Mauaji Kigoma kusini baada ya uamuzi wa Mbatia na genge lake

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Tunapaswa kujifunza demokrasia upya, najiuliza nini maana ya Freedom of expresion?

Tukiwazuia watu kuongea what we call siri katika media ni sawa? Maana kama chama kinarumika na CCM wasiseme? Ukiona Mbatia anafanya jambo ujue wakubwa zake wa kazi wamekwishampa go ahead, katika kesi ya kawe Mh. Mdee na mawakili wake walifanya juhudi hadi muda wa kesi ukaisha bila kesi kusikilizwa, lakini Kombani kawaongezea muda kusikiliza kesi hiyo kwani lazima lirudi CCM kwa kutumia kesi ya Kijana wao Mbatia.

Katika sakata la Kafulila, wajumbe walibadilishwa na nakala ikapelekwa kwa Msajili wa Vyama siku mbili kabla ya NEC ya dharura, Rungwe alipoenda kupinga akakuta Tendwa ana updated list ya Wajumbe na wengine wamefutwa na kuweka wapya ili wapige kura kwa adhma ya kuwafukuza waliompinga Mwenyekiti.

Hiyo haikutosha bali watu walilazimishwa kupiga kura kwa kunyanyua mikono, kwa ile fukuza wajumbe wengi wanakiri kuwa waliogopa na kwa kuangalia maslahi yao waliamua kunyoosha mikono kwa lazima.

Je madai ya Rungwe kuwa Mbatia alimzuia kuisema CCM katika uchaguzi wa mwaka jana ndio yameisha? Rungwe alikiandikia chama barua kulalamikia hatua hiyo, je majibu ya maswali hayo ndiyo hayo?

Kafulila alikataa kwenda kumuona Rais, masaa machache baada ya kufukuzwa chama kimepata mwaliko wa ikulu, je kuna shinikizo toka juu?

Tendwa na Nape wamezungumzia gharama za Uchaguzi mdogo kuwa utakuwa na gharama kubwa, tumeshuhudia katika uchaguzi wa Igunga mauaji na watu kujeruhiwa kutokana na mchakato ule wa uchaguzi, je hatuangalii gharama ya damu za watanzania wenzetu inayoweza kumwagika kigoma kusini kwenye uchaguzi huo mdogo kama ukitokea?

Mauaji hayo nani alaumiwe? Je, damu ya watu watakaopoteza maisha katika uchaguzi wa kigoma kusini kama ukitokea uwe juu ya kichwa cha Mbatia na genge lake?

Je, kuwa na uvumilivu wa kisiasa na kuwajibika katika changamoto zinazokukabili haina faida kubwa kuliko kuweka maisha ya watu katika hatari na kupoteza muda katika chaguzi?

Bilioni 19 zitakazotumika katika uchaguzi zingetumika kulipa madeni ya waalimu, je tatizo s lingepungua?

Tafakari chukua hatua!
 
Ohh god! i hate politics,will never be a politician.Could i live in isolation?God knows
 
siasa ina mambo mengi Kafulila usikate Tamaa jitahidi kuendelea kupambana.Lakini ni muhimu kuanza kufikilia kuanzisha chama kipya kama utashindwa kujinga na vyama vingine si unajua walikataa kabisa suala la mgombea binafsi. Vingi ya vyama nivyao wamevianzisha kwa malengo yao.Malengo yao ni kuhakikisha CCM,inaendelea kutawala tu kwa vyovyote vile. Kulikuwa hakuna haja ya kufukuzana wangeonyana ingetosha.
 
mkuu, umesema mambo mazuri tu, lakini hilo la mauaji kwenye chaguzi ndogo kule Igunga umekosea sana, kwa hiyo damu ile iwe juu ya ccm na Nape waliosababisha Rostam akajivua nafasi ya ubunge???
Kwa hiyo damu ile isiende kwa wauaji bali kwa vyama vilivyosababisha kuwepo na uchaguzi mdogo?

Kwa hiyo kigoma kusini kutakuwa na mauaji? Kitu gani kinachokufanya ufikiri hivyo?
 
Sasa unampinga Mbatia au Kafulila aliyekuwa akilia na kujutia kuwa kamkosea Mbatia? Maana Kafulila kakiri kosa na kujuta tena kwa machozi hadi Mbatia akamuonea huruma na kumuombea msamaha ina maana Mbatia na Kafulila sasa lao moja, kwa hiyo kama Mbatia ni CCM basi Kafulila pia amegive up na kuwa naye ni CCM.

Mnamteteaje mtu aliyekwisha kiri kosa? Tafakari mkuu. Amuombe ushauri rafiki yake Zitto
 
Sasa unampinga Mbatia au Kafulila aliyekuwa akilia na kujutia kuwa kamkosea Mbatia? Maana Kafulila kakiri kosa na kujuta tena kwa machozi hadi Mbatia akamuonea huruma na kumuombea msamaha ina maana Mbatia na Kafulila sasa lao moja, kwa hiyo kama Mbatia ni CCM basi Kafulila pia amegive up na kuwa naye ni CCM. Mnamteteaje mtu aliyekwisha kiri kosa? Tafakari mkuu. Amuombe ushauri rafiki yake Zitto
Kwa mtazamo wangu vyama vya siasa nchini vimeanzishwa kama taasisi binafsi. Tatizo ni pale wanachama wanaposhindwa kutengeneza katiba zinazo ondo Hali hiyo. Tumekua wavivu wa kusoma na kuzielewa katiba za vyama mpaka yaharibike Kama ilivyotokea
 
Sasa unampinga Mbatia au Kafulila aliyekuwa akilia na kujutia kuwa kamkosea Mbatia? Maana Kafulila kakiri kosa na kujuta tena kwa machozi hadi Mbatia akamuonea huruma na kumuombea msamaha ina maana Mbatia na Kafulila sasa lao moja, kwa hiyo kama Mbatia ni CCM basi Kafulila pia amegive up na kuwa naye ni CCM. Mnamteteaje mtu aliyekwisha kiri kosa? Tafakari mkuu. Amuombe ushauri rafiki yake Zitto

Mkuu FIKIRI basi kidogo. magazeti na mitandao yataendelea kuwafikiria mpaka lini?

Watu wanoona mambo kwa picha kubwa wanahoji je NCCR wamefikiria kweli gharama za uchaguzi mdogo na tija lake kwa taifa/, je hakukua na adhabu nyingine mbadala na kuweka utaifa mbele?

Hizo hela zitakazotumika si zingejenga hata barabara KM 15 huko Lindi. Kakosea au hakukosea sio issue hapa. Hapa tunajiuliza uwezo wa viongozi wa NCCR na wajumbe wao.
 
Kwa mtazamo wangu vyama vya siasa nchini vimeanzishwa kama taasisi binafsi. Tatizo ni pale wanachama wanaposhindwa kutengeneza katiba zinazo ondo Hali hiyo. Tumekua wavivu wa kusoma na kuzielewa katiba za vyama mpaka yaharibike Kama ilivyotokea

Hivi Mvungi ali-chair ule mkutano wa kumfukuza Kafulila kama nani ndani ya chama??? Isije ikawa alichea kulinda ukanda maana mbatia na mvungi wanatoka Kilimanjaro.

TZ hakuna democracy nchini na ndani ya vyama
 
huyu kijana (kafulila) kama kweli anataka kufika mbali katika siasa, inampasa atulie na asiwe na tamaa ya madaraka, bali ajifunze njia bora zaidi za kupitia ili aweze kufika mbali, ni kweli mtu ana uhuru wa kuongea mabaya ya chama chake, lakini si kuna vikao vya chama basi la muhimu ni kutumia nafasi hiyo na si kupanga mikakati nje ya chama kumpindua kiongozi wake!
 
NCCR wanatakiwa kukaa na kutafakari upya uamuzi waliouchukua.... wanatakiwa kujiuliza mwananchi wa Kigoma Kusini anafaidika nn au uamuzi wa kumfukuza Kafulila una maslahi gani kwa wananchi wa Kigoma Kusini..... Tafakari chukua hatua.....
 
katika maisha yetu ya kila siku huwezi tenganisha siasa,siasa ndiyo key leader ya mustakabali wa taifa na wananchi wake.Tatizo linalosababisha siasa ionekane mbaya ni viongozi wahusika kuitumia fursa hii au kwa kukandamiza demokrasia ama kuiua kabisa demokrasia.Wengi wetu tunashindwa kujua kuwa hata hivi vyama ni taasisi za umma na si za watu fulani.Vinginevyo wangeanzisha vyama vya kifamilia vyenye mitazamo ya kifamilia zaidi.Haiwezekani hata kidogo chama cha kisiasa kugeuka ni mali ya mtu binafsi.ikifikia hivyo ni hatari sana katika mustakabali wa maisha yetu na nchi yetu.Hatupo katika mfumo wa kikomunisti kuwa na chama cha wateule wachache(vanguard party)

Napenda sana pia kutumia fursa hii kumshauri msajili wa vyama vya siasa nchi kuwa makini,ikibidi kupeleka mapendekezo kwa waziri wa sheria kuangalia upya aina ya vyama vinavyoanzishwa kama vina malengo ya kuwalinda wachache ilikukidhi maslahi yao au vina tija katika mustakabali wa kuwaonyesha njia wananchi.Madiwani wasaliti wa CHADEMA walipofukuzwa ndani ya CDM serikali nzima ilikurupuka kiasi cha waziri wa TAMISEMI kuwakingia kifua kulipwa posho za vikao ili hali akijua kabisa anakiuka na kutoitia katiba ya nchi.Leo hii watusiki msajili wa vyama wala waziri aliyethubutu kulizungumza hili kwa kuwa halina maslahi na chama tawala na serikali yake.Ni hatari sana kwa watu wachache tena waliopandikizwa kumng'oa mbunge wa wananchi wakati wananchi wanamuhitaji katika kupigania maendeleo ya jimbo lake.

mimi kama kijana nimesikitishwa sana na umangimeza huo uliotumika kukandamiza demokrasia na kuvunja katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 18 ya katiba inayosema-kila mtu

(a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake.

Kwanini basi mawazo ya Kafulila yasiheshimiwe na kuwa changamoto katika mustakabali wa kukiboresha chama hicho?Hakuna hata mmoja alizaliwa kuwa kiongozi na atakufa akiwa kiongozi!Kumsulubu Mh. Kafulila ni ombwe la uongozi linaloikumba nchi yetu.Watanganyika wenzangu tuwe makini sana na vyama vya kibabaishaji na vyenye mrengo wa kifamilia zaidi,vinaweza vikatuingiza pabaya kwa kukuabali kununuliwa kwa lengo la kuangamiza upinzani nadni ya nchi yetu.Ni hatari kubwa vinastahili kuogopwa kuliko ukoma.
 
yaelekea mpango wa kafulila ulikuwa umepikwa vizuri sana! Sema mbatia alimzidi kete kidogo sana na ndio maana dogo akatoa chozi
 
Katiba yetu ina vacum kubwa, tunahitaji kurekebisha mapungufu kama haya yanayotuingiza kwenye gharama zisizo na lazima. Maamuzi ya watu wasiozidi 70 yanawaondolea mwakilishi bungeni wananchi wanaozidi elfu 70.
 
Sam ruhuza,,,,kipindi kile cha uchaguzi 2010 alitumwa na Magamba kupunguza kura za upinzani ili mzee ntukamazina ashinde ubunge wa jimbo la ngara...hawa jamaa wa mageuzi ni vibaraka kabisa
 
Kumbe Mbatia alianza zamani ? Je uchaguzi wao hao NCCR uko lini na Mbatia anategemea kuendelea kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti ?
 
Back
Top Bottom