Mauaji Nyororo - Trivia Question - Michael Kamuhanda yupo picha zote mbili?

https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=63619&d=1346616304Re: Mauaji Nyororo - Trivia Question - Michael Kamuhanda yupo picha zote mbili?

quote_icon.png
By Candid Scope
attachment.php


Re: Mauaji Nyororo - Trivia Question - Michael Kamuhanda yupo picha zote mbili?

quote_icon.png
By Candid Scope
attachment.php


Hii picha ina majibu mengi sana; Polisi wanaweza kutumia kila mbinu kujitetea lakini kwa hili wamecheza faulo mbaya...Jaribu kuiangalia kwa makini hii picha na kusoma kitendo cha kila askari. Utagundua kuwa wapo waliokuwa wanawazuia wenzao kuendeleza kipigo kwa mwandishi huyo(angalia movement za askari kanzu mwenye fulana ya bluu, pia kuna askari mwenye kofia nyekundu asiye na kikinga risasi, pia kuna askari upande wa pili mwenye kofia nyeusi)....
Hivyo huyo mwandishi alipigwa tena kipigo kibaya na Hivyo huyo mwandishi alipigwa tena kipigo kibaya na ndio maana yupo chini akiwa hajiwezi.
Angalia pia mkono wa kulia wa huyo mwandishi, katika kiganja chake ameshika kamera, kwa hilo tu polisi walitakiwa watoe ulinzi maana kitendo cha kuwa na kifaa kama kamera ni ishara kuwa jamaa alikuwa ni mwanahabari naalikuwa katika harakati za kazi.
Halafu pia ukijaribu kuivuta picha kwa karibu utaona kuna kitu kama moshi kinafuka karibu kabisa na mwili wa marehemu na moshi huo unaelekea moja kwa moja
HAYA MANENO NIMEKOPI NA KUPESTI KUTOKA JAMII FORUM SIASA!












 
Mungu awabari sana waliopiga hizi picha ambazo zimeendelea kuweka wazi uovu unafanyika ndani ya Jeshi la polisi, maana viongozi wa police ni wazuri sana wa kufunika uovu. wakifanya uovui chapu chapu wanakimbilia kwenye media kuapindisha ukweli, kama vile walivyofanya kwa tukio la ulimboka. sasa watu wa media kuweni macho kutumiwa na police ili kuficha uovu wao. wanafanya waua wana report kwenye media story tofauti
 
Mbona chadema hawaonekani kama wanavyo dai? au mwandishi ndo chadema
 
Mie naomba niulize swali moja tu!!!

" KWA NINI CHADEMA WANAFANYA MAANDAMANO PASIPO KIBALI.....? "

Hakuna maandamano yanayohitaji kibali, ni taarifa tu kwa polisi inahitajka. Kazi ya polisi ni kulinda waandamanaji na wengine ambao si waandamanaji, ili maisha ya wote yawe salama na uharibufu wa mali usitokee.
 
Ninavyoona mimi nahisi hatujui sheria inayoongoza jambo hili. Kwanza hakuna sheria inayosema ili chama cha siasa kifanye mkutano lazima kiombe ruhusa polisi ili waruhusu. Kilichopo ktk sheria ni kutoa taarifa polisi kwa ajili ya kupatiwa ulinzi. Pili, katika mikutano ya chadema hata siku moja vurugu huanza na waanachama bali polisi. Katika hali ya kawaaida, fikiri labda sheria inaruhusu polisi kukataza mikutano ya vyama. Ikiwa jambo hilo ndivyo lilivyo, baada ya kukaidi polisi walipaswa kufika na kuwakamata hao wanaofanya mkutano na kuwafikisha katika vyombo vya sheria na siyo kuua watu tena mwandishi wa habari ambaye hata kwa akili ndogo tu hakuwa na shida maana alikuwa pale kuchukua habari. Kama polisi walikuwa wanafanya shughuli yao kisheria kwa nini wamwogope mwandishi wa habari? Lakini pia fikiri kidogo, hivi kweli polisi anadiriki kuwasha moto gari ambalo limesimama limekosa nini hilo? Nenda mbali zaidi, ndugu yangu Mtanzania ebu tuwe wapembuzi wa mambo siyo kuongea ongea tu bila fikra ya ndani. Narudia tena, zamani sikufikiri polisi kama binadamu anaweza kufikia hatua ya kuchukua silaha na kumwua binadamu mwenzake aliye na watoto na kuacha hao watoto wahangaike maisha yao yote kwa ajili tu ya kulinda maslahi ya mtu. Kama watanzania mtakuwa na ushabiki na michango isiyoenda ndani zaidi polisi na wote wataendelea kuua maana hata vichwa vyenu vinaonyesha hali ya unyama na si ubinadamu. Sisi Waafrika tunamwelekeo fulani ambao hata watu wa mabara mengine wanatuona tunamwelekeo wa kiunyama zaidi kuliko ubinadamu. Tumekosa ustaarabu wa kibinadamu. HUWEZI KUMWUA MWENZAKO KWA MASLAHI MADOGO UNAYOPEWA NA ALIYEKUTUMA. Mimi nawashangaa watu wanaochezea maisha ya watu. Mtu mnayemwua anategemewa na mama yule ambaye ni mzee sana, mke na watoto. Baba leo kaondoka kwenda kutafuta riziki kihalali ili sisi watoto wake tule tushibe. Anarudi amekufa kapigwa risasi na polisi bila sababu ya msingi. Leo sisi hatuana ada na njaa inauma maana hatuna wa kutulisha maana baba aliuawa na polisi akiwa kwenye kazi halali. Nyie mnaofikiri CHADEMA HUANZISHA FUJO naapa si kweli ila polisi huanzisha FUJO. Kwa maslahi ya nani, mimi sijui.
 
Ugaidi mara nyingi unazalishwa na watawala kwa staili kama hizi.
Haiwezekani mzazi wako anatolewa roho hivi hivi na wanaolipwa kwa Kodi yako/jasho lako.Iko siku na si muda Mrefu tutakuwa na Boko Haram ya Tanzania Kama hatua hazitachukuliwa dhidi ya wahalifu hawa(POLISI).
 
Hatuwezi kuendelea na kuwa na amani iwapo kundi moja halikubali mabadiliko na linatetea lenyewe kuendelea kuongoza hata kama limeshindwa kuwaondoa wananchi wa kawaida katika rindi la umaskini LALA KWA AMANI DAV

Tusidanganyike kuwa Tanzania ina Amani, hayo ni mahubiri ya wanasiasa ambao wanatumia lugha hiyo kuogopesha wananchi wasing'amue madudu wanayoyafanya. Kwa waliozunguka kidogo hata kwa majirani zetu kama Zambia, Botswana, namibia n.k, achilia mbali nchi za ulaya; wataelewa namaanisha nini. hali tulionayo sisi ni hali fulani ya utulivu, na ni utulivu wa kijinga ambao haukupasi kuhoji lolote lile ili mradi mkono uende kinywani, hata kama ukimya huu utavigarimu vizazi vijavyo.

na tukija kwenye swala la haki hapo ndio hapaelezeki kabisa.
 
SAM_4974.JPG
attachment.php


Gazeti la Uhuru linatoa taarifa kuwa katika tukio la kuuawa mwanahabari, OCS aliumia vibaya na yuko mahututi hospitalini, je katika kundi lililomzingira hayati Mwangosi, OCS ni yupi kati ya hao, kwa vyo vyote alikuwa karibu na marehemu na kuweza kujeruhiwa. Wanaokaa Iringa kwa vyo vyote wanamjua wanaweza kutujulishwa ni yupi katika kundi hili.
 
Tumefika hapa? Kweli watanzania tumwombe Mungu. Haya sii mambo ya kawaida. Kamanda huyu atakufa kesho tu, lakini alichokionyesha kwa umma kinatisha mno. Unamwua mtu mchana kweupe tena mbele za watu kama mnyama ati kisha amekuhoji tu maswali machache ya msingi? Tunaenda wapi na hili jeshi la polisi? Tunalipeleka wapi taifa hili na watoto wetu? Matumizi ya silaha ndiyo haya? Kazi ya RPC ndiyo hii? Mungu uturehemu kwani polisi wetu wamegeuka kuwa wanyama wa msituni!
 
Angalia picha vizuri, utaona kuwa mwandishi ameelekezewa mtutu wa bunduki ya kufyatulia mabomu ya machozi. amuda mfupi tu mwandishi amefariki kwa kulipuliwa na bomu hilo. Hii ina maana kuwa askari aliywmwelekezea mwandishi bomu mtutu wa bunduki alifyatua bomu hilo ambalo lililipuka tumboni kwa mwandishi na kumuua papo hapo. Kwa kuwa mwandishi alikua karibu sana na askari, mlipuko huo ulimjeruhi pia askari huyo, ambaye anaonekana kwenye picha akisaidiwa (akibebwa) na wenzake.

je bomu la machozi hulipukia hapo hapo au kwenye distance fulani..tena kwa muda fulani????? hicho kifaa(bunduki say) je hutumikaje? kama chombo cha kurushia tu ama?
Tuambiane ukweli na si kushabikia tu, ndo maana inasemekana IMECHAKACHULIWA... wajuzi tujuzeni uongo huu uenezwao
 
Angalia picha vizuri, utaona kuwa mwandishi ameelekezewa mtutu wa bunduki ya kufyatulia mabomu ya machozi. amuda mfupi tu mwandishi amefariki kwa kulipuliwa na bomu hilo. Hii ina maana kuwa askari aliywmwelekezea mwandishi bomu mtutu wa bunduki alifyatua bomu hilo ambalo lililipuka tumboni kwa mwandishi na kumuua papo hapo. Kwa kuwa mwandishi alikua karibu sana na askari, mlipuko huo ulimjeruhi pia askari huyo, ambaye anaonekana kwenye picha akisaidiwa (akibebwa) na wenzake.
Vyombo vyetu vya habari vimekua nikuchochea machafuko baada ya kueleza ukweli kuhusu matukio yanayojiri maeneo mbalimbali!!
 
Mie naomba niulize swali moja tu!!!

" KWA NINI CHADEMA WANAFANYA MAANDAMANO PASIPO KIBALI.....? "

Kwa sababu kuandamana ni haki ya kikatiba hata wewe unayo haki hiyo ndiyo maana unaandamana mara nyingi tu na hupati bughuza, hakuna mwenye hati miliki ya maandamano ambaye anatakiwa atoe kibali,polisi kwa kuwa hawajui na wala hawajijui wanafikiri wao ndiyo wenye haki ya kutoa kibali cha kuandamana lakini si kweli.
KUANDAMANA NI HAKI YA RAIA WA NCHI HII,labda na wewe tusaidie ni maandamano gani ambayo yameweza kusababisha maafa pasipo kuwa na polisi ?
 
je bomu la machozi hulipukia hapo hapo au kwenye distance fulani..tena kwa muda fulani????? hicho kifaa(bunduki say) je hutumikaje? kama chombo cha kurushia tu ama?
Tuambiane ukweli na si kushabikia tu, ndo maana inasemekana IMECHAKACHULIWA... wajuzi tujuzeni uongo huu uenezwao

Angalia picha hii hapa chini, halafu uniambie kama kuna uchakachuaji, basi polisi ndio wanaochakachua tukio zima.
Hapa kwenye picha mwandishi amezingirwa na polisi saba! wakiwa na silaha za moto. Unaziona silaha za moto mikononi mwa polisi?
Ni baada ya hapo tu ndio mwandishi akawa amekufa kwa kulipuliwa na mlipuko.
Sasa niambie mlipuko ulitokea wapi?
Mlipuko ulisababishwa na nini?
kama mlipuko ungekuwa ni wa bomu la kutupwa kwa mkono (hand grenade), asinge pona hata mtu mmoja kwenye kikundi hiki hapa kwenye picha.
Labda, wewe unasema kuwa mwandishi alipasuliwa tumbo na hao polisi, lakini si kwa kutumia bunduki ya kufyatulia mabomu ya machozi, ila ni kwa kutumia kisu, panga, n.k.
Acha kutetea mauaji, kwani hujui aktakaye fuata kuuawa anaweza kuwa wewe mwenyewe, na watu wengine kama wewe wakaja hapa JF kutetea mauaji hayo kama wewe unavyofanya!!

attachment.php
 
Mungu irehemu Tanzania, utuhurumie . Warehemu na hao walio na nafasi ambazo wanageuza kuzitumia vibaya,utu umetoweka,watanzania imefika mahali utashi hatuna,lakini utu pia umetoweka. Mungu irehemu Tanzania ,utuponye. It is against humanity.
 
Angalia picha hii hapa chini, halafu uniambie kama kuna uchakachuaji, basi polisi ndio wanaochakachua tukio zima.
Hapa kwenye picha mwandishi amezingirwa na polisi saba! wakiwa na silaha za moto. Unaziona silaha za moto mikononi mwa polisi?
Ni baada ya hapo tu ndio mwandishi akawa amekufa kwa kulipuliwa na mlipuko.
Sasa niambie mlipuko ulitokea wapi?
Mlipuko ulisababishwa na nini?
kama mlipuko ungekuwa ni wa bomu la kutupwa kwa mkono (hand grenade), asinge pona hata mtu mmoja kwenye kikundi hiki hapa kwenye picha.
Labda, wewe unasema kuwa mwandishi alipasuliwa tumbo na hao polisi, lakini si kwa kutumia bunduki ya kufyatulia mabomu ya machozi, ila ni kwa kutumia kisu, panga, n.k.
Acha kutetea mauaji, kwani hujui aktakaye fuata kuuawa anaweza kuwa wewe mwenyewe, na watu wengine kama wewe wakaja hapa JF kutetea mauaji hayo kama wewe unavyofanya!!

attachment.php
mbona umetoa picha yenye maelezo ya uchakachuaji??? kunapicha yenye kuonyesha RPC,MUUAJI NI HUYU n.k
Inatulazimisha kuamini kuwa hiyo ndo pointi hasa MAREHEMU akafa sekunde chache zilizofuata kitu ambacho ni ngumu kumeza kwani kuna maelezo kuwa RPC alikuwa kwenye GARI.....!
BIBLIa INATUAMBIA KUHUSU KWELI NA KWELI KUTUWEKA HURU........sasa RPC alikuwa kwenye GARI au alikuwa eneo la tukio akiamrisha mauaji....!
SIKUBALI KUTUMIA UONGO KUELEZEA TUKIO ILI IONEKANE KWELI
 
Aliyesimama katika ya hao askori walimzingira marehemu mwenye kifimbo ni RPC ambaye picha yake nyingine ni hiyo hapo Chini. Ni uthibitisho kwamba aliyetoa amri ya kumwua ndugu yetu mpiganaji ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa. Hapa chini laleta gari lake ambalo lilikuwepo katika tukio.

DAUD.JPG


Gari la Kamanda wa Polisi Mkoa ambaye alikuwapo katika tukio hilo na ndiye aliyeshuhudia tukio la Kuuawa Mwanahabari Daud Mwangosi.
DAUDI.jpg
 
Kama huyo mnaye mtaja kuwa ni Kamuhanda ndiye, basi namsamehe kwa kuwa alikua anamtetea na ndiye aliyevunjwa miguu akikumbatiwa na Mwenzetu Mwangosi. Hii ndiyo inasababisha tunaoneka tunachakachua picha
 
Back
Top Bottom