Mauaji ya albino, vikongwe, serikali inao mkono

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
TATIZO la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino ), tuhuma nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa waganga wa tiba za jadi ambao hudaiwa kuwa ni chanzo.

Hata akili na fikra za baadhi ya Watanzania zimegota kwenye dhana hiyo kuwa waganga wa jadi ndio hutoa masharti kwa wateja wao, kiasi cha kuwalazimisha kuua.

Kutokana na kuaminishwa hivyo, kauli za viongozi zimejikita zaidi katika kulaani waganga na kinachofuata ni kufutwa kwa vibali vyao vya kazi ili
waombe upya.

Kwa nini? Hili ni swali la msingi ,lakini je, anayetoa vibali anayo elimu au uelewa wa uganga wa tiba asilia? Je, anawajua vipi hao waganga matapeli na wakweli?

Lakini, udhaifu wa Serikali kwa upande mmoja imebainika kuwa umechangia katika mauaji ya albino, vikongwe kwani imekuwa ikishughulikia zaidi dalili badala ya tatizo.

Kwa mfano, maofisa utamaduni na michezo kaitka kila wilaya ndio waliokuwa watoa vibali kwa
waganga hao wanaodaiwa kuwa matapeli ambao wanadaiwa kutumia njia za kutoa masharti magumu
kwa wateja wao ili wajipatie fedha.

Maafisa hao ambao hawana uelewa wowote wa kazi hiyo licha yakutekeleza maagizo kama ya halmashauri, manispaa na jiji, mamlaka ambazo zimeweka malipo ya vibali kama chanzo cha mapato yao.

Matokeo yake maofisa hao wa serikali wakaruhusu
ongezeko kubwa la waganga wakiwamo matapeli kuwa karibu kila kona .

Vibali hivyo holela au fedha zikifika katika mamlaka hizo za kiserikali, maofisa hao hujinufaisha nazo huku waganga hao wakiishi katika kila nyumba ya kulala wageni.

Bila tahadhari, ,waganga hao wamekuwa wakijitangaza kwa tiba mbalimbali zikiwamo za utajiri, kuondoa nuksi, kurejesha wapenzi na kadhalika.

Uchunguzi unaonyesha kuwa wengi wao wanatoka maeneo ya Sumbawanga,Tanga na Kigoma.

Bika kujulikana walikotoka kama kweli ni waganga wanaofahamika hata kwenye vyama vyao , wamekuwa wakiachiwa kuendesha shughuli zao katika maeneo husika au mwafaka bila bughudha, kwani wanavyo vibali, wamejidhamini wao.

Kwa upande wa serikali inayoratibu vibali, kitu pekee kinachoangaliwa ni fedha zinazotokana na vibali.

Baada ya kuzuka kwa tatizo la mauaji ya abino, serikali katika maeneo mbalimbali ikakurupuka kuendesha zoezi la upigaji kura kwa watuhumiwa
mbalimbali wakiwamo wanaodaiwa kuwa wauaji ya albino.

Kiasi kikubwa cha fedha kimekuwa kikitumika kwa kura hizo ambazo zimepigwa mpaka leo, lakini hakuna majibu wala hakuna anayesema .

Viongozi wa vyama vya mila na desturi kama Lungo tiba asilia ,Chawatiata navingine hawajajulishwi matokeo ya upigaji kura huo,pamoja na kulaumiwa
kwa wanachama wao, yaani waganga wa tiba asilia.

Mayunga Kidoyayi (42), ambaye ni Katibu wa Mila na Desturi katika Mkoa wa Shinyanga anakiri kuwa halmashauri hutoa vibali kiholela ili kupata mapato
na hilo limechangia mauaji hayo kwani waganga matapeli wamekuwa wakitumia mwanya wa elimu duniya wakazi wa Shinyanga kuua albino na vikongwe.

"Mimi ni mganga wa tiba asilia, tena nimerithi mikoba ya baba yangunikiwa mdogo, kiungo cha albino hakimpi mtu utajiri na hakuna dawa ya
hivyo, huo ni utapeli wanafanyiwa kutokana na uelewa mdogo na udhaifu wa serikali kutoa vibali kwa matapeli wengi,"anasema.

"Moja ya tatizo ni elimu katika maeneo hayo watu walichelewa kusoma, hivyo wanatapeliwa na kwa masharti magumu na kuwa wakipata bado
wangeambiwa walikosea masharti.

"Mimi ni kiongozi wa mkoa sijawahi
kushirikishwa katika kutolewaa vibali huku waganga wanaota kila siku kama uyoga,"anasema.

Kidoyayi anaeleza kuwa aliwahi kumweleza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye kikao katika ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga jinsi Serikali ilivyochangia mauajihayo,na ndipo akafikia hatua ya kufuta vibali vyote waweze kuanza upya kusajili.

Mtandao.

Anasema kuwa kutokana na umaskini unaowakabili watu wengi, wenye fedha wakipewa masharti hayo ya kitapeli hukodi vijana na kuwa inadaiwa
wanawalipa kuanzia Sh200,000 hadi 400,000.

"Wanaofanya mauaji hayo hawatoki mbinguni wanajulikana ,tatizo ni ushirikiano duni uliopo kati ya waganga na Serikali inatutuhumu sisi bila
kukaa nasi.

Wauaji husafishwa kwa dawa na baadhi ya waganga waliowasajili wao warudi tushirikiane,"anasema.

Usajili unaotarajiwa kuanza upya utafanikiwa iwapo vyama vya wagangavitashirikishwa ili kubaini ni wapi amepata uganga,chimbuko lake, anatoa tiba zipi kwa ramli au dawa. Pia, iangaliwe historia yake, "anasema.

Kuhusu mauaji ya vikongwe anasema mabaraza ya kata ya ardhi ni chanzo cha mauaji hayo
kwa kuwa wajumbe wake hawana uelewa wa sheria na wengine hawajui kusoma na kuandika, lakini wanatoa uamuzi tata ambao husababisha watu
kutafuta waganga kwa ajili ya kesi.

"Hakuna dawa ya kesi zaidi ya ushahidi, lakini watu wanapoona hawakutendewa haki wanatafuta njia za mkato na wakifikia mikononi mwa matapeli ndipo hupewa masharti magumu na mauaji hayo yanagusa makundi hata ya vijana, lakini wakiua vikongwe hudaiwa kuwa wanahusishwa na
uchawi,"anabainisha Kidoyayi.

Pia, anadai mahakama za mwanzo zinachangia kwa kuwa hubadilisha kesi kwa maslahi binafsi hasa migogoro ya ardhi na kudai jinai na mtu anaposhindwa hutafuta waganga kama njia pekee ya kumaliza kesi.

Kidoyayi ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu wilaya ya Bariadi anasema kutokana na mlipuko wa magonjwa mbalimbali, mgonjwa
wa malaria akiwa akizungumza kwa maneno ,huambiwa wamelogwa na kutokana na
uelewa mdogo hupewa masharti magumu ya kuua vikongwe, mwishowe mgonjwa hufa na huambiwa walikosea masharti.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bariadi, Jackson Sima anakiri kuwa migogoro ya ardhi ni mwanzo wa mauaji ya vikongwe na wala si kama inavyoelezwa
kuwa ni imani za kishirikina na kuwa maamuzi mabaya ya migogoro imeifikisha wilaya kuwa na sura mbaya ya mauaji.

"Kuna ongezeko kubwa la watu ardhi inapungua na wanaomiliki ardhi wengi ni wazee matokeo yake wenye fedha ama vijana hutaka wakifikishana kwenye baraza wakiona wanaweza kushindwa hununua watu na kuwakamata, kuwavisha sifa za uchawi.

Mfano, mama mmoja aliuawa baada ya kutoka kwake kutokana na kutokubaliana na uamuzi wa baraza,"anasema.

Naye mratibu wa mila na desturi, Kanda ya Ziwa, Gambag'adi Kaliba anasema utitiri wa vyama vya waganga ni chanzo cha kuficha matapeli kwa kuwa
wanakuwa wote wanatibu kwa njia ya asili na wanatumia miti shamba wangekuwa na chama kimoja ingepunguza matatizo.

Chanzo.
Mauaji ya albino, vikongwe, serikali inao mkono
 
:A S 20:
Tanzania imeendelea kufanya mambo ya aibu ilihali dunia inatuchangaa.Hivi karibuni yameripotiwa mauaji ya kijana albino mwenye umri wa kati ya miaka 25 na 30 waliyodai yamefanyika kwa imani za kishirikina kutokana na wauaji kumkata mikono yote miwili, sehemu za siri, na kuondoka navyo.

Mwenyekiti wa TASS mkoani Arusha, Godson Mollel alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ikiwa ni siku moja baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa za kupatikana kwa mtu huyo Mei 26, mwaka huu wilayani Arumeru, ambaye mwili wake umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti kwenye Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.
Jamani aibu itaendelea mpaka lini? kwa nini watanzania mnapenda ushirikina na uchawi? kwa hali hii unafikiri mauaji ya albino Tanzania yatakoma?
 
Back
Top Bottom