MAUAJI ARUSHA: Tamko la Rais Jakaya Kikwete

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Rais Kikwete leo ametoa tamko lake huku akisikitishwa na tukio la Arusha lililosababisha mauaji ya raia wawili na kuacha mali za mamilioni ya shilingi zikiharibiwa.

Kikwete ameonesha ukomavu mkubwa wa kisiasa tofauti na mtangulizi wake BWM ambaye hakuonesha kusikitishwa na mauaji ya Pemba yaliyopoteza maisha ya watu 27 zaidi ya kuendelea kuwalaumu viongozi wa CUF.

SOURCE: HABARI TBC1
 
Amesikitishwa na nini wakati vijana wake ndio wamefanya hivyo? Na je atachukua hatua gani dhidi ya wauwaji? Bullshit.
 
Amesikitishwa na nini wakati vijana wake ndio wamefanya hivyo? Na je atachukua hatua gani dhidi ya wauwaji? Bullshit.
 
Kama amesema bila unafiki itakuwa amekomaa kisiasa ila kama nikujikosha kwa watu ndiyo mbaya zaidi lakini kinadharia inaonekana kuna mkono wake,kwani kuwepo IGP Mwema ni maagizo kutoka juu.
 
"...Sudan has scored medium in human development in the last few years,[22] ranking #150 in 2009, between Haiti and Tanzania. Statistics indicate that about 17% of the population live on less than US $1.25 per day......." ........hebu ongelea na haya mheshimiwa Rahisi, au bado hujajua kwa nini wewe ni Rahisi??
 
Ni vyema kwa kuwa amesikitika. Inatia moyo ila aoneshe hayo masikitiko kwa vitendo.

1. Amfute kazi IGP Mwema,
2. Amfute kazi Vuai Naodha.
3. Amfutekazi na kumshitaki RPC wa Arusha.
4. Amfutekazi na kumyonga mpaka kufa OCD wa Arusha mjini.
5. Amfute kazi, amshitaki na amfirisi mali zote mkurugenzi wa jiji la arusha aliyeendesha uchaguzi kinyume na taratibu.

Atende haki kwa wote waliohusika katika mauaji hayo (polisi wadogo waliofyatua risasi) kwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani.
 
Kitu ambacho sielewi ni kuwa yanapotokea mabaya wanajaribu kutenganisha CCM na serikali; yakitokea mazuri ya serikali CCM hutamba kuwa ni "serikali ya CCM". Ndio maana sikumuelewa kabisa Vuai jana! Alikuwa anazungumza kana kwamba yaliyofanywa hayahusiani na Chama kilichoko madarakani.
 
Nasikitishwa sana na mauaji hayo lakini viongozi wa siasa hasa za upinzani nao waache UHASIDI kama wa AL-SHABIBY ya somalia. Watumie busara mwafaka kulingana na mazigira husika.
 
Rais Kikwete leo ametoa tamko lake huku akisikitishwa na tukio la Arusha lililosababisha mauaji ya raia wawili na kuacha mali za mamilioni ya shilingi zikiharibiwa.

Kikwete ameonesha ukomavu mkubwa wa kisiasa tofauti na mtangulizi wake BWM ambaye hakuonesha kusikitishwa na mauaji ya Pemba yaliyopoteza maisha ya watu 27 zaidi ya kuendelea kuwalaumu viongozi wa CUF.

SOURCE: HABARI TBC1
Plain hypocrisy. Period.
 
MM naungana na wewe, sasa hivi nikitoa taarifa police kwamba KESHO tunataka kuandamana ili ku support Dowans walipwe pesa zao, nafikiri kibali kitatolewa saa tatu asubuhi na maandamano ruksa. mimi namlaumu moja kwa moja Rais Kikwete kwa haya yote yaliyotokea Arusha.
 
Rais Kikwete leo ametoa tamko lake huku akisikitishwa na tukio la Arusha lililosababisha mauaji ya raia wawili na kuacha mali za mamilioni ya shilingi zikiharibiwa.

Kikwete ameonesha ukomavu mkubwa wa kisiasa tofauti na mtangulizi wake BWM ambaye hakuonesha kusikitishwa na mauaji ya Pemba yaliyopoteza maisha ya watu 27 zaidi ya kuendelea kuwalaumu viongozi wa CUF.

SOURCE: HABARI TBC1

Meanwhile he is very happy that is ofshore company(DOWANs) gonna be paid half openly and another half in secret...sorry folks you have to dig deeper into ya empty pockets in darkness
 
Ni vyema kwa kuwa amesikitika. Inatia moyo ila aoneshe hayo masikitiko kwa vitendo.

1. Amfute kazi IGP Mwema,
2. Amfute kazi Vuai Naodha.
3. Amfutekazi na kumshitaki RPC wa Arusha.
4. Amfutekazi na kumyonga mpaka kufa OCD wa Arusha mjini.
5. Amfute kazi, amshitaki na amfirisi mali zote mkurugenzi wa jiji la arusha aliyeendesha uchaguzi kinyume na taratibu.

Atende haki kwa wote waliohusika katika mauaji hayo (polisi wadogo waliofyatua risasi) kwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani.

kaka hana uwezo wa kufanya haya yote, kwanza ndiye aliyeagiza Mbowe na DR. Slaa wakamatwe. tuna kiongozi asiyepima upepo.

Mlio karibu naye mwambieni wiki ijayo tunaandamana kupinga Dowans kulipwa mabilioni, sasa mwambieni atafute magari mengi zaidi ya upupu na risasi aagize mapema.
 
Alikuwa akiwahutubia mabalozi wa nchi za nje hapa Tanzania alipowaalika leo kwenye chakula cha kuwatakia heri ya Mwaka Mpya

Source: Taarifa ya habari ya saa 2 usiku TBC1

My take:
Hili jambo linamuuma JK kama maumivu ya kidole kilichobanwa na mlango. amegundua madhara yake kwenye uongozi wake na mapato yake, kwa kuwa hutegemea sana wahisani na wawekezaji kuendesha nchi.

Amegundua kwamba hawezi tena kuzurura nchi za watu akijisifu kwamba Tz ni nchi ya amani na demokrasia

Amegundua kwamba sasa hata nchi za kimataifa zimeshutuka kwamba inawezekana kwamba yeye siyo mshindi halali wa urais. mara nyingi ni vigumu kupata tukio la kishindo namna ile kutoka upinzani kwa nchi ambaye rais kweli ameshida kwa asilimia 60+

Amegundua kwamba polisi ni wataalamu wa kutekeleza maagizo ya wanasiasa ili wapate sifa na kubaki katika vyeo vyao. Anajuta kuingia ubia na polisi kudhibiti upinzani!

Kwa maneno mengine, JK ametangazia ulimwengu kwamba amekoma, hatarudia tena!! Lakini, kwa nini atangazie mabalozi wa nchi za nje badala ya kutangazia wananchi na kuwaomba radhi moja kwa moja? Nani mwenye thamani kwake?
 
Anasanifu tu watu, wala hana uchungu wowote. sanasana ameonekana kuhofia mali zlzopotea...sijaona km ana jipya.
 
Kitu ambacho sielewi ni kuwa yanapotokea mabaya wanajaribu kutenganisha CCM na serikali; yakitokea mazuri ya serikali CCM hutamba kuwa ni "serikali ya CCM". Ndio maana sikumuelewa kabisa Vuai jana! Alikuwa anazungumza kana kwamba yaliyofanywa hayahusiani na Chama kilichoko madarakani.

Ninachojiuliza kila siku ni upi uwezo wa viongozi wetu kifikiri boldly. Kuna mambo ukiyafanya lazima utatengeneza martyrs. Sasa iweje leo wadanganye kwamba hawajui hali ile ya Arusha imetokeaje? Namheshimu sana RPC wa Arusha aliyeondolewa kwa mizengwe ya uchaguzi. Leo hii anasimama kando ya wote ndani ya jeshi la polisi wasiotaka kutumia akili zao aking'ara kwa kutukuka.

Ipo siku nchi hii itawanyanyua watu wa aina ile na kuwaweka sehemu wanayostahili maana walijua wanachofanya. Wale ambao wana vichwa halafu wanafikiri kazi ya kichwa ni kubebea mabox na sio kufikiri, I wish them all the best.

Their days are numbered.
 
Rais Kikwete leo ametoa tamko lake huku akisikitishwa na tukio la Arusha lililosababisha mauaji ya raia wawili na kuacha mali za mamilioni ya shilingi zikiharibiwa.

Kikwete ameonesha ukomavu mkubwa wa kisiasa tofauti na mtangulizi wake BWM ambaye hakuonesha kusikitishwa na mauaji ya Pemba yaliyopoteza maisha ya watu 27 zaidi ya kuendelea kuwalaumu viongozi wa CUF.

SOURCE: HABARI TBC1

Amesikitishwa na nini? Hii ni danganya toto tu. Watanzania hatujasahau alipowatisha TUCTA walipotaka kuandamana kwa kuwaambia wangekumbana na nguvu ya dola na kwamba polisi wangewatandika sawasawa. Polisi walichokifanya Arusha ndiyo maelekezo yake. JK asiwapige changa la macho watanzania. Kama ansikitika kweli, basi afanye kama Magafu alivopendekeza.
 
Eeeh yaani huo unafiki uliofanyika mbele ya wanadiplomasia wa kimataifa ndiyo ukomavu wa kisiasa baada ya kuibaka demokrasia kazi ipo.
Nadhani yakupasa utafakari kwa kina ikibidi ufute hiyo kauli.
 
Amesikitishwa na nini wakati vijana wake ndio wamefanya hivyo? Na je atachukua hatua gani dhidi ya wauwaji? Bullshit.
Kikwete ni mnafiki mkubwa sana, kuonyesha kusikitika ni kutaka kuwaaminisha watanzania kwamba yeye hausiki
na kutaka kuwapoza wananchi ambao tayari wameonyesha kutokuwa na imani na CCM, Kweli bado viongozi wanawaona watanzania ni wajinga.
 
Back
Top Bottom