Bigirita
Platinum Member
- Feb 12, 2007
- 15,986
- 7,366
hii ni aina ya Watanzania walio wengi sana, hawasomi wala hawataki kufahamu vitu kwa undani wake.Mie naomba niulize swali moja tu!!!
" KWA NINI CHADEMA WANAFANYA MAANDAMANO PASIPO KIBALI.....? "
1) CHADEMA hawajafanya maandamano, walikuwa wanafungua matawi kwenye mitaa, vijiji na kata pamoja na kufungua ofisi katika ngazi hizo.
2) Hakuna sheria inayokataza maandamano au inayotaka kupata kibali polisi......kama sheria haipo, hakuna mwenye mamlaka ya kukataza maandamano yasifanyike. Polisi hawawezi kujipa mamlaka hayo kwasababu tu wao wana mabomu ya machozi na risasi za moto.
Tabia ya matumizi ya ecessive force by the police tumeiona ikikua siku hadi siku. Hata wanafunzi wa Vyuo wakigoma, polisi wanatumwa wakawapige....kwanini umpige mwanafunzi aliyegoma kuingia darasani? sheria zinasemaje kama mwanafunzi akigoma kuingia darasani?
Upuuzi wa CCM na Udhaifu wa kiongozi wa serikali ndio unaotufikisha huku. Sasa hivi ni fashion kuwatuma FFU kufanya fujo.