Mauaji Songea Utata Mtupu

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,216
Sakata la mauaji ya waandamanaji Songea limezua utata mtupu kwenye ofisi za serikali wakitofautiana kwenye idadi ya waliokufa.
Jeshi la polisi limesema-Wawili wafa then 10 wajeruhiwa.

Ofisi ya Mkuu wa mkoa-wawili wafa then 20 wajeruhiwa.

Hosptali ya mkoa yasema-Wanne wafa then 41 wajeruhiwa.
Huu mkanganyiko wote ni dhambi ya Uonevu.
 
Poleni ndugu zetu wa Songea, haya ya polisi wa kitanzania ni mauza uza kwani hata sheria hawazifahamu vizuri. Kuua mtu ambaye hata manati hana ni mauaji. HAKUNA UBISHI HAPA lakini nikikumbuka boss wao pia alisha amuru watu wauawe kule Arusha sishangai - ni mtiririko huohuo.

Tukirudi nyuma, hivi hiyo iezi sita siju au tisa ambayo mtu anafundishwa uplosi inatosha kufahamu basics za sheria? Sidhani!

Upumbavu wanaoufanya wa kusingizia maandamano na fujo ni za Chadema wanatengeneza bomu litakalo kuja kulipuka siku moja, kwani nani kawaambia CCM inapendwa ki hivyo.

What the police force is doing now is trying with force to awaken the sleeping giant, ngoja hili jibabe liamke sijui walilisha nini.
 
Kama kawaida wanataka kutuficha wananchi ukweli kuhusu mauaji hayo, je kama wakiweza kutuficha sisi kwa Mungu wataweza kumficha?
 
Tuna hasira sana wananchi juu ya usenge kama huu wanaoufanya polisi na serikali yake.
 
Sakata la mauaji ya waandamanaji Songea limezua utata mtupu kwenye ofisi za serikali wakitofautiana kwenye idadi ya waliokufa.
Jeshi la polisi limesema-Wawili wafa then 10 wajeruhiwa.

Ofisi ya Mkuu wa mkoa-wawili wafa then 20 wajeruhiwa.

Hosptali ya mkoa yasema-Wanne wafa then 41 wajeruhiwa.
Huu mkanganyiko wote ni dhambi ya Uonevu.
hata angekufa mtu mmoja, hakuna maisha ya Mtanz\ania yanapaswa kupotezwa namna hii
 
Tarehe 22 feb ikumbukwe another bullet -in -back day on long road to true freedom kwa Watanzania.
 
Utetezi wa Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamhanda alisema polisi ililazimika kutumia nguvu ya ziada baada ya wananchi kukaidi amri ya kuwataka watawanyike.
Alidai waliopoteza maisha kutokana na vurugu hizo ni wawili na majeruhi 10 akisema watu hao walifariki dunia kwa kupigwa risasi za moto baada ya kukaidi amri ya polisi kutawanyika.

"Tulilazimika kutumia risasi za moto baada ya hawa vijana kukataa kutii amri ya polisi," alisisitiza Kamanda Kamhanda.
Kamanda Kamhanda alisema watu 56 wamekamatwa kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na tukio hilo.
Kamanda Kamhanda alisema ingawa bado uchunguzi unaendelea, taarifa za awali zinaonyesha kuwa chanzo cha vurugu hizo ni imani za kishirikina na siasa. Hata hivyo, hakufafanua ushirikina wala siasa zilivyochochea maandamano hayo.
RC atoa amri ya kutombea usiku

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu alisema vurugu hizo zilizodumu kwa saa sita zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na kuhatarisha usalama katika mji huo.

Kutokana na hali hiyo, alitoa amri ya kutotembea usiku akisema msako wa kuwasaka watuhumiwa wa maandamano hayo bado unaendelea.

"Kama watakuwa hawana shughuli za muhimu wabakie tu majumbani mwao ili kuepuka usumbufu. Polisi itaendelea kuwasaka watuhumiwa usiku ili kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria," alisema.

Mkuu huyo wa Mkoa alitoa kauli hiyo baada ya kuongoza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kilichoitishwa ghafla kutokana na machafuko hayo makubwa.
 
Hawa polisi wa stairi hii wanapatikana tanzania pekee kiwe kivutio basi cha utalii
 
Back
Top Bottom