Mauaji Kigoma kusini baada ya uamuzi wa Mbatia na genge lake

Hivi Mvungi ali-chair ule mkutano wa kumfukuza Kafulila kama nani ndani ya chama??? Isije ikawa alichea kulinda ukanda maana mbatia na mvungi wanatoka Kilimanjaro.

TZ hakuna democracy nchini na ndani ya vyama
Napenda nikuhakikishieni kwamba Dr.Mvungi hakuwa mwenyekiti wa mkutano huo. Tanzania tunayo matatizo mengi; hili la uongo na upotoshaji nalo ni kubwa.
 
Dkt Mvungi ni VC wa chuo cha Bagamoyo pia ni mpinzani.

Inashangaza mpinzani anapandishwa vyeo wakati wapinzani wengine wanatimuliwa, nilipojiuliza swali hili nimepata majibu kuwa inawezekana upinzani wake iso hatari kwa mustakabali wa ruling party. Sasa naanza kuwa na wasiwasi kwa nini wajumbe hawakupiga kura ya siri kwa kitu sensitive kama hichi?

Lakini vita hii ya kupata uhuru wa kweli kutoka kwa syndicate ya ruling party tutashinda.
 
Hii inaonyesha wazi kuwa viongozi wa baadhi ya vyama hawapo kuttea maslahi ya wananchi, bali wapo kwa malengo yao. Iwapo watu wanamkosoa Rais wa nchi, itakuwaje Mbatia yeye hataki jina lake kuguswa. Ni dhahiri watu wa namna hiyo si watu wakutegemewa katkia kuimarisha demokrasia. Hawajali hata matumizi ya hela za taifa katika chaguzi ndogo alimradi wao wanapata watakayo. Kweli Tendwa yupo sahihi hata huu ni ufisadi.
 
Kwa nini umehusisha uchaguzi mdogo na mauaji mkuu?
Hapana.....haifai hata kidogo...usihusishe mauaji ya Igunga na demokrasia...hapana mkuu...
Jenga hoja kwa vigezo vingine....sio mauaji, kwamba tuache kufanya uchaguzi kwa kuogopa mauaji?

Hata hivyo, nakubaliana na wewe kuhusu ukubwa na gharama....
Hata kichwa cha habari hakina mashiko....its more of shigongo thing!
 
kweli mkuu,inaonekana Mvungi upinzani wake ni targeted,hauna madhara yoyote ndio maana serikali imeendelea kumkumbatia
 
Sasa unampinga Mbatia au Kafulila aliyekuwa akilia na kujutia kuwa kamkosea Mbatia? Maana Kafulila kakiri kosa na kujuta tena kwa machozi hadi Mbatia akamuonea huruma na kumuombea msamaha ina maana Mbatia na Kafulila sasa lao moja, kwa hiyo kama Mbatia ni CCM basi Kafulila pia amegive up na kuwa naye ni CCM.

Mnamteteaje mtu aliyekwisha kiri kosa? Tafakari mkuu. Amuombe ushauri rafiki yake Zitto

kusema ukweli kitendo cha huyu bwana mdogo kupiga magoti kuomba msamaha na kulia ni aibu kubwa sana kwake na kwa wanaharakati, sasa huyu kuna nyakati alikuwa anatoa kauli kali kama za nelson mandela au solomon mahlangu akitoa hisia za ukombozi, akatishia maandamano nchi nzima sasa hii kupoteza tu ubunge anaanza kupiga magoti je angekamatwa na kutupwa gerezani na torture kama akina mandela ingekuwaje?? hafai ni aina ya walewale ambao wanachochea vurugu lakini zikianza wanaingia uvunguni!!
 
[/QUOTE]mmbangifingi kweli mkuu,inaonekana Mvungi upinzani wake ni targeted,hauna madhara yoyote ndio maana serikali imeendelea kumkumbatiapat john Hii inaonyesha wazi kuwa viongozi wa baadhi ya vyama hawapo kuttea maslahi ya wananchi, bali wapo kwa malengo yao. Iwapo watu wanamkosoa Rais wa nchi, itakuwaje Mbatia yeye hataki jina lake kuguswa. Ni dhahiri watu wa namna hiyo si watu wakutegemewa katkia kuimarisha demokrasia. Hawajali hata matumizi ya hela za taifa katika chaguzi ndogo alimradi wao wanapata watakayo. Kweli Tendwa yupo sahihi hata huu ni ufisadi.
Hawa viongozi dizaini ya kina Mvungi wapo wengi katika vyama vyetu vya siasa.
 
Khaaa!!

Kumbe kule NCCR-Mageuzi vita huenda ikawa na kati ya IKULU na wabunge machachari wapenda mabadiliko na wanachama washabiki wao eti kwa kosa tu la kukisema CCM, kupinga dhuluma na wakati mwingine kukiunga mkono CHADEMA hadharani?

Pamoja nayote, James Mbatia hebu katuridhishe umma wa Tanzania unachokifahamu juu ya madai haya mazito mnoooo na hizo biashara mnazodaiwa kuendesha na CCMnyuma ya pazia kwa kutaka kuangamiza vyama vingine vya ushindani nchini.

Come out clean on these Mbatia hatutaki mchezo!!!


Tunapaswa kujifunza demokrasia upya, najiuliza nini maana ya Freedom of expresion?

Tukiwazuia watu kuongea what we call siri katika media ni sawa? Maana kama chama kinarumika na CCM wasiseme? Ukiona Mbatia anafanya jambo ujue wakubwa zake wa kazi wamekwishampa go ahead, katika kesi ya kawe Mh. Mdee na mawakili wake walifanya juhudi hadi muda wa kesi ukaisha bila kesi kusikilizwa, lakini Kombani kawaongezea muda kusikiliza kesi hiyo kwani lazima lirudi CCM kwa kutumia kesi ya Kijana wao Mbatia.

Katika sakata la Kafulila, wajumbe walibadilishwa na nakala ikapelekwa kwa Msajili wa Vyama siku mbili kabla ya NEC ya dharura, Rungwe alipoenda kupinga akakuta Tendwa ana updated list ya Wajumbe na wengine wamefutwa na kuweka wapya ili wapige kura kwa adhma ya kuwafukuza waliompinga Mwenyekiti.

Hiyo haikutosha bali watu walilazimishwa kupiga kura kwa kunyanyua mikono, kwa ile fukuza wajumbe wengi wanakiri kuwa waliogopa na kwa kuangalia maslahi yao waliamua kunyoosha mikono kwa lazima.

Je madai ya Rungwe kuwa Mbatia alimzuia kuisema CCM katika uchaguzi wa mwaka jana ndio yameisha? Rungwe alikiandikia chama barua kulalamikia hatua hiyo, je majibu ya maswali hayo ndiyo hayo?

Kafulila alikataa kwenda kumuona Rais, masaa machache baada ya kufukuzwa chama kimepata mwaliko wa ikulu, je kuna shinikizo toka juu?

Tendwa na Nape wamezungumzia gharama za Uchaguzi mdogo kuwa utakuwa na gharama kubwa, tumeshuhudia katika uchaguzi wa Igunga mauaji na watu kujeruhiwa kutokana na mchakato ule wa uchaguzi, je hatuangalii gharama ya damu za watanzania wenzetu inayoweza kumwagika kigoma kusini kwenye uchaguzi huo mdogo kama ukitokea?

Mauaji hayo nani alaumiwe? Je, damu ya watu watakaopoteza maisha katika uchaguzi wa kigoma kusini kama ukitokea uwe juu ya kichwa cha Mbatia na genge lake?

Je, kuwa na uvumilivu wa kisiasa na kuwajibika katika changamoto zinazokukabili haina faida kubwa kuliko kuweka maisha ya watu katika hatari na kupoteza muda katika chaguzi?

Bilioni 19 zitakazotumika katika uchaguzi zingetumika kulipa madeni ya waalimu, je tatizo s lingepungua?

Tafakari chukua hatua!
 
Sasa unampinga Mbatia au Kafulila aliyekuwa akilia na kujutia kuwa kamkosea Mbatia? Maana Kafulila kakiri kosa na kujuta tena kwa machozi hadi Mbatia akamuonea huruma na kumuombea msamaha ina maana Mbatia na Kafulila sasa lao moja, kwa hiyo kama Mbatia ni CCM basi Kafulila pia amegive up na kuwa naye ni CCM.

Mnamteteaje mtu aliyekwisha kiri kosa? Tafakari mkuu. Amuombe ushauri rafiki yake Zitto

Mkuu Kafulila amekiri kosa gani,lini na wapi?Na kama alikiri kwanini hakusamehewa?Na kama alikiri kweli na hakusamehewa uko wapi uungwana wa wale waliokataa kusamehe??,,,,Dogo amechinjwa kwa sababu ya chuki,husda,tamaa,visasi na kukomoana FULL STOP!Mbona suala liko wazi kabisa waungwana?
 
Hapa kuna hoja kuwa Mbatia ni CCM je kafulila akirudishiwa Uanachama Mbatia atabadirika kuwa CCM??
 
katika maisha yetu ya kila siku huwezi tenganisha siasa,siasa ndiyo key leader ya mustakabali wa taifa na wananchi wake.Tatizo linalosababisha siasa ionekane mbaya ni viongozi wahusika kuitumia fursa hii au kwa kukandamiza demokrasia ama kuiua kabisa demokrasia.Wengi wetu tunashindwa kujua kuwa hata hivi vyama ni taasisi za umma na si za watu fulani.Vinginevyo wangeanzisha vyama vya kifamilia vyenye mitazamo ya kifamilia zaidi.Haiwezekani hata kidogo chama cha kisiasa kugeuka ni mali ya mtu binafsi.ikifikia hivyo ni hatari sana katika mustakabali wa maisha yetu na nchi yetu.Hatupo katika mfumo wa kikomunisti kuwa na chama cha wateule wachache(vanguard party)

Napenda sana pia kutumia fursa hii kumshauri msajili wa vyama vya siasa nchi kuwa makini,ikibidi kupeleka mapendekezo kwa waziri wa sheria kuangalia upya aina ya vyama vinavyoanzishwa kama vina malengo ya kuwalinda wachache ilikukidhi maslahi yao au vina tija katika mustakabali wa kuwaonyesha njia wananchi.Madiwani wasaliti wa CHADEMA walipofukuzwa ndani ya CDM serikali nzima ilikurupuka kiasi cha waziri wa TAMISEMI kuwakingia kifua kulipwa posho za vikao ili hali akijua kabisa anakiuka na kutoitia katiba ya nchi.Leo hii watusiki msajili wa vyama wala waziri aliyethubutu kulizungumza hili kwa kuwa halina maslahi na chama tawala na serikali yake.Ni hatari sana kwa watu wachache tena waliopandikizwa kumng'oa mbunge wa wananchi wakati wananchi wanamuhitaji katika kupigania maendeleo ya jimbo lake.

mimi kama kijana nimesikitishwa sana na umangimeza huo uliotumika kukandamiza demokrasia na kuvunja katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 18 ya katiba inayosema-kila mtu

(a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake.

Kwanini basi mawazo ya Kafulila yasiheshimiwe na kuwa changamoto katika mustakabali wa kukiboresha chama hicho?Hakuna hata mmoja alizaliwa kuwa kiongozi na atakufa akiwa kiongozi!Kumsulubu Mh. Kafulila ni ombwe la uongozi linaloikumba nchi yetu.Watanganyika wenzangu tuwe makini sana na vyama vya kibabaishaji na vyenye mrengo wa kifamilia zaidi,vinaweza vikatuingiza pabaya kwa kukuabali kununuliwa kwa lengo la kuangamiza upinzani nadni ya nchi yetu.Ni hatari kubwa vinastahili kuogopwa kuliko ukoma.
hivi Kafulila akirudishwa NCCR atakubali kwenda kumuona Rais Kikwete suala la katiba mpya??
 
Mi naona kama uchaguzi utafanyika basi bora wapewe CDM tu, kuepusha mauaji ya wananchi. Akipelekwa Lema tu basi ujue lazima roho zitoke.
 
Hivi Mvungi ali-chair ule mkutano wa kumfukuza Kafulila kama nani ndani ya chama??? Isije ikawa alichea kulinda ukanda maana mbatia na mvungi wanatoka Kilimanjaro.

TZ hakuna democracy nchini na ndani ya vyama

luhanjo na makinda hawajakutosha wewe mnyalu?
 
kuna kazi kubwa sana juu ya haya mambo,japo kijana ni mkosaji lakini nilitegemea wazee wa chama wangeongea nae na uamuzi wa kumvua uanachama ungekuwa wa mwisho kabisa baada ya kushindikana,adhabu hii ni kubwa sana kwa mara moja labda tujulishwe hatua zilizochukuliwa mpaka kufikia hapo.Vijana waangalie na wajiulize sana kabla ya kuingia kwenye migogoro kwa sababu waliopo madarakani katika chama chochote huondolewa kwa utaratibu,ukitumia medani za porini unatakiwa ujidhatiti sana lasivyo yatakukuta ya kafulila na mzee rungwe aliyejitahidi kuzuia zoezi lisifanyike kumbe kachelewa hii ni hatari sana.
 
Napenda nikuhakikishieni kwamba Dr.Mvungi hakuwa mwenyekiti wa mkutano huo. Tanzania tunayo matatizo mengi; hili la uongo na upotoshaji nalo ni kubwa.
Mkuu nashukuru umo humu, binafsi ningependa kujua maoni yako kuhusu kufukuzwa kwa Kafulila na Mzee Rungwe chamani?
 
Tendwa na NEC watupe mchanganuo kwanza 19 bn ni matumizi makubwa sana kwa jimbo moja kufanya uchaguzi.
kama wapiga kura hawafiki laki ipo haja ya ku revisit nia hasa ya wanasiasa manake bajeti ya maendeleo kwa jimbo haifiki hizo digits na value addition ya wabunge wengi haifiki hizo digits.
 
watu wanamsakama Kafulila hawajui kuwa kitendo cha yeye kui-support CDM kutoka nje kwenye sakata la katiba lilionyesha ni jinsi gani ilivyo hatari mbele ya safari kwani upinzani ulianza kuonekana unaweza kuungana na kuipa shida CCM....Wana macho lakini hawaoni; Kafulila asingekuwa threat haya yote yansingetokea vijana unganeni kumsupport kijana mwenzenu muone ni jinsi gani watu watakavyo panic!
 
Back
Top Bottom