi dhaifu.

An Injury To All Should Reflect An Injury To All......
 
tunaomba huyo Rais wa waandishi asikubali kuwekwa sawa na serikali hii iliyowaweka sawa akina Ulimboka na Mwakyembe,naunga mkono hoja kwa mashaka makubwa
 
Waaamndishi mlianza kubanwa kwa kufungiwa kwa mwanahalis na sasa wanaanza kuwafumua mabomu na risasi.....polisi sio wabaya wabaya ni ccm na vioongozi wake wa serekali,,msiandike mazuri ya serekali sasa andikeni mabaya na maovu ya ccm maana imeshindwa kuwa tendea haki......virushwa vidogo vidogo vitawaumiza kuweni kama marehemu mwangosi.
 
Kwakweli mimi naomba niwashauri tu waandishi wa habari kwamba jambo kubwa ni kuelimisha watu nakuwapa mbinu mbadala ikiwa ni pamoja na wananchi wote kutoogopa kifo kwa kuhofia hawa wanyama wanaoua watu wenzao kirahisi namna hii..Waelezeni watu kwamba nchi haina serikali ila genge la vibaka na wauaji chini ya Jakaya Kikwete na damu inayomwagika haitazuilika kwa kukimbia mikutano bali kwa kuandamana na kupambana na genge hili mpaka mtanzania wa mwisho atakapodondoka au wao watakapo ikimbia nchi watuachie ardhi yetu na uhai wetu wenye thamani na sio kutuwinda kama wanyama pori!!!
 
Tumeshuhudia waandishi wa habari wengi wakinunulika na vyombo vingi vya habari vikitumika kinyume na maadili ya uandishi. Labda kwa tukio hili mtakuwa wamoja katika kutetea hakijaharibika zenu na kututendea haki sisi wananchi kwa kupata habari sahihi. Tunasikitika na kulaani udhalimu huu unaoendelea kutendeka katika nchi inayokaririwa kuwa ni kisiwa cha amani.
 
Waandishi mlipotoka pale Mwana halisi lilipofungiwa na mkakaa kimya....basi tusahau yaliyopita tujipange tena. Tumepata nafasi hii ya kupigania haki yetu, asiwepo wa kubaki nyuma. Tunao ushahidi wa maneno na picha na vitendo. Damu ile itakumbukwa
 
Enough is enough!!! We need solution only! Kulalamika inatosha! naomba nieleweke nikisema hivi simaanishi Vita ndio only solution iliyobaki bali shinikizo kwa njia ya amani dunia ijue Tanzania tuna tatizo kubwa na vyombo vya dola.
 
Natoa rai susieni kuandika habari za polisi kwa mwaka mmoja mpaka watakapo jirekebisha.
 
Susieni habari za polisi na ccm ili ziwe zinaandikwa na gazeti la uhuru!!!!!!!!
 
Nafikiri umefika wakati vyombo vya usalama virudi nyuma na kufikiria wanafanya haya kwa maslahi ya nani? Na je hao wanaowatuma watakuwepo madarakani milele? Nionavyo mimi raia wa hali ya chini wamechoka na vyombo hivi vya usalama
 
Kwa kila mpenda haki, bila kujali dini wala itikadi ya vyama, hakuna mtu atakayeunga mkono unyama huu. walipo uwawa watu katika machafuko huko Arusha,, tuliomba iwe fundisho kwa vyombo vya dola, na tukadhani watajifunza, na kufanya tukio hilo kuwa la kwanza na la mwisho, yakatokea mauaji Igunga, tukasisitiza iwe mwisho, Ikaja Juzi kauliwa Ally zona, tukaomba iwe mwisho, sasa leo Iringa, na mbaya zaidi, mtu akiwa mikononi mwa vyombo tunavyodhani eti ni vya usalama. Sasa katika hili, tumechoka kuona ndugu zetu wanauwawa na vyombo vya dola. Tunaomba Tamko, toka kwa mkuu wa kaya, likiwa na hatua ambazo tayari zimechukuliwa kuhakikisha unyama huu unakomeshwa, vinginevyo, imani kwa vyombo vya dola, pamoja na kwa serikali, itatoweka.
 
Back
Top Bottom