Mauaji kikatili ya kimara temboni

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,568
2,911
Ama hakika Dunia imeisha! Maana imeshuhudiwa watu wawili wakipigwa risasi live mbele ya familia za bila hata wao wenyewe wala familia zao kujitetea!!( Soma nipashe ya Jumapili). Mimi bahati niko jirani na waliouliwa! na wauaji walifyatua risasi na Shortgun zao kutishia raia wema kusogea maeneo ya tukio.
Wa kwanza aipigwa risasi sebuleni na kuvutiwa chumbabi huku damu zikichuruzika, wa pili alifumaniwa gaetini akiingia na gari lake kutoka katika shughulu zake. Matukio yote yalipishana kama 30 minutes.
Maana majirani tumebakia midomo wazi hatujui tuanzie wapi ama kumalizaia wapi. Na hii si mara ya kwanza matukio kama hayo kuripotiwa. Je yawezekana turudishe enzi za Lyatonga mrema (SUNGUSUNGU) ambapo kila ikifika saa1 jioni kila mwanaume anakuwa nje? Maan kutegemea Polisi tu naona haitoshi! Naomebeni ushauri:confused2:
 
Poleni sana.
Sasa kama nimeajiriwa na shirika la uma au serikalini (mfano mwalimu, daktari, hakimu etc) na polisi ni vivyo hivyo. Sasa nikifanya kazi ulinzi (Lyatonga style) usiku kucha ni nani atafanya kazi zangu keshoye? This is problem of inefficient government, period!
 
poleni jamani, kusuhudia vitu kama hivi ni ngumu...ndio msiba wa ndugu uliotangazwa humu?
 
Kwani mkiweka sungusungu ndio mtakomesha mauaji?
Wao wana bunduki, nyie mna mapanga na fimbo...
Hamna haja ya sungusungu, kila mtu akiweka moyo wake safi haya mambo ya kuuana yatapungua.
Mioyo yetu imejaa dhuluma na tamaa ya mali.
Tumrudie muumba.
 
Samahani sikuweza kuwa hewani kwani tulienda kuaga miili ya marahemu pamoja na miili kupelekwa kanisa la mavurunza kwa misa( Catholics) Ila jamani hali inatisha sana. Kila mtu anasema lake. Maana hata sie majirani bado tumepigwa na Butwaa!! Though there is a clear evidence of kisasi!!!! it wa a planned move! However at the end if the day je waliofanya hivi wot have thery achieved???
 
Jamaa wote walikuwa ni wafanyibiashara pale kariakoo. garments. Walikuwa wankwenda nje nje kufuata mizigo yao wenyewe(they were successful) Na wote ni marafaiki na waote wanatoka Kibosho. Mengine siwezi kueleza maana ni hear say!
 
Hiyo lazima itakuwa issue ya kibiashara, si ajabu wameshinda pahali wakakataa kutoa haki za wengine, maana hakuna pesa zilizochukuliwa kutoka kwao, kwani hamkumbuki issue ya ABDUL OMAR MASUDI WA RTD?
 
Jamaa wote walikuwa ni wafanyibiashara pale kariakoo. garments. Walikuwa wankwenda nje nje kufuata mizigo yao wenyewe(they were successful) Na wote ni marafaiki na waote wanatoka Kibosho. Mengine siwezi kueleza maana ni hear say!

we weka na hearsay zote,hearsay zingine huwa zinasaidia polisi, pia inaweza kusaidia watu wengine humu kubadili mielekeo ili yasiwakute kama hayo. jimwage tu, hapa ni pahala pa uwazi na ukweli...
 
Ama hakika Dunia imeisha! Maana imeshuhudiwa watu wawili wakipigwa risasi live mbele ya familia za bila hata wao wenyewe wala familia zao kujitetea!!( Soma nipashe ya Jumapili). Mimi bahati niko jirani na waliouliwa! na wauaji walifyatua risasi na Shortgun zao kutishia raia wema kusogea maeneo ya tukio.
Wa kwanza aipigwa risasi sebuleni na kuvutiwa chumbabi huku damu zikichuruzika, wa pili alifumaniwa gaetini akiingia na gari lake kutoka katika shughulu zake. Matukio yote yalipishana kama 30 minutes.
Maana majirani tumebakia midomo wazi hatujui tuanzie wapi ama kumalizaia wapi. Na hii si mara ya kwanza matukio kama hayo kuripotiwa. Je yawezekana turudishe enzi za Lyatonga mrema (SUNGUSUNGU) ambapo kila ikifika saa1 jioni kila mwanaume anakuwa nje? Maan kutegemea Polisi tu naona haitoshi! Naomebeni ushauri:confused2:

Poleni sana ni meisoma hii leo, inasikitisha sana, Mbezi Juu na sie yalitukuta, but believe me sungusungu imesaidia sana, mwezi sasa Mungu yupo tumepumzika maana ilikuwa nyumba kwa nyumba, risasi hewani wote wanatawanyika, ila tuliposema na iwe vipi risasi ikipigwa watu twende kutoa msaada unaambiwa masai na mkuki wezi na bastola waliua jambazi mmoja na watu kadhaa kujeruhiwa ila ndo kama mwisho wa stori, ila ulinzi unaendelea una hela toa masai wanawekwa mtaani.
sie mwanzo ilikuwa toa hela la sivyo wanakukata mapanga na risasi miguuni, mmoja aligomea walimkata hadi kufa kwa kuvuja damu, kwa hiyo sio suala la biashara pekee wote ni wahalifu.
 
Sungusungu yawezekana Tatizo ni ku mobilse watu!!
 
1.ulinzi na usalama wa watanzania upo mikononi mwa watanzania wenyewe.....sungusungu ni muhimu.
2.Unapofanya biashara,jitahidi sana USIMDHULUMU mtu yeyote(sijasema marehemu walidhulumu)
3.Ni hatari pia kudisclose unaishi wapi kwa kila mtu,eti kisa wajue unanyumba nzuri na ni tajiri.
4.Wale watakaojua unaishi wapi si vizuri wakajua unafanya nini.
5.Kuna SUPER DEALS ambazo mtu akikudhulumu huwezi kwenda polisi,kwa mfano umedhulumiwa tani moja ya madawa ya kulevya utashitaki wapi?(sina maana wamedhulumiana)
6.Ni kosa pia kumuachia mtu kiasi kikubwa cha pesa tasilimu za biashara labda akakununulie bidhaa au akalipie malipo fulani.
tumia hundi siku zote. FIKIRIA ukifa ghafla itakuwaje?
7.Mshirikishe mungu katika biashara zako hasa kwa kutoa zaka.Kwa kufanya hivyo Mungu anakuwa mbia/share holder....na si unajua ulinzi wake mungu?
8.Mwisho usimwamini mtu yeyote,ndio i mean mtu yeyote hapa duniani.mke,mzazi,rafiki.....mchungaji,shehe...
.
HAYO NI MAWAZO YANGU.................POLENI SANA WAFIWA..
 
Na mimi nasema usimwamini mtu ye yote kupita kiasi.
 
Tatizo ni kwamba majambazi wanapiga ma-deal na polisi, kipindi cha sungusungu hizi deal hazikuwepo kwa sababu sungusungu ni jamii nzima na polisi walichukia sana kwa kukosa ma-deal kipindi kile ndiyo maana serikali ilipoanza kuwamulika sungusungu polisi walifurahi sana na wakawaonea sana viongozi wa sungusungu hivyo ku-discourage wengine kujishugulisha na sungusungu kwa moyo wote.
 
Anzia kwa watu ambao unaona wanaguswa na hii issue ya usalama kwa sababu ndani ya jamii pia kuna watu wanashirikiana na wezi hivyo utakuwa discouraged, anzia na watu wakaribu then wao waambiane hadi mnakuwa wengi mnamfuata mw/ serikali ya mtaa. kunakuw ana kamati maalumu ya ulinzi ndio hao watakaohusika na nini kifanyike.
Sie kwetu tulipoanza wezi ghafla wakajua muda sungusungu wanaamka, wakaanza kuja saa zingine, na kamati inajaipanga tu hadi walipokamatwa.
Mambo ya kunyooshea kidole kuwa ni wafanyabiashara sio sawa sie pia tulisema hivyo maana hao ndio wana hela na wezi walianzia huko then ikawa kama shopping... Tunatakiw atuwe na ulinzi wetu kisasi au sio je haya yanaweza kutokea oysterbay? shaban robert? kwani kule hawana visasi? ni kwa sababu hatuna ulinzi na polisi akiitwa anakuja baada ya saa 8 (asubuhi).

Sungusungu yawezekana Tatizo ni ku mobilse watu!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom