Mauaji ya Bulyanhulu yaleta Debate kali Norway

Nyangumi

JF-Expert Member
Jan 4, 2007
507
17
Kuna debate kali inayoendelea hivi sasa ndani ya bunge la Norway kutokana na serikali ya Nchi hiyo kuwekeza kiasi cha US $235.3 million kwenye kampuni ya Barick huko Bulyang'ulu. Pesa hizo ambazo ni mfuko wa pension nchini humo, umesababisha kinyaa miongoni mwa wananchi baada ya kutambua kuwa wananeemeka na "BLOOD GOLDMINE". Kwa maana ingine wananeemeka baada ya vifo vya Watanzania Masikini na wengine kupoteza nyumba na mali zao. waliofukiwa katika mashimo ili Serikali ya CCM iweze kutoa ardhi hiyo kwa Barrick

Nitawaunganishia video hizo muda si mrefu
 
Unajua kweli kuna wazungu wa aina nyingi..the same goes to one of my law professors..mwanamke anafuatilia wapi pension fund yake inainvest..akiona noma anachomoa...yani inaonyesha, the two different worlds we live in!!

Hivi bongo tunajua NSSF na wenginewo wanainvest vp hizo hela?? Lol
 
Serikali ya Norwey yaambiwa iishinikize hiyo kampuni ya Barrick kulipa compesation kwa wote waliodhurika la sivyo iuze shea hizo mara moja.
 
tunashukuru sana kwa taarifa hii muhimu,lakini sijui tz kama itawafikia wadanganyika au vyombo vyetu vya habari ili isambazwe kwa walengwa
 
Pinda,
Na huku unatuambiaje........any kifutia machozi kwa waliofiwa?.............mchezo wa kuwasaidia TRL uliouanzisha......tunautaka na huku pia
 
Mwaka huu sijui kama kuna pa kutokea.....lazima uongo wao wote utadhihirika.

Wakati akina Tindu Lisu wakati wanaongea walikuwa wanasema ukweli, ila serikali ikapinga kama kawaida yake ya kutetea wazungu na wahindi.
 
Ukiangalia kwa makini hizi video na hasa wawakilishi wa serikali utagundua matatizo tuliyonayo waafrika. Yaani hatuna hata aibu tunavyoonyesha ujinga wetu.Waafrika kwa ujinga wetu tuko tayari kuwaua waafrika wenzetu, kutetea wizi.Barrick hawalipi kodi pamoja na bei kubwa ya dhahabu!!(kuwa balance sheet yao inaonyesha hasara ndo maana hawalipi kodi)ili tumfurahishe mtu mweupe,Mgeni.Upumbavu huu huwezi kuukuta kwa wenzetu. Hawako tayari kufanya upumbavu ili kumnufaisha mgeni,achilia mbali kuwa mweusi.
Yaani ukisikiliza hata hili swali analoulizwa huyo bwana wa wizara ya Madini, utagundua kuwa huyo mwandishi ndani ya kichwa chake alikuwa anamwambia kuwa "hivi nyie ni wajinga kiasi gani,kiasi cha kushindwa kujua kuwa hapa mnaibiwa"
 
CCM kila siku wanakataa juu ya haya mauaji lakini pia hawatakai kuchunguza .Je hawa wananchi nao ni waongo au mimi ndiye sijaelewa kitu hapa ?
 
CCM kila siku wanakataa juu ya haya mauaji lakini pia hawatakai kuchunguza .Je hawa wananchi nao ni waongo au mimi ndiye sijaelewa kitu hapa ?

Sijakuelewa hapa,unaseme CCM hawakatai kuchunguza? CCM walisha kataa kuchunguza. Waliambiwa kama wao wanasema hakuna watu waliofukiwa hai basi watoe ruhusa mashimo yafukuliwe kuangalia kama hakuta kuwa na watu. Sasa kama CCM inauhakika, kwa nini isiruhusu mashimo yafukuliwe
 
Mie nafikiri hili suala tunaweza kwa mara nyingine kuikalia shingoni ili ifanye uchunguzi. Kwani hii serikali ilipenda kufanya uchunguzi kuhusu Richmond au EPA? Ilifanya hivyo kwa sababu ya kuogopa kelele za wananchi pamoja na wabunge. Nafikiri Wana JF tukikomaa hapa, vyombo vingine vya habari kama kawaida yao watachukuwa hapa habari na kupeleka kwenye magazeti yao na ujumbe ukafika kunakohusika. JF ni KIBOKO kwa LOLOTE. Kwa hiyo tufanye kweli.
 
Back
Top Bottom